Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Soma alama za Nyakati,hujui kilichotokea hapo morogoro leo asubuhi?
Nimefikia Morogoro mjini kwa kua sina ndugu au mtu ninayemfahamu basi nmefikia Guest za karibu na Msamvu , kilichonishangaza mno ni wanaume wa maeneo haya kupenda sana kununua malaya .Unaweza ukawa unatembea tu mtu anakuuliza naomba company yako Usiku au je uko na mtu ukimjibu sna mtu anakuomba mechi
Uzi tayari
 
Pole yao lakini kuna ajali ya hivyo ilitokea Mbeya lakini watu hawajifunzi tuu may be hawa vijana hawajui

Yaa, kwa mtoto mwenye umri wa 0 to 7 hawezi kujua kinachotokea. Wengi wenye boda boda kipindi hicho walikuwa wana umri wa chini ya miaka 10. Sasa wana chini ya miaka 30. Hawawezi kujua kilichojili mwaka huo wa 1999.
 
Una uhakika wahanga hawasaidiwi ?

Una uhakika wa hilo au unaropoka ropoka tu hapa

Kwa hiyo unataka hao watu wabaki na hayo mafuta humo ndani ?
Unajua madhara ya mafuta hata kijiko chake kimoja ?

Unaongea nini hapa ?

Soma ulkchoandika upya
Sikubaliani na kauli yako hii...tamaa ya binadamu na pia 'unyama' ndiyo inawasukuma watu kuanza kuiba kwenye magari yaliyopata ajali baadala ya kuwasaidia wahanga..hii imetokea mara kadhaa katika barabara zetu nchi hii...Gari inaanguka au kupata ajali lakini watu wanakimbilia kwenye ajali wengi wao siyo kusaidia bali kuporana hata kuwamalizia kwa kuwaua majeruhi...Ilitokea hii kati ya Njombe na Songea maeneo ya Lukumburu ambako basi lilidondoka lakini wachache wenyeji wakajitokeza siyo kusaidia bali kupora na kuwaua wale waliokuwa wakiomba msaada...ni unyama...
 
Yaa, kwa mtoto mwenye umri wa 0 to 7 hawezi kujua kinachotokea. Wengi wenye boda boda kipindi hicho walikuwa wana umri wa chini ya miaka 10. Sasa wana chini ya miaka 30. Hawawezi kujua kilichojili mwaka huo wa 1999.
Kwahiyo hawajui kuwa petroli ni hatari hadi kuwepo na matukio yenye kujirudia kila mwaka ili kutoa funzo kwa kila kizazi!!
 
Nawapa pole sana ndugu juhudi za kusaka maisha izo unaweza sema zari kumbe majanga kimsingi hili tukio litakuwa funzo kwa wengine
Tatizo atuchelewi kujisahaulisha, haya magari ya mafuta yanalipukaga sana na watu kuungua baada ya kupata ajari,
 
Duuu police ikapige mabomu kweny Lori la mafuta ulisema??????
Kuna Lori Moja la mafuta lilipinduka mbele ya mto ruvu nikakuta watu na madumu nikaandika humu jamii forums kuwa polisi nendeni mkawapige virungu na mabomu nikatukanwa Sana humu jamii forums kuwa Nina roho ya shetani nk kwa tamko langu lile ona sasa maafa hayo
 
*Ajali Ya Moto Morogoro*

*Changamoto:*
[emoji91]Tumekosa Elimu elekezi mara kwa mara juu ya kujikinga au kuepuka kukaa, kusogelea sehemu hatarishi *(Ngazi ya familia)*

[emoji91] Umasikini na Tamaa ya kupata pesa bila kuwajibika *(Uchumi wa watanzania kwa ujumla)*

[emoji91]Uharaka wa vyombo vya ulinzi na usalama kufika sehemu zenye matukio hatarishi kwa ajili ya kuzuia watu wenye tamaa *(naamini kuna waliopiga 911 kutoa taarifa)*


[emoji1280]Mpaka kesho bado kuna Bus za ability zinaenda kituo cha mafuta kwa ajili ya kuweka mafuta wakiwa wamebeba abilia na hakuna abilia anayepiga kelele *(Tuendelee kuona gap ya Elimu na Uwajibikaji katika Kukwepa Majanga)*

*Hitimisho*
[emoji615]Tuwaombee ndg, jamaa na marafiki waliokumbwa na janga hili

[emoji615] Turudi nyumbani tukaongee na familia zetu juu ya namna Bora ya kuepuka Majanga yanayoweza kutokea katika maisha yetu ya kila siku

[emoji615]Serikali nao tuwaombe wafanye kazi yao ya ulinzi wa raia na Mali zao kwa ufanisi wa juu zaidi

*_Imetolewa na Mtanzania_*
 
Hii kwa namna moja itakuwa fundisho tosha kwa wananchi wa morogoro, maana nikisema nchi nzima ntakuwa nakosea tungesha jifunza kutoka Mbeya
Kujifunza katika hali ya uchungu kabisa.​
 
Kiukweli wewe ni kiumbe katili na jahili sana
Kuna Lori Moja la mafuta lilipinduka mbele ya mto ruvu nikakuta watu na madumu nikaandika humu jamii forums kuwa polisi nendeni mkawapige virungu na mabomu nikatukanwa Sana humu jamii forums kuwa Nina roho ya shetani nk kwa tamko langu lile ona sasa maafa hayo
 
Pole kwao pamoja na familia zao zote na watanzania kwa ujumla kwa kupotelewa na vijana ambao jamii na taifa lilikuwa likiwategemea katika juhudi za kukuza uchumi
 
Back
Top Bottom