Monalisa apata presha mtoto wake aliye Ukraine kimasomo, vita ya Urusi yamvuruga mama mtu

Monalisa apata presha mtoto wake aliye Ukraine kimasomo, vita ya Urusi yamvuruga mama mtu

Na ukitoboa ndo wa Kwanza kuomba omba,,

Nilipataga sekeseke la kimaisha mwaka juzi bhana karibu watu wote wa karibu hawakutaka hata kunijua, walivyosikia nimepata mwanaume mwenye uchumi bomba baadhi yao walianza kujipendekeza na nilivyo mstaarabu niliwazawadia block wote sitaki mazoea
So uchumi wa mwanaume ni wako[emoji15]!?

Aisee
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Wabongo tuna PhD za unafiki acha kabisa,, hebu soma comments nyingi uone watu wanavyofurahia maumivu ya monalisa na bintiye,, halafu siku akifanikiwa hao hao utawaona watakavyoanza kulaani oooh tulimsaidia kupaza sauti ili mwanae apate msaaada mara tulimuombea,,, utumbo utumbo tu mxiiiieeeew
Monalisa kalileta hilo swala public ili iweje!?

Ukishaleta kitu in public kuwa tayari kupokea yote.

Kama huwezi matatizo yako maliza mwenyewe kila mtu ana matatizo yake!?

So wakati mwingine walimwengu hawana baya inategemea na wewe umejiweka katika position gani

Unaweza watu wanakuchukia kumbe unajishtukia tu[emoji2]
 
Siku hizi Mona sijuwi kawaje, yaan hadi nishaanza kumdharau msieeew, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
FB_IMG_16459958621259558.jpg
 
Baada ya Urusi kuonyesha nia ya dhati kabisa ya kuishambulia Ukraine, mataifa mengi Duniani yalichukua hatua za kuwarudisha raia wake nyumbani.

Wale ambao hawakuwa na nauli Serikali zao ziliwatumia nauli.

Na baadhi ya nchi kama Israel na Germany walituma ndege kabisa kubeba raia wao.

Wakati hayo yakijiri, Tanzania ilikuwa kimya utadhani hakuna mtanzania yoyote Ukraine.

Baada ya Urusi kutangaza kuyatambua majimbo ya Donetsk,Donbass na Lugansk yaliyoasi kutoka Ukraine na kujitangaza Jamhuri,ndipo Serikali ya Tanzania ilipotoa ushauri tu,na siyo msaada kuwataka Watanzania waliopo Ukraine warudi nyumbani.

Yaani ni ushauri tu,na si kwamba Serikali haikujua kwamba ni lazima vita iwepo, hapana, Serikali ilijua yote kuwa vita ipo kwa sababu kila kitu kilikuwa wazi ktk uso wa Dunia.

Ila kwa sababu ya kutokuwa na Desturi ya kupenda watu wake ndo sababu haikuchukua hatua zozote kuokoa watu wake.

Mmoja Kati ya Watanzania wenye majonzi na hili janga la Ukraine ni msanii wa Bongo movie,Monalisa, anadai kwamba amepoteza mawasiliano na Bintiye anayesoma Ukraine na hajui hatima yake hadi sasa hivi.

Kulikuwa na ugumu gani Serikali kuchukua hatua mapema za kuokoa watu wake kwa gharama yoyote ile?

Huwa tukisema kwamba Serikali ya CCM imechoka na imechakaa kifikra na kiutendaji tunaonekana watu wabaya sana.

Tuendako tutaongea lugha moja,sasa hivi mipaka ya Ukraine imefungwa,na anga limefungwa, hairuhusiwi ndege yoyote ya kiraia kuruka kwenye anga la la Ukraine.

Rais wa Ukraine amewataka raia wote kwenda kwenye kambi za kijeshi kuchukua silaha za kujihami.

Hatima ya Watanzania waliopo Ukraine hadi sasa haijulikani itakuwaje.
Kwahio Sonia nae itabidi apewe Gun ili apambanie life lake😎
 
Monalisa kalileta hilo swala public ili iweje!?

Ukishaleta kitu in public kuwa tayari kupokea yote.

Kama huwezi matatizo yako maliza mwenyewe kila mtu ana matatizo yake!?

So wakati mwingine walimwengu hawana baya inategemea na wewe umejiweka katika position gani

Unaweza watu wanakuchukia kumbe unajishtukia tu[emoji2]
Wabongo tunajuana kwa unafiki,,
 
Baada ya Urusi kuonyesha nia ya dhati kabisa ya kuishambulia Ukraine, mataifa mengi Duniani yalichukua hatua za kuwarudisha raia wake nyumbani.

Wale ambao hawakuwa na nauli Serikali zao ziliwatumia nauli.

Na baadhi ya nchi kama Israel na Germany walituma ndege kabisa kubeba raia wao.

Wakati hayo yakijiri, Tanzania ilikuwa kimya utadhani hakuna mtanzania yoyote Ukraine.

Baada ya Urusi kutangaza kuyatambua majimbo ya Donetsk,Donbass na Lugansk yaliyoasi kutoka Ukraine na kujitangaza Jamhuri,ndipo Serikali ya Tanzania ilipotoa ushauri tu,na siyo msaada kuwataka Watanzania waliopo Ukraine warudi nyumbani.

Yaani ni ushauri tu,na si kwamba Serikali haikujua kwamba ni lazima vita iwepo, hapana, Serikali ilijua yote kuwa vita ipo kwa sababu kila kitu kilikuwa wazi ktk uso wa Dunia.

Ila kwa sababu ya kutokuwa na Desturi ya kupenda watu wake ndo sababu haikuchukua hatua zozote kuokoa watu wake.

Mmoja Kati ya Watanzania wenye majonzi na hili janga la Ukraine ni msanii wa Bongo movie,Monalisa, anadai kwamba amepoteza mawasiliano na Bintiye anayesoma Ukraine na hajui hatima yake hadi sasa hivi.

Kulikuwa na ugumu gani Serikali kuchukua hatua mapema za kuokoa watu wake kwa gharama yoyote ile?

Huwa tukisema kwamba Serikali ya CCM imechoka na imechakaa kifikra na kiutendaji tunaonekana watu wabaya sana.

Tuendako tutaongea lugha moja,sasa hivi mipaka ya Ukraine imefungwa,na anga limefungwa, hairuhusiwi ndege yoyote ya kiraia kuruka kwenye anga la la Ukraine.

Rais wa Ukraine amewataka raia wote kwenda kwenye kambi za kijeshi kuchukua silaha za kujihami.

Hatima ya Watanzania waliopo Ukraine hadi sasa haijulikani itakuwaje.

Kwani walipelekwa na serikali?

Kwanini mnatetea sana waliopo nje kubebwa na serikali wakati bibi zenu kila siku wanakwama kule vijijini na hampigi kelele? Waliopo nje ni bora zaidi kuliko wa ndani?

Kufananisha bongo na US ni sawa na kumfananisha mzee wako na Bakhressa. Bakhressa akimnunulia mwanae Ferrari na wewe unataka baba yako akununulie Ferrari wakati unajua uwezo wake?

This comes from a diasporic.
 
Muigizaji mkongwe wa Bongo Muvi, Monalisa ameelezea jinsi ambavyo mgogoro wa Urusi na Ukraine unavyompa hofu kwa kuwa mwanaye yupo nchini Ukraine.

Rais wa Urusi, Vladimir Putin alitangaza kuanza oparesheni ya kijeshi katika baadhi ya maeneo ya Ukraine baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili.

Monalisa ameandika: “Tumbo linanicheza kama mzazi. Ukraine! Hakuna ndege, nampataje mwanangu? Mungu wasimamie watoto wetu.”

Ameandika maandishi hayo katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha moja ikionyesha moto katika moja ya maeneo inayodhaniwa kuwa ni Ukraine.

Binti huyo, Sonia inaelezwa kuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Sumy State kilichopo katika Mji wa Sumy akisomea kozi ya Uhasibu na Ukaguzi (Accounting and Auditing) kwa kipindi cha miaka minne.

Sonia mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema: "Sababu ya kuchagua kwenda kusoma nchi hiyo ni kwanza wametutangulia kiteknolojia kwa hiyo tunapoenda huko kusoma tunaweza hamisha teknolojia kwa njia ya elimu kuja hapa Tanzania.

"Kitu kingine Ukraine na Urusi ni nchi ambazo zina fursa nyingi za utalii hivyo tunavyoenda huko kusoma ni nafasi yetu kuwaambia Tanzania kuna nafasi nyingi za Uwekezaji, kuna Mlima Kilimanjaro, Tanzanite na mengine mengi ambayo Tanzania tunajivunia," amesema Sonia.

View attachment 2129730

View attachment 2129731
hawapo watanzania wengine wanosomesha watoto huko ukraine au ni huyu msanii tu
 
Wanawapeleka watoto wao kusoma nje wakirudi wanaishia kuajiriwa mshahara laki tatu 😁, afadhali ya housegirl alieajiriwa nchi za kiarabu anakula laki 6 hadi 9 per month.
 
Ameenda kusomea Accounts ..
Kuna mtu alienda Russia akasomea Tourism..mwaka wa sita anamaliza hata Interview moja hajawahi itwa.
Ni vizuri Wazazi wakawa wanashauriwa vizuri nini mtoto akasome huko nje, otherwise Tanzani we have the best Universities
 
Africa aliyetuloga alaaniwe Yan unaenda Russia kusomea tourism na lile baridi lakule ukae miaka 6 haha wakati kuna watu hapa wanapiga 6months tu wanakua vizur Hata asipopata kazi anajianzishia tu kikampuni chake cha utalii
 
Tatizo la watanzania wengi hua wanadhani kila nchi ya huko ulaya ni nzuri na mtu akisoma huko atapata elimu nzuri.

Hawajui kuna nchi za ulaya ambazo ni za hovyo kuliko hata tz na kuliko kwenda huko bora kubaki tu hapa hapa.
Sifa kwenda kusoma nje,wee hujui hilo hata kukaa nje lakini unapata shida na tabu ni poa tuu🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom