Modi kamchana live Puttin uso kwa uso bila kupepesa macho

Yaani kwa sasa naona kabisa uhusiano kati ya Russia na China umekuwa maradufu tofauti na awali kitu ambacho ni kibaya zaidi kwa U.S.A .

Mimi kwa sasa napenda kuona namna cooperation mbalimbali zilizo anzishwa na China na Russia zinavyo zidi kuimarika mara dufu na mataifa mbalimbali yana omba kujiunga nazo huu ni ushindi mkubwa sana kwa China na Russia.
 
Mbaya zaidi kawawekea vikwazo kwenye bidhaa za kimataifa (gesi&mafuta) wanalipia kwa Ruble. Matokeo yake EU thamani ya pesa yao inashuka.

Walikurupuka kwa kweli.
 
Mbaya zaidi kawawekea vikwazo kwenye bidhaa za kimataifa (gesi&mafuta) wanalipia kwa Ruble. Matokeo yake EU thamani ya pesa yao inashuka.

Walikurupuka kwa kweli.
Walikurupuka sana Italy kiongozi wa upinzani anaye pinga vikwazo kwa Russia pia anapinga Italy kujihusisha na hii vita kitu ambacho katiba ya Italy ndivyo inavyotaka jamaa anapata uungwaji mkubwa sana wa raia wa Italy .

Russia na China huu muunganiko utawa sumbua sana west .
 
Hakika!

Kuna kitabu kimoja kama kumbukumbu zangu zipo sawa kinaitwa "the clash of civilisation) kipo sipo sahihi utanisahihisha.

Mwandishi wa hicho kitabu anasema: west wanaitawala dunia si kwa sababu ya akili sana ama teknolojia sana. Bali ni kwa umahiri wa kuanzisha vikundi vya kiuhalifu pale wanapoona hatarishi ya maslahi yao.

Nahofia kwa nchi nyengine hizi za kati kwa kati sijui zitachukua maamuzi gani! Afrika tumeshapigwa biti! Rais wa Serbia kila mara anazungumza vitisho anavyovipata kutoka kwa West.

Sijui itakuwaje, ngoja tuone!
 
Na ndio maana Taiwan haitambuliki Umoja wa Mataifa (UN) inawakilishwa na PRC (People's Republic of China)
 
On top of that., Russia ana wanajeshi majeruhi karibu 80,000 lakini waliouliwa pia kwa ripoti za hivi karibuni ni takriban 54,300, Upande wa putini ndio wenye maumivu zaidi
 
West wana ujinga mwingi sana sera zao za mambo ya nje ni mbovu sana , kwangu Mimi nawaona ushindani wa kiuchumi & kibiashara hawezi zaidi ya figisu za vikundi na uchochezi wa vita vya ajabu mtazame U.S.A anacho fanya Taiwan na alicho kuwa anataka kufanya Xinjiang namna NATO ilivyo kuwa ina expand kwenda Russia . Hizi ni figisu za kijinga sana fanya biashara ukishindwa buni mbinu mbadala kuweza.

Africa tuna safari ndefu sana tukubali tukate ila inabidi viongozi na raia wa huku kwetu kufunga mikanda na kupambana hatuna namna .Elimu bora tuipe kipaumbele huu ndio ukombozi wa kweli kwa mwafrika na Afrika . Tujiunge na Cooperation mbalimbali za kimataifa za kiuchumi kama afanyavyo SA. ningependa kuona Tanzania tunaomba ushirikiano wa kimataifa wa kibiashara na cooperation mbalimbali ikiwemo SCO, BRICS n.k
 
Ni ngumu sana. China anacheza hili game kwa akili sana. Marekani ndo anatapatapa. Chinese are so smart
Wale mabwana kwanza kuhusu namna walivyo lihandle swala la bi. Pelosi daah nikashangaa sana pili ziara za viongozi mbalimbali wa U.S.A Taiwan zilizo fuatia jamaa waliendelea kutulia tu. hii ni hesabu nzuri sana walipiga, kudeal na marekani inabidi utumie akili pale wao wanapo tumia nguvu.

Wachina wanaupiga mwingi sana kwenye vita vya kiuchumi dhidi ya U.S.A mpaka sasa marekani anazidi kutapata kwa maamuzi ya kijinga anayo chukua kuhusu Taiwan.
 
Mara anataka amuuzie silaha kali sijui ndege za kivita mara sijui kuwatrain wajeshi wa Taiwan, mara wanafikiria vikwazo vya kumwekea China endapo ataovamia Taiwan

Yaani anatapatapa tu Mmarekani
 
China inapigana na nani vita vya Uchumi?
 
Marekani inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa wahamiaji kuliko taifa lengine kutoka pande zote za dunia.
Kwa ground mambo ni tofauti sana.
 
 
Kama Russia na China yanaongozwa na watu wenye akili basi US na Ulaya wanaongozwa na ma-genius.
 
Una uelewa mdogo sana kuhusu Geopolitics.
Sera kubwa ya China ya mambo ya nje ya kutuuzia earphones, toothpicks, vitana, kuchukua tenda kubwa kubwa za kujenga barabara na vibarua kutoka kwao huku kampuni za wazawa wakitoa tu macho wewe ndio unaona sera bora ya mambo ya nje??

Inasikitisha kufurahia Africa kuwa dampo la bidhaa hafifu za wachina na sehemu za kujaza wachezesha kamari wa Kichina.
Ujamaa ni laana hakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…