Modi kamchana live Puttin uso kwa uso bila kupepesa macho

Kabla ya OP ya Russia hapakuwa na uagizwaji wa mafuta na gesi? Kwann sasa uagizwaji iwe ni unafiki?
Una fahamu kila siku zelensky ana lia kisa nini ? Kila uchwao zelensky anaomba Russia awekewe vikwazo zaidi vya kiuchumi vitakavyo mfanya asimamishe OP yake hapo Ukraine na vikwazo alivyo pendekeza bwana Zelensky ni mataifa kuacha kuagiza mafuta Russia je India imefanya hivyo au ndio imeongeza zaidi uagizwaji wa mafuta Russia tofauti na miaka ya awali alafu leo huyo PM wao anakuja kumuambia Putin aache unafiki aanze kwanza yeye apige stop mafuta ya Russia hapo ndipo nitamuelewa Ila asipo fanya hivyo yeye ndiye kiongozi wa unafiki.

: Zelensky alisema mafuta ya Russia ni damu za waukraine maana yake ni kuwa India inaendelea kufadhili umwagaji damu pale Ukraine sasa mtazame nani mnafiki hapo Kati ya Russia au India.
 
Hahahaha!

India hii hii maika ya 1950s wakati US alipopeleka meli zake za kivita ili aiadabishe India ikawa haijui nini cha kufanya mpaka wakaomba msaada Moscow!

US kushtuka anaona nyambizi ya Russia inaibuka mbele yao karibu na India na meli za US kurudi nyuma na India kupona!? Hahaha

Hahahaha!

Halafu Putin hakujibu hivyo na wala Mondi hakusema kwa maudhui uliyoweka humu jamvini Mkuu! Video zipo Mzee sijui unapata raha gani kutoa habari ya uongo!
 
Hakuna anaye pinga kuhusu uhusiano wa kibiashara baina ya Russia na India , ila unafiki ni hayo maneno ya PM huku yeye mwenyewe akiwa supporter mkubwa wa OP ya Russia hapo Ukraine kupitia uagizwaji mkubwa wa mafuta na gas unao fanywa na India kitu kinacho mfanya Russia kupata pesa za kendesha OP yake pia India chini ya PM Modi mpaka sasa haija pinga wala kulaani OP ya Russia hapo Ukraine huu pia ni unafiki wa India na PM modi , aache unafiki awe straight kama Xi Jinping .
China kajifunza pakubwa alichofanyiwa na Pelonsi kuwa kibarua kilichopo mbele yake ni cha namna gani! Haikuishia hapo wajumbe wengine wa NATO wakapeleka viongozi wao Taiwan. Haikuishia hapo wajumbe wengine wa EU vilevile wakapeleka viongozi wao Taiwan kwa rasmi kuwa wanaitambua Taiwan ni ardhi huru. Akili ikamkaa China pakubwa ni aina gani ya watu anaopambana nao.

India msimamo wake hafungamani na popote. Popote penye maslahi na nchi yake anatia mguu. Nafikiri wameicheza kidiplomasia zaidi ili kuepuka pressure kubwa zaidi kutoka kwa US.
 
Putin ni mbabe kichwani box, wenzake wanawaza pesa. Vita waachie wapumbavu
Kama US vita inazopambana ni faida kwa uchumi wake na Russia kwake ni faida kwao. Kwako kinaweza kikawa kizuri kwa wengine kibaya. Kila mtu ana maslahi yake! Maadamu Russia imechagua kwao imeona ni maslahi kwao itabakia hivyo! Lakini ukumbuke kaifanya EU wanakata kuni kwa kujiandaa na winter, bili za umeme kupanda na viwanda kufungwa. Ama kwa hakika Putin ni kichwa boksi!
 
Hong kong ipo china ila kwa jinsi USA alivyowekeza hong kong machawa wengi wa USA wapo mule.
Ase nilikuwa nimeisahau South Korea huyo nae chawa namba moja.
India usimwamini hadi kesho yule ni chawa wa USA
Hong Kong hapamtii China shida! Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi wakati UK inairudisha Hong Kong kwa China makubaliano ni kuwa itakuwa chini ya China lakini itajitegemea mfumo wake wa kujiendesha kwa miaka 50.

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa Hong Kong imerudi kwa China mwaka 1999. Miaka miaka ishirini naa imebaki hivyo Mchina hana shida. Wenye shida watakuwa hao machawa wa west.
 
sio chawa , hayo ni mataifa yanajielewa , Na ndio maana yameendelea sana kweny kanda hizo , hata china alipokuwa chawa wa USA ndipo alipiga hatua sana
 
China kajifunza pakubwa alichofanyiwa na Pelonsi kuwa kibarua kilichopo mbele yake ni cha namna gani! Haikuishia hapo wajumbe wengine wa NATO wakapeleka viongozi wao Taiwan. Haikuishia hapo wajumbe wengine wa EU vilevile wakapeleka viongozi wao Taiwan kwa rasmi kuwa wanaitambua Taiwan ni ardhi huru. Akili ikamkaa China pakubwa ni aina gani ya watu anaopambana nao.

India msimamo wake hafungamani na popote. Popote penye maslahi na nchi yake anatia mguu. Nafikiri wameicheza kidiplomasia zaidi ili kuepuka pressure kubwa zaidi kutoka kwa US.
Nimependa namna China anavyo “win game” ni akili tu anatumia kuwin hili game wanalo mchezea west. Na uziri au advantage aliyo nayo China ni makubaliano ya UN 1971 na makubaliano yake na U.S.A 1979 kwamba marekani anaitambua Taiwan kama sehemu ya China hii ni faida kubwa kwa China kuliko U.S.A . Marekani akitaka kufanya uhuni wa kuitambua Taiwan Kama nchi huru lazima avunje makubaliano ya 1971 & 1979. Na mataifa mengine duniani pia yanaitambua Taiwan kama sehemu ya China makubaliano ya 1971 yana wafunga minyororo. Maana yake “One China Policy” ni faida kwa PRC.

: China akili mingi sana hawa mabwana, bado vita ya uchumi ana mkimbiza U.S.A balaa.
 
Kama US vita inazopambana ni faida kwa uchumi wake na Russia kwake ni faida kwao. Kwako kinaweza kikawa kizuri kwa wengine kibaya. Kila mtu ana maslahi yake! Maadamu Russia imechagua kwao imeona ni maslahi kwao itabakia hivyo! Lakini ukumbuke kaifanya EU wanakata kuni kwa kujiandaa na winter, bili za umeme kupanda na viwanda kufungwa. Ama kwa hakika Putin ni kichwa boksi!
Italy & Germany mambo yame zidi kuwa magumu balaa kwa Viwanda , migahawa na kwenye makazi ya watu nishati haishikiki shughuli nyingi sana zitafungwa.
 
Akiacha hiyo vita Putin itakua poa sana watu wanapata tabu bila sababu za msingi..Modi huwa ananyoosha maneno na Putin alitegemea atapata msaada kutoka China na India sasa anaona marafiki zake wakimkataa kuendelea na hiyo vita...mimi naomba leo au kesho wasitishe Dunia irudi kwenye ustaarabu wake wa kawaida hizo mambo za kizamani zilishapitwa na wakati..
 
"have spoken to you on the phone about this," Modi told Putin, according to Reuters.
Putin told the Indian leader, "I know about your position on the conflict in Ukraine, and I know about your concerns".

Putin anatamani amalize vita hata leo ila concern yake kubwa ni nani tena atanunua mavyuma vyuma yake baada ya kuiaminisha dunia kwa kipindi kirefu kuwa ana dhana kazi bora kuliko hasimu wake mkubwa😂.
Mimi nilipomsikia majuzi anapiga kelele eti ana zana bora za kivita iliyo miaka 10 mbele kitechnologia zaidi ya nchi za magharibi na marekani nikajua, tayari kaisha receive negative feedback kutoka kwa wateja wake juu ya muelekeo wa kibiashara wa hayo mavyuma yake.
 
Nimependa namna China anavyo “win game” ni akili tu anatumia kuwin hili game wanalo mchezea west. Na uziri au advantage aliyo nayo China ni makubaliano ya UN 1971 na makubaliano yake na U.S.A 1979 kwamba marekani anaitambua Taiwan kama sehemu ya China hii ni faida kubwa kwa China kuliko U.S.A . Marekani akitaka kufanya uhuni wa kuitambua Taiwan Kama nchi huru lazima avunje makubaliano ya 1971 & 1979. Na mataifa mengine duniani pia yanaitambua Taiwan kama sehemu ya China makubaliano ya 1971 yana wafunga minyororo. Maana yake “One China Policy” ni faida kwa PRC.

: China akili mingi sana hawa mabwana, bado vita ya uchumi ana mkimbiza U.S.A balaa.
Na balaa lengine kubwa alilofeli US ni kuifanya Russia na China kuungana. Juzi Xi Jinping katangaza wazi msimamo wa China kuwa wanaiunga mkono Russia.

Chini ya Biden sera za US zimefeli pakubwa sana. Kuwaweka pamoja mahasimu wawili mmoja ana nguvu kubwa ya kijeshi na mwengine ana nguvu kubwa ya kichumi. China kwa sasa hivi anapata gesi nyingi na kwa bei ndogo kutoka Russia kwa maana viwanda vitafanya uzalishaji mwingi kwa ubora mkubwa kwa bei ndogo tofauti kwa EU. Kwenye soko hapo umeshawakalisha.

Bomba jengine la usafirishaji wa gesi linatoka Russia kinapitia Mongolia mpaka China. Uchumi unahamia mashariki ya mbali ya Asia kwa sababu mfumo wa energy/nishati unahamishiwa huko. Hii inapelekea kuanzishwa kwa mifumo mipya ya miamala ya kibiashara kwa pande hizo. Hivyo Russia na China watavuna zaidi. Kujiimarisha kwa ukubwa wa namna hii ni pigo kubwa sana kwa US. Ikiwa Russia atashinda hii SMO inayoiendesha nchini Ukraine itakuwa ni pigo kubwa sana kwa EU na US kwa sababu nguvu ya ushawishi, nguvu za kijeshi na kiuchumi zitahama.

Naam, nakubaliana na wewe! China inatumia akili kubwa sana kupambana na US. Naionea huruma Taiwan. Hii operation Russia ikishinda ndani ya miaka 5 mbeleni Taiwan itavamiwa kijeshi. CIA hili wameshaliona na ndiyo maana ripoti yao inasema 2027 China inapanga kuivamia kijeshi Taiwan. Lakini kwa bahati mbaya viongozi wa Taiwan hawalioni hili! China itawadhalilisha pakubwa!
 
Hong Kong hapamtii China shida! Kama kumbukumbu zangu zipo sahihi wakati UK inairudisha Hong Kong kwa China makubaliano ni kuwa itakuwa chini ya China lakini itajitegemea mfumo wake wa kujiendesha kwa miaka 50.

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa Hong Kong imerudi kwa China mwaka 1999. Miaka miaka ishirini naa imebaki hivyo Mchina hana shida. Wenye shida watakuwa hao machawa wa west.
Upo sahihi mkuu . marekebisho kidogo Hongkong ilirudi 1997 na Macau 1999.
 
Na balaa lengine kubwa alilofeli US ni kuifanya Russia na China kuungana. Juzi Xi Jinping katangaza wazi msimamo wa China kuwa wanaiunga mkono Russia.

Chini ya Biden sera za US zimefeli pakubwa sana. Kuwaweka pamoja mahasimu wawili mmoja ana nguvu kubwa ya kijeshi na mwengine ana nguvu kubwa ya kichumi. China kwa sasa hivi anapata gesi nyingi na kwa bei ndogo kutoka Russia kwa maana viwanda vitafanya uzalishaji mwingi kwa ubora mkubwa kwa bei ndogo tofauti kwa EU. Kwenye soko hapo umeshawakalisha.

Bomba jengine la usafirishaji wa gesi linatoka Russia kinapitia Mongolia mpaka China. Uchumi unahamia mashariki ya mbali ya Asia kwa sababu mfumo wa energy/nishati unahamishiwa huko. Hii inapelekea kuanzishwa kwa mifumo mipya ya miamala ya kibiashara kwa pande hizo. Hivyo Russia na China watavuna zaidi. Kujiimarisha kwa ukubwa wa namna hii ni pigo kubwa sana kwa US. Ikiwa Russia atashinda hii SMO inayoiendesha nchini Ukraine itakuwa ni pigo kubwa sana kwa EU na US kwa sababu nguvu ya ushawishi, nguvu za kijeshi na kiuchumi zitahama.

Naam, nakubaliana na wewe! China inatumia akili kubwa sana kupambana na US. Naionea huruma Taiwan. Hii operation Russia ikishinda ndani ya miaka 5 mbeleni Taiwan itavamiwa kijeshi. CIA hili wameshaliona na ndiyo maana ripoti yao inasema 2027 China inapanga kuivamia kijeshi Taiwan. Lakini kwa bahati mbaya viongozi wa Taiwan hawalioni hili! China itawadhalilisha pakubwa!
Kweli kabisa China kuichukua Taiwan sio sasa mpaka miaka 2025 na kuendelea huko ndipo wanaweza kufanya hicho kitu. Mkutano wa juzi wa SCO umeyavuta mataifa mengi sana Iran na Turkey nao wanataka kujiunga na huo ushirikiano wa kiuchumi hapa Russia na China Wana win tena na wanapendekeza kila taifa kutumia pesa yake kwenye biashara napo BRICS inazidi kuongeza matawi . Pia bomba la mafuta na gas lengine kutoka Russia mpaka China linajengwa by 2023 litakuwa limekamilika . Hawa mabwana Russia na China huku kwenye Vita vya uchumi wana upiga mwingi balaa.
 
Italy & Germany mambo yame zidi kuwa magumu balaa kwa Viwanda , migahawa na kwenye makazi ya watu nishati haishikiki shughuli nyingi sana zitafungwa.
Waziri Mkuu wa Hungary anasema kwa mwendo wanaokwenda nao EU kwa hali ya namna hii ikifika winter 40% ya viwanda vitafungwa. Hili kwa hakika ni pigo kubwa!

Juzi ama jana aliwakumbusha viongozi wenzake wa EU kwamba: Siku zote vikwazo vinawekwa kutoka kwa mkubwa kwenda kwa mdogo. Sisi (EU) tunaweka vikwazo kutoka mdogo kwenda kwa Mkubwa (Russia) ambaye ndiye injini wa mfumo wa nishati kwao.

Wao wanataraji utunishaji wa misuli yao itamaliza mgogoro huu Russia vs Wao kwa kinachoendelea Ukraine. Russia kwa kuligundua hili kairefusha operation kwa sababu hasara zaidi itakuwa kwa EU. Sasa sijui hii winter Russia itawafanyia nini? Huku Russia inawekeza pakubwa uchumi wake mashariki ya mbali ya Asia, Afrika na bara Amerika ya kusini.
 
Kweli kabisa China kuichukua Taiwan sio sasa mpaka miaka 2025 na kuendelea huko ndipo wanaweza kufanya hicho kitu. Mkutano wa juzi wa SCO umeyavuta mataifa mengi sana Iran na Turkey nao wanataka kujiunga na huo ushirikiano wa kiuchumi hapa Russia na China Wana win tena na wanapendekeza kila taifa kutumia pesa yake kwenye biashara napo BRICS inazidi kuongeza matawi . Pia bomba la mafuta na gas lengine kutoka Russia mpaka China linajengwa by 2023 litakuwa limekamilika . Hawa mabwana Russia na China huku kwenye Vita vya uchumi wana upiga mwingi balaa.
Trump aliligundua hili na ndiyo maana akaamua kumfanya mmoja adui na mwengine rafiki. Aliamua kupambana na China ambaye kiuchumi ni tishio kubwa kwa US. Aligundua kuwa China analinda sana uchumi wake kuliko Russia hawezi kukubali umtie kidole machoni lazima kitawaka. Sasa ili uwawin wavuruge wasiwe pamoja. Wanawakati mgumu sana US. Si china wala Russia itawaamini kwenye mambo ya kulinda mustakabali wa uchumi na usalama wa mipaka ya nchi zao. Hatua walizozichukua dhidi ya Russia kwenye hii operation dhidi ya Ukraine ni mbaya sana kitaswira ya kimataifa.
 
Waziri Mkuu wa Hungary anasema kwa mwendo wanaokwenda nao EU kwa hali ya namna hii ikifika winter 40% ya viwanda vitafungwa. Hili kwa hakika ni pigo kubwa!

Juzi ama jana aliwakumbusha viongozi wenzake wa EU kwamba: Siku zote vikwazo vinawekwa kutoka kwa mkubwa kwenda kwa mdogo. Sisi (EU) tunaweka vikwazo kutoka mdogo kwenda kwa Mkubwa (Russia) ambaye ndiye injini wa mfumo wa nishati kwao.

Wao wanataraji utunishaji wa misuli yao itamaliza mgogoro huu Russia vs Wao kwa kinachoendelea Ukraine. Russia kwa kuligundua hili kairefusha operation kwa sababu hasara zaidi itakuwa kwa EU. Sasa sijui hii winter Russia itawafanyia nini? Huku Russia inawekeza pakubwa uchumi wake mashariki ya mbali ya Asia, Afrika na bara Amerika ya kusini.
Jamaa kwenye swala la vikwazo wangetulia kwanza sio ile mihemko walio fanya unapo dili na mataifa makubwa kama U.S.A, Russia na China usitumie nguvu na mihemko tumia akili nyingi walimuwekea vikwazo vingi Russia mwisho wa siku imefika zamu yake Russia kupiga vya kwake tena vina umuhimu kwao balaa sasa hivi wamebaki kulalama kuwa Russia anatumia gas kama silaha ya kuwaumiza EU wamesahau vikwazo vyao walivyo muwekea Russia.

Hii kitu Ina nikumbusha trade war 2018 kati ya U.S.A na China Trump alionywa kuhusu tarrifs kwa bidhaa za China hakutaka kusikia kilicho fuata ni maumivu kwa U.S.A mpaka akaomba kukutana na Xi Jinping tena na kuweka mambo sawa .

Haya mataifa ya China na Russia watu wasiya chukulie poa yana ongozwa na watu wenye akili nyuma yao ukimuondoa Xi Jinping na Vladimir Putin hata U.S.A ana tambua hilo , Ila humu jukwaani watu wanaya chukulia poa Sana.
 
Back
Top Bottom