Mpaka leo najiuliza, ilikuwaje mpaka Magufuli akawa Rais?

Lazima kuwa katili dhidi ya mapanya.

Fyekelea mbali mafisadi mpaka yakachanganyikiwa yakaamua kumdondosha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Chuma kile, hakikutepeta mpaka umautiii. Ni mwendo wa kukaza kamba kweli kweliiii ikibidi hadi uhai kutoka!

Ametufundisha somo kubwaa kwamba mafisadi na majizii yanahitaji kushughulikiwa kwa moto mkalii. Peleka moto kweli kwelii bila huruma.

JPM CHUMA!!!
Sasa ilikuwaje chuma kikadondoshwa hali ya kuwa kilimiliki majeshi yote?

Huoni alikuwa muoga aliyepitiliza hivyo aliamini mabavu yangesaidia kutisha watu na kujiweka salama?

Hata mwalimu asiyejua kufundisha huwa anakuwa mkali sana na mafimbo kibao mkononi ili wanafunzi wamuogope baada ya kugundua udhaifu wake.
 
Kifupi nchi hii haina succession plan wala vetting. Nchi yenye vetting huyo Magufuli hata form asingepewa. Kwa sababu alikuwa na shida kichwani
Hii ni jambo kubwa, walikuwa wanalifahamu, lakini bado wakampitisha.
Walitegemea nini haswa?
Si vizuri kulaumu lakini Jakaya Kikwete na Mzee Benjamin Mkapa alipitiwa na kitu gani?
Haya maswali lazima yapate majawabu.
 
hujafikilia criticaly, umewaza kwa ku trace background. Ukiuliza imekuwaje hadi akawa Rais, ni ile nyota kukubalika kwa falsafa zake , maono yake ambapo waliompinga wengi walikua working classes ambao si kundi kubwa la wananchi, so kundi kubwa liliweza kuyatambua mazuri yake na ndomana akawa Rais.

Walimchagua kwa vigezo vikuu vitatu. kwanza ubabe wake , utendaji wake wizara ya uvuvi na utendaji wake wizara ya uchukuzi, ukizungumzia madudu , ni kweli he was not perfect lakn jamii ilimjua kwa postivity zake na maono
Kila wizara alipopita alitia hasara zaidi kuliko faida kwa kukurupuka.

Refer meli ya uvuvi ilivyotumwaga kisheria na kuingia gharama kubwa. Meli ilikaa bandarini hadi ikashika kutu na mwishowe ikataka kuzama baada ya kutelekezwa.

Uuzaji nyumba za serikali kwa bei chee na kujiuzia yeye mwenyewe.
 
Tulimpigia kura wanyonge
Mnyonge ni nani?

Acha kuona ufahari kuitwa mnyonge wakati wewe ni binadamu uliyekamilika sawa na mwingine yeyote.

Kuitwa mnyonge ndo kichaka cha wanasiasa kuwapiga matukio ya kifisadi huku nyie wanyonge mkikata viuno kushangilia unyonge wenu.
 
Hili swali kwa sasa ni bypassed by events, ila kwavile umeuliza ilikuwaje, wakati tayari ameisha kuwa halina maana tena huku ni kuzidi tuu kumsema vibaya marehemu!.

Haya wewe unayouliza leo, akina sisi tuliyauliza tangu 2014 kabla hajawa na tukayaleta humu tukajadili, sababu za kwanini ni Magufuli pia nilizisema humu Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli ila zinaweza kusoma na watu wenye jicho la tatu pekee! Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli na wasio na jicho la tatu walibaki kuuliza Kwanini Pasco wa JF anaficha sababu alizoambiwa 2014 kuwa zitampeleka Magufuli Ikulu?

Maadam ametangulia mbele ya haki huu ni ushauri wangu kwako Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
Mkuu wewe ulikuwa unamfahamu kwa vile tu ulikuwa unamsikia.
Kuna ambao hatukuwa mbali sana, kwa vituko, afya na hata katia visivyo halali tulivisikia vingi tu. Mifano niliyotoa ni ile ilikuwa inajulikana.
Sasa kama inajulikana hadharani system ilikuwa usingizi, au ilipigwa ganzi.
P. Mayala you are better placed kuyafahamu haya.
Kwamba tunayaongelea sasa ni kuzuia yasitokee tena huko mbele.
System vetting isiwe kwa ushabiki.
 
Mpaka hii leo nafikiria, tena critically, ilifanyika vipi hadi John Pombe Mgufuli akafikia hatua ya kuwa Rais wa Tanzania?

Sijamfahamu Magufuli akiwa Rais, nilikuwa namfahamu toka akiwa Naibu Waziri pale Wizara ya Ujenzi. Kuingia ofisini tu siku alipoteuliwa na Rais mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, kuna mhandisi walisoma wote chuoni akamtania kuwa anafanya nini pale wizara ya mainjinia, Magufuli akamwambia hamjui yeye nani, na akaagiza atimuliwe, akatimuliwa.

Na huko alikopata ubunge, tunaambiwa kuna watu wamepotea au wamepotezwa.

Pale Wizara ya ujenzi, uwekaji mipaka ya barabara zimeliwa fedha nyingi sana nchi nzima. Uuzaji wa nyumba za serikali ndio usiseme, wakubwa wote walifaidika. Serikali ilikuw wapi?

Mimi nashindwa kuelewa kuwa kama vyombo vilikuwa vinamjua Magufuli ni kwa nini Mkapa na hata Kikwete walifumbia macho mapungufu yake?

Sitagusa mapungufu ya Magufuli akiwa madarakani, maana hata hawa viongozi wa leo serikalini walionja joto la jiwe.

Imefika wakati lazima tupate post mortem ya kisiasa ya kwa nini hii blunder ilifika kupata Rais ambaye hata uraia wake ulikuwa na maswali? la sivyo Magufuli no. 2 yupo round the corner.
Nina imani kuwa JF haifuti kumbukumbu zake tokea ilipoanzishwa, tunaweza kutafuta kumbukumbu zinazomhusu kila mchangiaji aliyewahi kuingia jukwaani humu.

Mimi simtetei Magufuli, na kumbukumbu za niandikayo humu zipo; lakini wakati huo huo, kinachonishangaza ni baadhi ya watu waliokuwa watetezi wakubwa wa Magufuli, leo hii ni kama wamepewa kazi maalum ya kumsema kwa ubaya wake.

Hili tu ndilo linalonishangaza sana na tabia hizi za kiTanzania ya leo.

Leo hii ni sifa kumshutumu mtu yule yule, ambaye jana tu tulikuwa mtetezi mkubwa bila ya kujali matendo yake machafu!
Hii ni tabia mbaya kabisa.
 
Issue ya kuhubiri daily mabaya ya Magu na kuacha mema yake,

Inaiharibia sana CCM kuliko upinzani.

SABABU ni kuwa Magu na sa100 wote ni CCM na wanatekeleza ilani Ile Ile Kila Mmoja Kwa wakati wake.

Kama CCM Pana wakubwa na wazee, waitane na kuonyana.

Wasipofanya hivyo wanatoa mwanya Kwa umma uamini kuwa MARIDHIANO yamelenga kupeleka CHARACTER ASSASSINATION Kwa Magu marehemu.

Wakiendelea kupuuza, Upinzani utapata ushindi wa mserereko.

Tusubiri.
Siyo siri, Magu hakuwa chaguo la kwanza la Kamati Kuu ya CCM kuwania Urais.
Umakundi na uhasama kati ya yale makundi ndiyo yaliyomuibua Magu ambaye wasifu wake kuukamata Urais vile vile siyo siri, ulikuwa hautoshelezi.
 
Nina imani kuwa JF haifuti kumbukumbu zake tokea ilipoanzishwa, tunaweza kutafuta kumbukumbu zinazomhusu kila mchangiaji aliyewahi kuingia jukwaani humu.

Mimi simtetei Magufuli, na kumbukumbu za niandikayo humu zipo; lakini wakati huo huo, kinachonishangaza ni baadhi ya watu waliokuwa watetezi wakubwa wa Magufuli, leo hii ni kama wamepewa kazi maalum ya kumsema kwa ubaya wake.

Hili tu ndilo linalonishangaza sana na tabia hizi za kiTanzania ya leo.

Leo hii ni sifa kumshutumu mtu yule yule, ambaye jana tu tulikuwa mtetezi mkubwa bila ya kujali matendo yake machafu!
Hii ni tabia mbaya kabisa.
Dunia haisimmi, kama wanaosema ati dunia isiame ili mtu ashuke.
Kuna mtu aliwahi kusema ukitaka kujua tabia ya mtu, mpe madaraka na pesa.
 
Hata mm najiuliza hili jiwe ilikuwaje likaingia ikulu?
siku anaapishwa ndiyo siku niliacha kutumia FB mpaka leo situmii na sijui kama nitakuja kutumia tena
Nilijua angefuatilia sana mitandao yule na mm ni mtu wa kuandika ningekiona
namkumbuka mwandishi (johanson mbwambo, Raia mwema, jamaa alipinga sana na alistaafu mwaka uleule akarudi kijijini kwao upareni}
 
Mpaka hii leo nafikiria, tena critically, ilifanyika vipi hadi John Pombe Mgufuli akafikia hatua ya kuwa Rais wa Tanzania?

Sijamfahamu Magufuli akiwa Rais, nilikuwa namfahamu toka akiwa Naibu Waziri pale Wizara ya Ujenzi. Kuingia ofisini tu siku alipoteuliwa na Rais mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, kuna mhandisi walisoma wote chuoni akamtania kuwa anafanya nini pale wizara ya mainjinia, Magufuli akamwambia hamjui yeye nani, na akaagiza atimuliwe, akatimuliwa.

Na huko alikopata ubunge, tunaambiwa kuna watu wamepotea au wamepotezwa.

Pale Wizara ya ujenzi, uwekaji mipaka ya barabara zimeliwa fedha nyingi sana nchi nzima. Uuzaji wa nyumba za serikali ndio usiseme, wakubwa wote walifaidika. Serikali ilikuw wapi?

Mimi nashindwa kuelewa kuwa kama vyombo vilikuwa vinamjua Magufuli ni kwa nini Mkapa na hata Kikwete walifumbia macho mapungufu yake?

Sitagusa mapungufu ya Magufuli akiwa madarakani, maana hata hawa viongozi wa leo serikalini walionja joto la jiwe.

Imefika wakati lazima tupate post mortem ya kisiasa ya kwa nini hii blunder ilifika kupata Rais ambaye hata uraia wake ulikuwa na maswali? la sivyo Magufuli no. 2 yupo round the corner.
Nasikia hata mkewe aliposikia mumewe ameteuliwa na CCM kugombea Kwa niaba ya chama aliuliza Kwa mshangao;
"Nyie nyie nyie, huyuhuyu John? Hamumujui kabisa huyu, atawavuruga shauri yenu mie simo"
 
Hili swali kwa sasa ni bypassed by events, ila kwavile umeuliza ilikuwaje, wakati tayari ameisha kuwa halina maana tena huku ni kuzidi tuu kumsema vibaya marehemu!.

Haya wewe unayouliza leo, akina sisi tuliyauliza tangu 2014 kabla hajawa na tukayaleta humu tukajadili, sababu za kwanini ni Magufuli pia nilizisema humu Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli ila zinaweza kusoma na watu wenye jicho la tatu pekee! Hakika Pasco alikuwa sahihi kuhusu Magufuli na wasio na jicho la tatu walibaki kuuliza Kwanini Pasco wa JF anaficha sababu alizoambiwa 2014 kuwa zitampeleka Magufuli Ikulu?

Maadam ametangulia mbele ya haki huu ni ushauri wangu kwako Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani
P
aachwe apumzike kwa amani? tusimpangie mungu cha kufanya
 
Nasikia hata mkewe aliposikia mumewe ameteuliwa na CCM kugombea Kwa niaba ya chama aliuliza Kwa mshangao;
"Nyie nyie nyie, huyuhuyu John? Hamumujui kabisa huyu, atawavuruga shauri yenu mie simo"
Watu wengi waliomjua tabia yake Magu na mapungufu yake , walishangazwa sana na kutoona mbali kwa Kamati Kuu ya CCM kumteua Magu.
Na sasa wamejionea wenyewe alivyoivuruga serikali na chama chenyewe.
 
Kabla ya kuwa Rais alikuwa mtu poa sana mm mwenyewe nilikuwa shabiki yake kwa namna alivyokuwa anachapa kazi akiwa wazir ktk wizara tofauti hasa ya miundombinu, shida ilianza alipoukwaa u Rais akabadilika kabisa hata wale walioshiriki kumpitisha wakawa wanashangaa.
Mtu anayesema leo hii kwamba Magufuli hakuwa na mambo mazuri aliyoyafanya kwa manufaa ya nchi atakuwa ni mwongo; kama ilivyo kwa yule anayeweza kusifu tu na kusahau mabaya kabisa, tena tabia mbaya kabisa kuwa nazo kama kiongozi wanchi.

Kwa bahati mbaya sana, mabaya ya Magufuli yalikuwa ni mabaya kiasi kwamba mtu unaona kwamba yanafuta hata yale mazuri aliyoyasimamia kama kiongozi.

Ingewezekana kama kwa miujiza hivi, kuyaondoa yale mabaya ya kishetani kabisa, na kubakiza haya mabaya ya kibinaadamu tu, Magufuli angekuwa ni kiongozi wa kukumbukwa sana katika historia ya nchi yetu.
 
Watu wengi waliomjua tabia yake Magu na mapungufu yake , walishangazwa sana na kutoona mbali kwa Kamati Kuu ya CCM kumteua Magu.
Na sasa wamejionea wenyewe alivyoivuruga serikali na chama chenyewe.
Sasa hapa, kama kweli jukwaa hili ni la "great Thinkers", hili ndilo jambo ambalo lingetafutiwa jibu.

Ilikuwakuwaje Magufuli ndiye akateuliwa.Sina shaka kabisa kuna sifa alizokuwa nazo zilizofanya akateuliwa; na hivyo hivyo, patakuwa na mapungufu ambayo hao wajumbe bila shaka waliona kwamba siyo mazito kuliko ssifa zilizowavutia kumteua.

Wakati huo huo, haitupasi kusahau sifa za hao hao waliopo kwenye kundi hilo la uteuzi.
Je hawa ni wajumbe wa aina gani hasa?
 
Mpaka hii leo nafikiria, tena critically, ilifanyika vipi hadi John Pombe Mgufuli akafikia hatua ya kuwa Rais wa Tanzania?

Sijamfahamu Magufuli akiwa Rais, nilikuwa namfahamu toka akiwa Naibu Waziri pale Wizara ya Ujenzi. Kuingia ofisini tu siku alipoteuliwa na Rais mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, kuna mhandisi walisoma wote chuoni akamtania kuwa anafanya nini pale wizara ya mainjinia, Magufuli akamwambia hamjui yeye nani, na akaagiza atimuliwe, akatimuliwa.

Na huko alikopata ubunge, tunaambiwa kuna watu wamepotea au wamepotezwa.

Pale Wizara ya ujenzi, uwekaji mipaka ya barabara zimeliwa fedha nyingi sana nchi nzima. Uuzaji wa nyumba za serikali ndio usiseme, wakubwa wote walifaidika. Serikali ilikuw wapi?

Mimi nashindwa kuelewa kuwa kama vyombo vilikuwa vinamjua Magufuli ni kwa nini Mkapa na hata Kikwete walifumbia macho mapungufu yake?

Sitagusa mapungufu ya Magufuli akiwa madarakani, maana hata hawa viongozi wa leo serikalini walionja joto la jiwe.

Imefika wakati lazima tupate post mortem ya kisiasa ya kwa nini hii blunder ilifika kupata Rais ambaye hata uraia wake ulikuwa na maswali? la sivyo Magufuli no. 2 yupo round the corner.
Mi wala sitii neno bali nasoma comments za wazee wa legacy baaasi!!!
 
Sasa hapa, kama kweli jukwaa hili ni la "great Thinkers", hili ndilo jambo ambalo lingetafutiwa jibu.

Ilikuwakuwaje Magufuli ndiye akateuliwa.Sina shaka kabisa kuna sifa alizokuwa nazo zilizofanya akateuliwa; na hivyo hivyo, patakuwa na mapungufu ambayo hao wajumbe bila shaka waliona kwamba siyo mazito kuliko ssifa zilizowavutia kumteua.

Wakati huo huo, haitupasi kusahau sifa za hao hao waliopo kwenye kundi hilo la uteuzi.
Je hawa ni wajumbe wa aina gani hasa?
Umedadavua kweli.
Sasa inabidi vikso vya Kamati Kuu CCM viwe na uwazi ili viwajibike kwa wananchi na si kwa CCM peke yake.
 
Lazima kuwa katili dhidi ya mapanya.

Fyekelea mbali mafisadi mpaka yakachanganyikiwa yakaamua kumdondosha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Chuma kile, hakikutepeta mpaka umautiii. Ni mwendo wa kukaza kamba kweli kweliiii ikibidi hadi uhai kutoka!

Ametufundisha somo kubwaa kwamba mafisadi na majizii yanahitaji kushughulikiwa kwa moto mkalii. Peleka moto kweli kwelii bila huruma.

JPM CHUMA!!!
Panya buku wa kwanza kabisa ni yule jambazi aliyeficha fedha China
 
Back
Top Bottom