Mathanzua
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 17,251
- 22,929
Najisi always ni neno ambalo lili-imply kitu ambacho kinaharibu uhusiano kati ya wana wa Israel na Mungu kufuatana na Torati.Hata hivyo Sheria za Torati ambzo ni 613 zilikuwa za muda tu,na Biblia inasema ziliingizwa kwa sababu ya makosa(Wagalatia 3:19),ili aje mkombozi Bwana Yesu,ambaye yeyote atakaye mwamini atahesabiwa haki kwa imani katika Yeye.This was God's original plan,lakini Shetani kwa kumdanganya Hawa akaharibu God's original plan.Mnyama akiitwa ' najisi' maana yake ni nini ?.... Kwenye hiyo mistari ya mambo ya walawi nguruwe ametajwa kama 'najisi' na tena mtu akila atakuwa 'najisi' mpaka jioni.
Mambo ya Walawi 11 7
Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.
Mambo ya Walawi 11 24
Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;
Mambo ya Walawi 11 25
na mtu awaye yote atakayechukua cho chote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni.
Kwa maelezo hapo juu ni kwamba ukila nguruwe mchana utakuwa najisi siku nzima mpaka jioni tu au nimekosea ?
Tofautisha maneno najisi na haramu
"Najisi" na "haramu" ni misamiati inayotumika katika muktadha tofauti, hasa katika lugha za kidini kama vile Kiislamu.
1. Najisi:
- Ni muktadha wa kitu kuwa na uchafu au unajisi, mara nyingi kutokana na mambo kama vile uchafu wa kimwili au kitu kuhusishwa na kitu kinachokataliwa kulingana na imani au desturi.
- Mara nyingine, katika lugha za kidini, "najisi" inaweza kutumika kumaanisha kitu kinachotakiwa kuepukwa au kutakaswa.
2. Haramu:
- Ni kitu au tendo ambacho kimeharamishwa au kisichoruhusiwa kufanywa, kwa kawaida kulingana na mafundisho ya dini au sheria.
- Mara nyingine, "haramu" inaweza kutumika kumaanisha jambo lisiloruhusiwa kufanywa na inaweza kuhusisha mambo ya kisheria au ya kidini.
Kwa kifupi, "najisi" ni zaidi kuhusu uchafu au kitu kinachokataliwa kutokana na sababu fulani, wakati "haramu" ni kuhusu kitu au tendo ambalo limepigwa marufuku kufanywa kwa mujibu wa mafundisho au sheria.
zitto junior Mathanzua FaizaFoxy
Kwamba Torati haikuwa kitu cha kudumu is proved by the following verses.
i.Mwanzo 9:3
3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.
Mwanzo 9:3
ii.Wagalatia 3:17
17 Nisemalo ni hili; agano lililothibitishwa kwanza na Mungu, torati iliyotokea miaka mia nne na thelathini baadaye hailitangui, hata kuibatilisha ile ahadi.
iii)Marko 7:18-21
18 Akawaambia, Hivi hata ninyi hamna akili? Hamfahamu ya kwamba kila kitu kilicho nje ya mtu, kikimwingia, hakiwezi kumtia
19 kwa sababu hakimwingii moyoni, ila tumboni tu; kisha chatoka kwenda chooni? Kwa kusema hivi alivitakasa vyakula vyote.
20 Akasema, Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi.
21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
Kwa hiyo kufuatana na maandiko hayo,kwa Wakristo sasa hakuna kitu najisi,if you want to eat anything it is okay,ili mradi tu kisikwaze a new convert ambaye imani yake haijajengeka vizuri.Waislamu pia wànatumia neno hili,na maana yake ni ile ya kwenye Torati,isipokuwa kwenye Torati they go farther.Waislamu wao mahiri ni nguruwe tu,vingine ruksa.
Na haramu?Hili ni neno ambalo sisi wana wa Mungu hatulitumii,linatumika sana kwa Waislamu na vyombo vya Sheria.Kote kote lina maana ya kitu kinachokatazwa au kisichokubalika kidini na kisheria.