Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Duuuh mdau huko whatsap zilivyosambaa sijui hata unazuiaje watu wasisambaze
Mnajua kilichompata Mtanzania kule Uingereza aliyesambaza picha za wahanga wa tukio la ugaidi?...In short ni kosa kusambaza picha za wahanga iwe maiti au majeruhi kama kukatika viungo na kadhalika
 
Hahahahhahahaaa halafu kwenye misiba mimba nyingi hutungwa....

Ila leo niko kihatari sana, Staffordshire mkono wa uchokozi atakula sambusa za nyama... Sijui kitu gani kitanizuia..... Mwili unanivuta kwa nguvu zoteee.
[emoji28][emoji28][emoji28]

Ila we kasie bhana !
 
Inasikitisha sana....

Kuna siku nilikua njian to tanga,lori la gesi likashika moto berti na mfumo wa mafuta....kila mtu alikimbia gari lake na kutokomea maporini

Wakabak wajeda 4,tingo na dereva wakambana na moto mpaka wakaudhibiti kabla ngoma haijalipuka...

Kwenye msafara alikuwepo NB waziri wakat huo alikimbia bila viatu
Kwa uelewa wangu mdogo kwenye Open Space ni bora ya Gesi kuliko Petrol....Petrol ni shida sana...yani mnooooo
 
Nimefungua fasta nikidhani una update za tukio la moto kumbe ni uchuro tu!


🤣🤣🤣 Tena anadai yupo kwenye guest house iliyopo msamvu mahali ambapo ajali ya moto imetokea!!!.

Watu tunayo majonzi ya ndugu zetu kufa kwa moto yeye anatuletea mambo yake hapa!!.
 
Hizi ajali za watu kuungua mafuta wakichota kwenye malori yaliyoanguka nazisikia mara nyingi sana nikiwa tangu mdogo,
sasa unajiuliza hivi watu hawajifunzi?

Kuna watu watawatetea kuwa ni masikini, ila hata kama watu ni masikini kiasi gani, utaendaje kubet maisha yako kwenye mafuta ya 10,000 au 20,000 tena kwa kifo cha mateso kiasi hicho?.

Kilichowapata wamekikaribisha wenyewe
Kifo cha wengi harusi!
 
Niandike hili kwa hisia kali sana...

Asilimia kubwa ya ajali hapa nchini hutokea kwa sisi wenyewe kupenda iwe hivyo na uwezekano wa kupata kinga ya ajali japo kwa kiasi kidogo upo ila tatizo ni moja tu kuwa sisi hatupendi maisha yetu..

Hakuna mtu asiyejua hatari ya mafuta yoyote yale hata kama ni ya taa ila kwa vile hatujipendi basi tunabet roho zetu kwenye matukio kama hayo.

Magari ya mafuta kukutana nayo mtaani yakirandaranda ni suala la kawaida tena kwenye maeneo yenye watu. Ndiyo ni magari yenye kupita katika mazingira yetu ila mimi ni mmojawapo ya watu wenye kuchukia sana magari hayo kutembea nyakati za mchana. Serikali ingekuwa inasikia ingeamuru magari hayo kusafiri usiku na ingewezekana kabisa kutengwa barabara maalumu kwa miji mikubwa ambazo zitakuwa ni maalum kwa ajili ya kuingiza na kutoa magari hayo mjini.

Pili, Hivi Polisi kila siku mnakaa barabara kukusanya mapato kwa njia ya faini kwanini msigeuze shingo mtazame ukiukwaji wa sheria kwenye vituo vya mafua. Daladala na mabasi ya abiria huingia huko na watu kwenye kujaza mafuta, wakati huo injini za vyombo vyao ziko ON. Ni kipi kimewashinda katika hili au mnataka siku watu wafe ndipo mtoe rambirambi kisiasa?

Ukiwa Dar utakutana na hawa wajinga wenye kutembea na spana mkononi na rambo kwa ajili ya kuingia masalia ya mafuta kwenye hayo magari ya mafuta. Ila kwa vile haijawahi kutokea ajali au maafa hili limekuwa jambo la kawaida na linazidi kushika hatamu, ipo siku litafunguliwa gari lenye mafuta na kizaazaa kitokee.
 
Siungi mkono kauli yake lakini hata kusogea kwenda kushangaa nako ni ujinga uliopitiliza. Je, moto unajua huyu amekuja kushangaa tu? Na bado watu wanafanya makosa zaidi... wamejazana kuangalia miili iliyoungua kama wanaangalia sinema nzuri. Wengine wanafikia hata kuwa na ujasiri wa kupiga picha na ku-share. Ujinga ulioje!
Ndo hoja yangu kuu, kwamba tusiishie kutoa elimu kwa vibaka tu tuelimishie jamii ya watanzania hata kwenda kushangaa ajali za malori ya mafuta hata kwa umbali wa mita 500 bado si salama kwa uhai wa maisha yao
 
So sorry, very very sad.I've seen photos.. oh my God!!.Heart felt condolences to all and you tanzanians
 
Walioungua ni Mama Lishe wa Msamvu na Madreva Wa Boda boda. Wote walikua wanajiongeza kuchota mafuta ya bure.
 
Walioungua ni Mama Lishe wa Msamvu na Madreva Wa Boda boda. Wote walikua wanajiongeza kuchota mafuta ya bure.
 
Hebu ficha upumbavu wako mkuu

Unadhani hao wananchi wanajua jinsi ya ku handle hayo mafuta

Vipi yakilipuka utamlaumu nani

Tusiwe wajuaji wa kila kitu

Empty and rubbish mindset like this must be stopped

Sikubaliani na kauli yako hii...tamaa ya binadamu na pia 'unyama' ndiyo inawasukuma watu kuanza kuiba kwenye magari yaliyopata ajali baadala ya kuwasaidia wahanga..hii imetokea mara kadhaa katika barabara zetu nchi hii...Gari inaanguka au kupata ajali lakini watu wanakimbilia kwenye ajali wengi wao siyo kusaidia bali kuporana hata kuwamalizia kwa kuwaua majeruhi...Ilitokea hii kati ya Njombe na Songea maeneo ya Lukumburu ambako basi lilidondoka lakini wachache wenyeji wakajitokeza siyo kusaidia bali kupora na kuwaua wale waliokuwa wakiomba msaada...ni unyama...
 
Back
Top Bottom