Not the first or second to happen!Let this be a lesson
sana mkuu wangu....... mzigo mwingi sana yan nikiangalia hao waliokufa naona ni kama walipitiwa na upepo wenye joto kali dah...Aisee hizo litre ni nyingi sana mkuu, duh sikuwahi hata kuimagine.
Sasa hao jamaa nao walihisi zile ni koki za maji ama bia. Siwezi Risk maisha yangu kipumbavu hivyo
Ilikuwa Mbeya Bwana!!! Wahehe hawawezi kufanya kitu kama hicho
Kwahiyo ulitegemea polisi wakifika watu ndio hawatoteketea!?Polisi wanafika watu wanateketea
Wazee wa kuwasha mwenge buanaAjali imetokea eneo la Mzambarauni (Nje kidogo ya Mji wa Morogoro). Inadaiwa kuwa waendesha Bodaboda waliojaribu kuchota mafuta wameteketea ktk moto huo
> Mpaka sasa chanzo cha Lori hilo kupinduka na hatimaye kushika bado haijafahamika
======
Morogoro. “Inasikitisha”. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo.
Tukio hilo limetokea leo Jumamosi Agosti 10, 2019 ambapo Mwananchi limefika eneo hilo na kushuhudia miili iliyoungua ikiwa imelazwa pembeni ya barabara ya Dar es Salaam-Morogoro wengi wakiwa ni madereva bodaboda na mamalishe wanaofanya shughuli zao hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 57 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi.
Ajali hiyo imetokea umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.
Baadhi ya mashuhuda wamelieleza Mwananchi kuwa baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza kuchota mafuta hayo.
Wamesema mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alikuwa akivuta sigara, kwamba ndio chanzo cha mlipuko huo.
Chanzo: Mwananchi
Baadhi ya maeneo bajaj zinaelekea njia ile ile ya boda boda. Ni vurugu mtindo mmoja!Mh Kangi na mkuu wa trafiki polisi Sasa waje na mpango mkakati kuhusu hawa boda boda sasa. Kuwe na regulatory authority special kwa ajili yao. Ni kuwanyang'anya leseni tu na kuzifunga hadi akili ziwakae. Washakuwa majabali hawa
Nimeikumbuka hii Kuna mtangazaji was redio 1 kipind hicho alichombeza mwenye dumu twende,mweye ndoo twende,mweny sufuria twende, mwenye kijiko twende hata aliyekosa kitu alidiriki kwenda na kikombeeSiyo Iringa, ni Mbeya milima ya Uporoto kuelekea Tukuyu ambapo mtanashati John alisababisha moto ulipuke baada ya kujaribu kuiba betri, wenye sufuria hata, wenye vijiko nao wamo, wenye madumu twende, kaburi lao la pamoja lipo kando ya barabara.
Acha kubishana na wapumbafu mkuuUna uhakika wahanga hawasaidiwi ?
Una uhakika wa hilo au unaropoka ropoka tu hapa
Kwa hiyo unataka hao watu wabaki na hayo mafuta humo ndani ?
Unajua madhara ya mafuta hata kijiko chake kimoja ?
Unaongea nini hapa ?
Soma ulkchoandika upya
Kwahiyo hata majambazi wanapokwenda kuvamia wakiuliwa utasingizia umasikini?. Acha kuendekeza watu kufanya mambo ya kijinga kwa kisingizio cha umasikini, 90% ya waliofariki ni waendesha bodaboda waliokua wakichota mafuta kwa ajili ya bodaboda zao, zaidi ya pikipiki 10 zimeteketea kwa moto, wana umasikini gani wa kuwafanya kuhatarisha maisha yao?Madhara ya umasikin haya huku tunaendelea kufanywa wapumbavu kwa kuaminishwa kua uchumi unakua. I hate poverty
Vifo vya kujitakia hivi, ninahuzunika lakini sisikitiki.
Hata sio ya kuongozana nayo,ukipata upenyo wa kulipita hata usirembe! Kaa nao mbaliHilo gari likiwa mbele ama nyuma yangu huwa sina amani ,achilia mbali sijui lianguke nisogee lilipo
R.I.P
Hii hatari sanaVideo kabla ya moto kuwaka na baada ya moto kuwaka...shuhuda anasema chanzo cha moto teja alichomoa betri
Elimu kuhusu Moto itolewe hapo tumepoteza vijana wengi sana
View attachment 1177386
View attachment 1177389
View attachment 1177388
View attachment 1177391