Morogoro: Mpangaji afungiwa ndani Saa 27 na Mmiliki wa nyumba kwa madai ya kukiuka Notisi ya kuhama

Morogoro: Mpangaji afungiwa ndani Saa 27 na Mmiliki wa nyumba kwa madai ya kukiuka Notisi ya kuhama

Bongo sekta ya upangishaji nyumba imekaa kiduwanzi sana, mtu anataka malipo ya miezi sita wakati wafanyakazi karibia wote wanalipwa kwa mwezi, wiki au siku! Ni uhovyo tu ila ndio sekta huria hii kila mtu anafanya anavyoona inamfaa na mali yake.
Lakini hajalazimishwa mtu. Kama mtu anajijua hali yake ni bora akatafute nyumba inayoendana na hali yake. Kwa nini mtu akatafute kupanga nyumba ambayo mwisho wa siku itamshinda malipo kana kwamba kulikuwa hakuna nyumba zinazofaa yeye kuishi?
Nyumba za kupanga ni Biashara kama ilivyo kwa Biashara nyingine. Mwenye Biashara yake ndo anayepanga bei na utaratibu wa malipo. Sijawahi ona mtu unaenda buchani halafu unaambiwa kg. 1 ni Tzs 8,000/= halafu wewe mnunuzi unachukua kisu na kuanza kujikatia kg.1 pale unapopapenda.
 
Kwa hiyo usipopata nyumba nyingine ndiyo tuseme uhami na kodi hulipi kisa unatafuta nyumba nyingine ya kupanga!!??
Eti bhana. Hao ndo wakufungiwa ndani humo mpaka waelewe kwamba nyumba hiyo ni mali ya watu. Ila zipo taratibu za kiustaarabu za kumwondosha mpangaji ndani ya nyumba yako esp. ukizingatia Mkataba aliosaini.
 
Kuna muda maalumu wa notice kisheria, wenye nyumba zingatieni hilo, sio kwa sababu ndugu zako tu kutoka huko Kyela wamekuambia wanakuja kuishi kwako mjini unafukuza wapangaji kiholela.
Sidhani kama issue iko hivyo.
Mpangaji kama halipi kodi ndani ya muda mliokubaliana kwenye Mkataba na haoneshi dalili za kulipai.e. anapiga chenga - muongo-muongo e.g. Hapokei cm, hajibu msg, dharura haziishi, visingizio vya ugonjwa au ukienda hapo kwenye nyumba humkuti, ukimtafuta muonane ana kwa ana (physicaly) anakukwepa n.k. Je, mtu msumbufu wa namna hiyo unamfanyaje?? Au labda tuseme Wenye nyumba za kupanga (Land lords)huwaga hawana Hasira? i.e. unaweza kumkoroga,kumzingua kwa vitimbi vyako halafu unategemea yy atakuchekea tuu??
 
Tena ukikutana na mmiliki kichaa kama Mimi ninakuchapa risas... Live.
Duh! Umetisha mkuu. Halafu baada ya hapo kuchapa risasi; utakuwa sasa huna mpangaji bali una kesi nzito ya kujeruhi au kuua kwa makusudi ikiwa ni pamoja na kunyang'anywa kasilaha kako hako kanakokupa ujasiri na pia ww kuingia hifadhini (mahabusu). Je; Umepata au Umepatwa????
 
Kuna wapangaji wana kiburi na jeuri tena angemwagia nyumba petrol akamchomea humo humo kabsa huyo mpangaji.na ukifuatilia utakuta ni mwl wa shule x ya msingi huyo mpangaji
 
Duh! Umetisha mkuu. Halafu baada ya hapo kuchapa risasi; utakuwa sasa huna mpangaji bali una kesi nzito ya kujeruhi au kuua kwa makusudi ikiwa ni pamoja na kunyang'anywa kasilaha kako hako kanakokupa ujasiri na pia ww kuingia hifadhini (mahabusu). Je; Umepata au Umepatwa????
Kuna wapangaji wamekuwa sugu mkuu.
 
Gen-Z, hawataki kuulizia Bei za viwanja,hawatski kujenga, wanataka kupanga TU.
Sasa, kituko hawataki kulipa Kodi za nyumba.
Matokeo yake ,wanapenda
Mashangazi, starehe, pombe, magari mazuri ila hawajui watayapaki nyumba ipi na simu za milioni tatu.
 
Mwenye nyumba atamlipa huyo jamaa pesa isiyo pungua milioni 5 akisema Hana nyumba inapigwa mnada.
Na ukisikiliza upande wa pili,utasema mpangaji amlipe mwenye nyumba kwa kumsababishia usumbufu pamoja na uharibu wa mali!!
 
Wakuu, huu ni Uungwana kweli?

Huko Marogoro mwenye nyumba kamfungia ndani saa 27 mpangaji kisa amekiuka notisi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mmiliki wa nyumba Plot namba 149 BLOCK ‘A’ Kihonda Kilimanjaro, Dk. Lusako Mwakiruma ilioyopo Mtaa wa Kilimanjaro Manispaa ya Morogoro, amemfungia ndani mpangaji wake kwa saa 27 kisha kumtolea vitu vyake nje, kwa madai kuwa mpangaji huyo, Paschal Paulo alishindwa kupokea notisi ya kumtaka ahame kwenye nyumba hiyo ndani ya mwezi mmoja.
Ukishindana na mwenye nyumba hama, kwanini ugomee notisi!
 
Lakini hajalazimishwa mtu. Kama mtu anajijua hali yake ni bora akatafute nyumba inayoendana na hali yake. Kwa nini mtu akatafute kupanga nyumba ambayo mwisho wa siku itamshinda malipo kana kwamba kulikuwa hakuna nyumba zinazofaa yeye kuishi?
Nyumba za kupanga ni Biashara kama ilivyo kwa Biashara nyingine. Mwenye Biashara yake ndo anayepanga bei na utaratibu wa malipo. Sijawahi ona mtu unaenda buchani halafu unaambiwa kg. 1 ni Tzs 8,000/= halafu wewe mnunuzi unachukua kisu na kuanza kujikatia kg.1 pale unapopapenda.
Unalinganisha vitu visivyo faa kulinganisha.
Ukienda kununua nyama unaanza kuandikiana mkataba na muuzaji?
Nyama biashara ya pesa ndogo wakati nyumba biashara ya pesa nyingi.
Ushaona Chama Cha wanunuzi nyama buchani pekee?
Kuna Chama Cha wapangaji pekee.
Tumia akili yako yote kabla hujasema lolote.
Kuna kupata shida katikati ya mkataba wako ikachangia kukosa pango kamili inapoisha pesa iliyo lipia tayari. Tusijitoe utu, hata taasisi za fedha wanasikiliza wateja wanaowadai na kuchelewesha malipo baada ya kupata tatizo.
 
Gen-Z, hawataki kuulizia Bei za viwanja,hawatski kujenga, wanataka kupanga TU.
Sasa, kituko hawataki kulipa Kodi za nyumba.
Matokeo yake ,wanapenda
Mashangazi, starehe, pombe, magari mazuri ila hawajui watayapaki nyumba ipi na simu za milioni tatu.
Kupanga ni rahisi kuliko kujenga
 
Back
Top Bottom