Mpaka leo najiuliza, ilikuwaje mpaka Magufuli akawa Rais?

Sasa ilikuwaje chuma kikadondoshwa hali ya kuwa kilimiliki majeshi yote?

Huoni alikuwa muoga aliyepitiliza hivyo aliamini mabavu yangesaidia kutisha watu na kujiweka salama?

Hata mwalimu asiyejua kufundisha huwa anakuwa mkali sana na mafimbo kibao mkononi ili wanafunzi wamuogope baada ya kugundua udhaifu wake.
 
Kifupi nchi hii haina succession plan wala vetting. Nchi yenye vetting huyo Magufuli hata form asingepewa. Kwa sababu alikuwa na shida kichwani
Hii ni jambo kubwa, walikuwa wanalifahamu, lakini bado wakampitisha.
Walitegemea nini haswa?
Si vizuri kulaumu lakini Jakaya Kikwete na Mzee Benjamin Mkapa alipitiwa na kitu gani?
Haya maswali lazima yapate majawabu.
 
Kila wizara alipopita alitia hasara zaidi kuliko faida kwa kukurupuka.

Refer meli ya uvuvi ilivyotumwaga kisheria na kuingia gharama kubwa. Meli ilikaa bandarini hadi ikashika kutu na mwishowe ikataka kuzama baada ya kutelekezwa.

Uuzaji nyumba za serikali kwa bei chee na kujiuzia yeye mwenyewe.
 
Tulimpigia kura wanyonge
Mnyonge ni nani?

Acha kuona ufahari kuitwa mnyonge wakati wewe ni binadamu uliyekamilika sawa na mwingine yeyote.

Kuitwa mnyonge ndo kichaka cha wanasiasa kuwapiga matukio ya kifisadi huku nyie wanyonge mkikata viuno kushangilia unyonge wenu.
 
Mkuu wewe ulikuwa unamfahamu kwa vile tu ulikuwa unamsikia.
Kuna ambao hatukuwa mbali sana, kwa vituko, afya na hata katia visivyo halali tulivisikia vingi tu. Mifano niliyotoa ni ile ilikuwa inajulikana.
Sasa kama inajulikana hadharani system ilikuwa usingizi, au ilipigwa ganzi.
P. Mayala you are better placed kuyafahamu haya.
Kwamba tunayaongelea sasa ni kuzuia yasitokee tena huko mbele.
System vetting isiwe kwa ushabiki.
 
Nina imani kuwa JF haifuti kumbukumbu zake tokea ilipoanzishwa, tunaweza kutafuta kumbukumbu zinazomhusu kila mchangiaji aliyewahi kuingia jukwaani humu.

Mimi simtetei Magufuli, na kumbukumbu za niandikayo humu zipo; lakini wakati huo huo, kinachonishangaza ni baadhi ya watu waliokuwa watetezi wakubwa wa Magufuli, leo hii ni kama wamepewa kazi maalum ya kumsema kwa ubaya wake.

Hili tu ndilo linalonishangaza sana na tabia hizi za kiTanzania ya leo.

Leo hii ni sifa kumshutumu mtu yule yule, ambaye jana tu tulikuwa mtetezi mkubwa bila ya kujali matendo yake machafu!
Hii ni tabia mbaya kabisa.
 
Siyo siri, Magu hakuwa chaguo la kwanza la Kamati Kuu ya CCM kuwania Urais.
Umakundi na uhasama kati ya yale makundi ndiyo yaliyomuibua Magu ambaye wasifu wake kuukamata Urais vile vile siyo siri, ulikuwa hautoshelezi.
 
Dunia haisimmi, kama wanaosema ati dunia isiame ili mtu ashuke.
Kuna mtu aliwahi kusema ukitaka kujua tabia ya mtu, mpe madaraka na pesa.
 
Hata mm najiuliza hili jiwe ilikuwaje likaingia ikulu?
siku anaapishwa ndiyo siku niliacha kutumia FB mpaka leo situmii na sijui kama nitakuja kutumia tena
Nilijua angefuatilia sana mitandao yule na mm ni mtu wa kuandika ningekiona
namkumbuka mwandishi (johanson mbwambo, Raia mwema, jamaa alipinga sana na alistaafu mwaka uleule akarudi kijijini kwao upareni}
 
Nasikia hata mkewe aliposikia mumewe ameteuliwa na CCM kugombea Kwa niaba ya chama aliuliza Kwa mshangao;
"Nyie nyie nyie, huyuhuyu John? Hamumujui kabisa huyu, atawavuruga shauri yenu mie simo"
 
aachwe apumzike kwa amani? tusimpangie mungu cha kufanya
 
Nasikia hata mkewe aliposikia mumewe ameteuliwa na CCM kugombea Kwa niaba ya chama aliuliza Kwa mshangao;
"Nyie nyie nyie, huyuhuyu John? Hamumujui kabisa huyu, atawavuruga shauri yenu mie simo"
Watu wengi waliomjua tabia yake Magu na mapungufu yake , walishangazwa sana na kutoona mbali kwa Kamati Kuu ya CCM kumteua Magu.
Na sasa wamejionea wenyewe alivyoivuruga serikali na chama chenyewe.
 
Mtu anayesema leo hii kwamba Magufuli hakuwa na mambo mazuri aliyoyafanya kwa manufaa ya nchi atakuwa ni mwongo; kama ilivyo kwa yule anayeweza kusifu tu na kusahau mabaya kabisa, tena tabia mbaya kabisa kuwa nazo kama kiongozi wanchi.

Kwa bahati mbaya sana, mabaya ya Magufuli yalikuwa ni mabaya kiasi kwamba mtu unaona kwamba yanafuta hata yale mazuri aliyoyasimamia kama kiongozi.

Ingewezekana kama kwa miujiza hivi, kuyaondoa yale mabaya ya kishetani kabisa, na kubakiza haya mabaya ya kibinaadamu tu, Magufuli angekuwa ni kiongozi wa kukumbukwa sana katika historia ya nchi yetu.
 
Watu wengi waliomjua tabia yake Magu na mapungufu yake , walishangazwa sana na kutoona mbali kwa Kamati Kuu ya CCM kumteua Magu.
Na sasa wamejionea wenyewe alivyoivuruga serikali na chama chenyewe.
Sasa hapa, kama kweli jukwaa hili ni la "great Thinkers", hili ndilo jambo ambalo lingetafutiwa jibu.

Ilikuwakuwaje Magufuli ndiye akateuliwa.Sina shaka kabisa kuna sifa alizokuwa nazo zilizofanya akateuliwa; na hivyo hivyo, patakuwa na mapungufu ambayo hao wajumbe bila shaka waliona kwamba siyo mazito kuliko ssifa zilizowavutia kumteua.

Wakati huo huo, haitupasi kusahau sifa za hao hao waliopo kwenye kundi hilo la uteuzi.
Je hawa ni wajumbe wa aina gani hasa?
 
Mi wala sitii neno bali nasoma comments za wazee wa legacy baaasi!!!
 
Umedadavua kweli.
Sasa inabidi vikso vya Kamati Kuu CCM viwe na uwazi ili viwajibike kwa wananchi na si kwa CCM peke yake.
 
Bahati katika maisha inashinda juhudi na maarifa.
Tumuombeni Mungu tuwe na bahati huku tukifanya kazi kwa bidii
 
Panya buku wa kwanza kabisa ni yule jambazi aliyeficha fedha China
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…