Morogoro ni Mkoa mzuri namba Moja wa kuishi Tanzania

Masaa matatu ukiwa mjini na viunga vyake ambapo ni 15% ya mkoa wa morogoro
65% Ya morogoro inakuchukua masaa 10 hadi 16 hivi kufika Dar (zaidi ya Arusha to Dar). Ni vizuri tukasema ukweli na sio hadithi za kufurahisha watu
Halafu Morogoro mjini ni ndogo sana unaweza ukazunguka kwa dkt chache ukaimaliza yote
 
Yawezekana Moro bado huijui vizuri Mzumbe ipo pembezoni kabisa Wilaya ya Mvomero , ina impact ndogo Sana kwa Moro town . Hebu taja mkoa wako hapa nisijekuwa nabishana na mlughalugha wa huko sitimbi

Wafanyakazi wa mzumbe wanaishi morogoro mjini
 
umenena
kweli mkuu umenipa nguvu nina kiwanja changu kihonda kwa chambo nijiwekee hata kakibanda kakupangisha
 
Vyuo vya maana hapo ni viwili tu, SUA na Mzumbe, hivyo vingine ni zaidi ya vyuo vya Kata wanachuo wanachapwa bakora
Ukiachana na Dar kuna mkoa gani mwingine hapa Tz una vyuo vya maana hata viwili tu!?
 
Sasa tukikuita haraka dar, kuna party utawai kweli kuja?. Tunataka eneo tamu la karibu na dar au dom, na ndilo Moro.
Utakua una utoto au ujinga,kweni wewe tukikuita Mwanza kuna party,msiba au ndunguyo kapata shida hapa mjini utachelewa?ukichelewa ni umasikini wako,ila mimi ntakuja Dar chap na kurudi chap
 
Morogoro tatizo la maji sio la mitaa flani ni tatizo la mji mzima

Dar kuna mitaa ina shida ya maji Ila Morogoro labda uvune maji ya mvua Ila kama unategemea maji ya hilo bwawa sahau.

Nilishuhudia maji machafu yanatoka bombani nikapanyooshea mikono
Tatizo la maji Morogoro ni la mitaa utabisha hili labda kama ulienda mara moja tu na kurudi lakini sisi tulioishi kwa muda mrefu pale tunakuthibitishia tatizo la maji Morogoro ni la mitaa tu..Uzuri zaidi mimi kwa muda wote wa maisha yangu nimeishi hii mikoa miwili ya Dar na Morogoro,usichokijua chanzo cha maji Morogoro sio bwawa la mindu tu bwawa la Mindu linahudumia tu baadhi ya maeneo kwa mfano mimi niliishi Sabasaba tulihudumiwa na bwawa la Mindu na hatukuwahi kuona shida ya maji kwani maji ya bomba ilikuwa kila siku yanatoka halafu kuna wale ambao wanahudumiwa na maji kutoka mto Ruvu unaohudumia Dar pia kwa mfano maeneo kama bigwa,Kigurunyembe,na Kilakala wanahudumiwa na mto Ruvu hawa ndio kidogo wanaexperience shida ya maji kutokana na mto ruvu sometimes kupungua kina kumbuka unahudumia Dar,na maeneo ya pwani pia..Halafu kuna wale ambao wanaoishi sehemu za makao mapya kama Mkundi,Lukobe na Makunganya hawa nakiri wazi kwamba wanaexperience shida ya maji kama ilivyokuwa kwa maeneo mapya ya jiji la Dar ambao nao pia maji ya bomba wanayasikia kwenye redio
 
Naamini kibiashara ukitaka utoboe haraka

kama una mtaji wa kuanzia 20M kafungue duka la madawa ya mimea na mifugo Moro.

Ila u base hasa kwenye madawa ya mimea una weza piga sana pesa Moro.

Wana lima sana, ardhi na tabia ya nchi morogoro ina waruhusu kulima watakavyo.

kwahiyo wewe muuza madawa ya mime una weza kuwa tajiri mkubwa kwa kuwauzia madawa.


Hili wazo lina weza kumfaa mtu yeyote mwenye mtaji mzuri, hasa wa staafu, Pia hata kijana mungu aki bless ukawa na mtaji una weza lifanyia kazi hili wazo.
 
Elimu yangu nimeipatia morogoro na nikifikisha miaka 60 ntarudi kuishi morogoro na kufia ktk ardhi hio nnayo ipenda sana.
 
Daaah! Mkuu hiyo SIRI nlijua itakuwa ya mwisho ku-Disclose [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Napapenda zaidi Morogoro kwa kuwa hata kupatikana kwa Mademu wa 'Kuwabandua' ni rahisi kuliko Mikoa mingine yote.
 
Nafikiri una matatizo kidogo kufikiri, Mkoa wenye milima Mingi Tanzania ni Morogoro (Uluguru, Nguru, Udzungwa, Rubeho, Nyanda za Mahenge, n.k). Mkoa wenye mito yenye maji mengi na mirefu Tanzania ni Morogoro, Mto Kilombero unaanzia Mlimba hadi Kisaki ambapo unabadiri Jina na Kuitwa Rufiji huko pwani, Pia Mto Ruaha unaingia Kilombero uku Morogoro. Mto Ruvu Unaanzia Uluguru hadi Bagamoyo, Mto Wami Unaanzia Kilosa hadi Bagamoyo. Tanzania ina Mito 5 maarufu na 4, ipo Moro, achana na vimto vya uko kama pangani na kagera ambavyo havina impact kwa nchi. 1. Kilombero (Moro). 2. Ruvu (Moro), 3. Wami (moro), 4. Ruvuma(Mtwara/Ruvuma), 5. Rufiji (Morogoro/Pwani). 6. Ruaha (Morogoro/Iringa). Usilinganishe Morogoro na Uchwara wowote kimazingira, ingawa yote ni mikoa na ina uzuri wake.
 

Siwezi kubisha mkuu maana ni kweli huwa napita sana lakini nishaishi hapo zaidi ya mwaka na shida ya maji ilikuwa kubwa kiasi cha kutoa maji machafu hadi nikayasusia kuyatumia (around msamvu shule)

Na bado kwenye university year kuna marafiki zangu kibao walikuwa wanasoma SUA main & mazimbu campus, MUM, Jordan na wamepanga street lakini shida ilikuwa moja MAJI


Uzi mzima watu wanalalamikia maji kuwa tatizo ina maana wote hatuijui Morogoro isipokuwa wewe Tu mkuu
 
Sidhani. Tusubirie wataje Nauli ya SGR laah sivo Watumishi wa Umma hawatathubutu kujaribu, watabaki wafanya Biashara
Kama una biashara zako, unaingia ofisini mara mbili kwa wiki, unaachana na vurugu za Dar.
 
Comments za humu ni za watu wa Dar. Tuliosomea Moro tunajua shida za Maji na typhoid. Ukihamisha SUA na MZUMBE ujue umeiua Morogoro.
Kama watu wanatumia maji ya kutoka mindu basi kupata typhoid ni kawaida
Kuna makaz mengine wao wanatumia maji kutoka milimani hapo kdg nafuu

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…