Moja ya mambo yanayochangia migogoro kwenye ndoa nyingi ni wanaume kuingia kwenye ndoa wakitarajia wake zao kuwasaidia majukumu yao

Moja ya mambo yanayochangia migogoro kwenye ndoa nyingi ni wanaume kuingia kwenye ndoa wakitarajia wake zao kuwasaidia majukumu yao

Alimpa msaidizi na alimpa majukumu yake kuzaa kwa uchungu na Hilo ni jukumu ambalo hakuna mwanaume anaweza kumsaidia

Na mwanaume alipewa jukumu la kafanya kazi ahudumie familia
Kwa maana nyingine mwanamke hapaswi kufanya kazi sio?

Yaani asubiri kuzaa Kwa uchungu na kulea familia.
 
Naamini kuna mambo mengi yanayochangia migogogoro na kuvunjika kwa ndoa nyingi kwa wakati huu

Ila Naomba nielezee hii sababu majawapo ambayo ni
Wanaume wengi au vijana pengine niwaite wavulana kuingia kwenye ndoa wakidhani wanawake wao watawasaidia baadhi ya majukumu na wengine wajinga wakitamani wasaidie hata majukumu yote

Kigezo kikubwa kwa mwanaume na jukumu la kwanza ni kuoa mwanamke anayempenda na kumvutia kwa asilimia kubwa tabia sura na hata maumbile
Na hapa tunatofautiana Kila mtu ana tabia sura na maumbile yanayomvutia

Ukifanikiwa kwenye kigezo na jukumu la kwanza hayo mengine yote ni rahisi

Jukumu la pili na muhimu ambalo wanaume wengi haswa wa wakati wanalikimbia wakidhani watabaki salama ni
Kumuhudumia mke wako kwa Kila kitu kuanzia Nguo yake ya NDANI mavazi ya nje mahitaji yote muhimu kwa mwanamke ni jukumu la mwanaume kumuhudumia

Tatu mahitaji yote ya familia ni jukumu la mwanaume kuhudumia hata Kama mwanamke ana mshahara ana hiari ya kuchangia mahitaji ya familia au la

Hata akichangia weka akilini mwako kwamba anakusaidia majukumu yako usibweteke,
Siku akijisikia kutochangia Basi ukubaliane na hali na umshukuru walau kwa kile alichochangia

Kwenye maandiko jukumu la mwanamke kubwa ni uzazi na kumtii mume wake

Ukiona mwanaume ambae kigezo chake kikubwa anataka mwanamke mwenye kazi au mshahara au mpambanaji hiyo ni dalili ya hao wanaume

Nashauri hakikisha unakuwa na msingi mzuri wa kipato kabla ya kuoa Bora uchelewe kuoa ili
Uoe mwanamke unayempenda na mwenye uwezo wa kumuhudumia
Kwa asili
Wanawake hawaji kuongeza kipato Ila kutumia kile kipato chako

Uanaume ni kazi Sana na uwajibikaji wake ni mkubwa
Sio rahisi kuwa mwanaume na Wakati mwingine kuwa baba wa familia
Nikiwa Japani some years ago, nilimualika Binti wa kijapani (baby) tukale piza kwenye piza shop. Tulipo maliza kula akachukua menu, then akatoa nusu ya cost. Nilijaribu kumsihi asifanye hivyo mie ndo nilimualika aligoma. Nikalipa nusu ilobaki tukasepa. Ole wenu wabongo na hizo mentality zenu, akialikwa na kijana wa kiume (girlfriend or boyfriend) for outing, beba na hela ya kulipia nusu ya bili. Ukienda na mentality za kiafrika utaumbuka.
 
Pesa za mkewe hazimuhusu
Dini ina hesabu ni moja ya mali zako! Ata matumizi yake ni wewe unatakiwa kuyapangia Au kuelekeza

Kumsaidia mzazi ni wewe kwa ruhusa yako!

Hivyo kuoa na kutoa mahari ni kufanya manunuzi kama watumwa wanavyo nunuliwa japo kwa sasa Eti ni shukrani!? Wewe wazazi wako nani anawashukuru?

Na ndio maana watoto wataitwa kwa majina yako, yule mwanamke ni mtumwa wako umemnunua!

Bible ukisoma mwanzo walikuwa wanatumia maneno mtumwa, ukinunua mtu ni mtumwa wako ana kutumikia wewe na kila kitakacho patikana ni chako wewe sio yeye
 
Kwa maana nyingine mwanamke hapaswi kufanya kazi sio?

Yaani asubiri kuzaa Kwa uchungu na kulea familia.
Anapaswa kukutumikia! Kufanyakazi kwa ruhusa yako!

Ndio maana wanawake wengi wanatumikishwa ktk ndoa zao na kulea familia hivyo hawana tofauti na wafanyakazi wa ndani,
 
Nikiwa Japani some years ago, nilimualika Binti wa kijapani (baby) tukale piza kwenye piza shop. Tulipo maliza kula akachukua menu, then akatoa nusu ya cost. Nilijaribu kumsihi asifanye hivyo mie ndo nilimualika aligoma. Nikalipa nusu ilobaki tukasepa. Ole wenu wabongo na hizo mentality zenu, akialikwa na kijana wa kiume (girlfriend or boyfriend) for outing, beba na hela ya kulipia nusu ya bili. Ukienda na mentality za kiafrika utaumbuka.
Hii ndio 50 kwa 50 inavyofanya kazi huko duniani ila huku ni 50 kwa 50 katika mambo mengine
 
Kwa hali ya uchumi ya sahizi mwanaume ukiishi na mentality hii, utakufa kwa stress kabla ya muda wako na nguo zitaishia kukudondoka kuchase majukumu

Hujiulizi zamani kipato cha baba pekee kilitosha kutunza familia tena extended
Lakini siku hizi vipato viwili lakini watu madeni kibao na budget za kufa mtu..... times has changed buda

Cha msingi ni mwanaume kuwork even harder amzidi kipato mkewe at all times sababu yeye hazai wala hanyonyeshi na hana majukumu ya nyumbani kama mwanamke, so ana muda mzuri wa kupiga kazi bila vikwazo
Na akibarikiwa zaidi familia ijitosheleze kiasi cha mke kuwa na uhuru wa kulea familia na kufanya kazi katika miradi ya familia
 
Anapaswa kukutumikia! Kufanyakazi kwa ruhusa yako!

Ndio maana wanawake wengi wanatumikishwa ktk ndoa zao na kulea familia hivyo hawana tofauti na wafanyakazi wa ndani,
Mnaowaoa wana tabu sana....
Ntafanya kazi kadri uwezo wangu unaruhusu cha muhimu sivunji sheria na kama kuna watoto basi kuna utaratibu mzuri.....

Sitofanya kazi kama mimi binafsi sijataka na sio sababu mume wangu kanizuia

Kabla hujaleta blah blah za usifanye kazi basi hakikisha una kipato kimejitosheleza, emergency fund imetulia na kuna ongoing investments na ikiwezekana uniajiri wewe basi

Lakini fyokofyoko while all you have ni ajira ya utumishi au biashara ambayo haina hata system bado NO WAY
 
Dini ina hesabu ni moja ya mali zako! Ata matumizi yake ni wewe unatakiwa kuyapangia Au kuelekeza

Kumsaidia mzazi ni wewe kwa ruhusa yako!

Hivyo kuoa na kutoa mahari ni kufanya manunuzi kama watumwa wanavyo nunuliwa japo kwa sasa Eti ni shukrani!? Wewe wazazi wako nani anawashukuru?

Na ndio maana watoto wataitwa kwa majina yako, yule mwanamke ni mtumwa wako umemnunua!

Bible ukisoma mwanzo walikuwa wanatumia maneno mtumwa, ukinunua mtu ni mtumwa wako ana kutumikia wewe na kila kitakacho patikana ni chako wewe sio yeye
Mahari ni ya mke sio wazazi .
 
Basi kama lengo si kusaidiana, wanawake wasikubali kuolewa kila mtu abaki na yake
 
Wanabodi
Changamoto nyingi za ndoa zinatokana na mambo mengi ila makubwa matatu.
Moja Ni kukosekana Kwa hekima. Busara na maadili.kwa pande zote .

Pili changamoto za muingiliano WA desturi na mila.hapa watu wanaoana Hawajuani hivyo ni namna gani wanaweza kuwa flexible Ku adopt changamoto za kufahamiana ndo tatizo ,na ili iweze kutatua Hili lazima iwe umetatua tatizo la.kwanza hapo juu.
Namaanisha malezi na makuzi ya wahusika,Aina ya familia wanazotoka Aina za marafiki ,tofauti ya vipato na malengo ya wahusika kwenye ndoa .nk

Tatu :utu na namna ya kusululisha migogoro ,hili ni tatizo,wazazi ndugu wamekosa utu,wengi hawasululishi kwa maana ya kujenga ila.kwa maana ya mtt wao anataka nn,Nani anakipato kikubwa hata km amekosea kukemea inakua ngumu.

Zamani Bibi n babu wakilima shamba umiliki wa uchumi ni WA pamoja Leo Kwa nn wote tunafanya kazi ila vipato vyetu haviko pamoja? MTU unapooana na mwenzi wako maana yake ni mwili mmoja ,Kwa nn msikusanye mkapanga mkatumia pamoja?
Km umeolewa na MTU hamlingani kipato Kwa nn ukubali?halafu kijana WA watu umwambie mm nataka. Muishi masaki wakati unajua Kwa mweZi mshahara wake ni laki tatu na ww milion ,maana yake km Una hekima mtaamia masaki ila itakubidi uchangie Kodi ya masala ambayo ni mara kadhaa ya kipato chake Kwa mwezi la sivyo inshi nae uswahili.

Km unaona pesa zako ni zako na zake ni zenu je umewahi kufikiria wazazi na wategemezi wake wanaishije? Unadhani wake na mawifi watakupenda?maana zako utapeleka kwenu na haununui hata chumvi. Ila unataka mshahara wote mle vema mlale vema,unadhani mtapata baraka ya wazazi?Kwa stress hiyo.unadhan ataishi miaka Mingi?.

Tukiwa kwenye keyboard tunakuja na hoja ya uSawa ila uhalisia WA maisha kuna watu Wana Hali ngumu na wametolewa pagumu na jamii au ukoo.au familia hivyo hawana budi kulipa fadhila ....asiyefanya kazi na asile..
Ila pia kidole kimoja hakivunji chawa
 
Nikiwa Japani some years ago, nilimualika Binti wa kijapani (baby) tukale piza kwenye piza shop. Tulipo maliza kula akachukua menu, then akatoa nusu ya cost. Nilijaribu kumsihi asifanye hivyo mie ndo nilimualika aligoma. Nikalipa nusu ilobaki tukasepa. Ole wenu wabongo na hizo mentality zenu, akialikwa na kijana wa kiume (girlfriend or boyfriend) for outing, beba na hela ya kulipia nusu ya bili. Ukienda na mentality za kiafrika utaumbuka.
Na hao ndio wanatekeleza 50/50 kwa vitendo, huku kwetu wanataka usawa lakini hawataki wajibu unaotokana na huo usawa kwaiyo wamebaki kuokoteza tu vipengele vinavyowanufaisha. Elimu usawa, uongozi usawa, ajira usawa haya mama umepewa access zote kiuchumi tu-apply usawa kwenye gharama za ndoa/mahusiano hapo ndipo wanawake wa kibongo hawapataki
 
Siku mkikubali kuacha kuwatawala wanawake na kuwalazimisha wawatii na kuwaheshimu, na siku mkianza kufanya kazi za nyumbani na kulea watoto kila siku basi hata wanawake wataanza kuhudumia familia bila tatizo, yani ninyi mnataka majukumu sawa tu tena ikibidi mwanamke afanye zaidi ila haki sawa hamtaki kuwapa
 
Back
Top Bottom