Mpenzi wangu anaficha meseji kwenye simu yake, nahisi anawasiliana na wanaume wengine

Mpenzi wangu anaficha meseji kwenye simu yake, nahisi anawasiliana na wanaume wengine

Kweli wanaume tunapitia mengi, mbali na streess za kutafuta hera lakini streess za mapenzi ndizo zimesababisha wanaume tunakufa kwa magojwa ya moyo kabla ya umri wa uzee,

Kosa lako ni kushika simu ya huyo mpenzi wako.
Kosa la pili kama unafanya naye uzinzi ukafanya kwa kujiamini kuwa nipo peke yangu basi utambue kuwa unajiloga mwenyewe.
Mwisho nakushauri kuwa kama unahisi moyo wako hauwezi endelea naye basi achana naye kabisa maana utakuja kuua bira kukusudia kama yule jamaa wa Tabora aliyetanganzwa magazetini. Naamini umenielewa
 
Ifike mahali sisi binadamu wa leo tukue. I think we need maturity katika maisha ya mahusiano. Siku hizi matatizo ni mengi yasiyo na kichwa wala miguu na ni kwa sababu hatutaki kukua.

I think unapokutana na mtu embu tusichunguzane past tuiandike future pamoja. Kila mtu ana flaws hakuna mkamilifu.

Kama kweli unampenda mtu then things will fall into place lakini ndo kuangalia simu za mwenza wako huanzisha a stupid past. #rudikalalejuan#
Saw ila ila inakata stimu upo na mtu simu anaficha ficha bora
 
Kuna msichana nimekuwa nae kwenye mahusiano kwa muda wa miezi 7 sasa na siku kadhaa.

Na tulipanga hapo baadae tuje tuwe na mwisho mzuri (ndoa)

Katika kipindi chote hicho ambacho tulikua pamoja tuliweza kuwa na furaha japo pia kukwazana kupo kama binadamu, lakini tulikua tunaongea yanaisha na kurudisha uelewa kati yetu.

Pia tangu nimekua nae, baada ya muda nilianza kukagua simu yake, ili kuangalia je? Kama mwenzangu kweli ana nia na mimi au yeye ana mambo yake mengine anayowaza na watu wengine.

Katika hatua hiyo ya ukaguzi wa simu yake nilishawahi kukuta baadhi ya sms za mapenzi, ikiwa ni namba ngeni kabisa ndio iliyoingia zinaongoza kutuma kutuma sms hizo kwenye simu yake, na nilipojaribu kumuuliza mwenzangu yeye alijaribu kujitetea kwa kusema hizo namba hazifahamu na kudai tu ni watu ambao wanataka kumuharibia mahusiano.

Pia kuna uzi ambao nishawahi kuleta hapa kuhusu kutoelewana mimi na yeye, kutokana na simu ambayo nilipokea wakati wa usiku na huyo mtu alidai kwamba anamfahamu huyu msichana kuliko hata mimi ninavyomfahamu, na pale nilipomuasha usiku kujibu madai ya huyo mtu alianza kulia usiku hadi mida ya saa tisa(9) usiku akidai ya kuwa namuonea tu, lakini yeye hamfahamu.

Baada ya hapo hivi, juzi wakati naangalia whatsapp yake nilikuta chat ambazo ameweka password, lakini nilianza kuhisi pia kuna kitu hakipo sawa.. Baada ya hapo nilimuuliza kuhusu chat hizo lakini yeye alidai ya kuwa nisiwe na wasi wasi kwani hakuna baya linaloendelea.

Na ndipo siku ya jana nilimsihi sana atowe password hizo ili niangalie vitu hivyo ambavyo anachati na wao watu.

Sasa katika kubishana nilifanikiwa kuchukua simu ile ili aniambie password za kwenye zile chat, lakini aligoma.

Hivyo niliamua kuondoka na ile simu mpaka pale ninapokaa, na yeye kunifuata baadae... Pia hapo nyumbani tulibishana kwa muda sana, lakini aligoma kutoa password.... Ndipo aliponiambia nimpe simu ili atoe Mwenyewe hizo password... Kwa kuwa nilishahisi kuna vitu ambavyo anaficha na lazima vitakuwa ni viovu, niliamua kumpa simu yake.

Baada ya kuchukua simu, hakutoa zile password, ila badala yake aliamua kufuta zile chat zote... Hivyo kwa kuwa alifanya vile kwa makusudi, nilimuamuru aondoke zake. Lakini pia aligoma kuondoka... Hivyo nilitumia nguvu kumuondoa apo nyumbani kwa kuwa nilishahisi tu mambo yanayoendelea sio mema hata kidogo.

Hivyo leo alinisihi sana tuongee yaishe... Lakini kabla ya hapo kuna maswali nilitaka kumuuliza na katika kumbana sana niligundua mmoja kati ya wale watu aliokuwa akiwasiliana nao ni bwana wake wa kwanza kama alivyodai(ex boyfriend) na hawa wengine alidai tu, ni watu ambao wanamtongoza tu lakini hawajui...

Na kwa kuwa nilishaanza kumchunguza muda sana alisema ukweli wote

Sasa mimi binafsi nilimuambia ya kuwa sina tena imani na wewe, akaanza kama kawaida kulia usiku kucha, anadai nimsamehe...

Je wakuu hapo ingekua imetokea kwa upande wako ungefanyaje?
Achana nae,mwanamke anae chepuka wakati upo nae kwenye mahusiano kama mpenzi,girl friend,hata ukiingia nae kwenye ndoa atachepuka tu,
Huyo achana nae,utapata Ngoma ukicheza nae,tafuta mwingine.
 
Haya uliyokutana nayo yanaumiza sana ila hauko peke yako, wengi wanaumizwa na mambo kama hayo, na ukweli ni kwamba mtalaka hatongozwi, namaanisha yule x wake akihitaji kupasha kiporo moto ni yeye tu hakuna kizuizi. Hawa wenzetu ni wadhaifu sana hawana msimamo. Hata wewe ukimjaribu x wako kama hamkugombana haijalishi kama ameshaolewa ila huduma utapewa,. sasa huyo hata ukisamehe na ukamuoa ni vigumu kuwatenganisha.
 
Huko ndo kulia kwenyewe,ungekuwa hit and run kama mnavyojisifu wanaume usingegongewa mchana kweupe afu bado ukomae hapohapo...
Hv bado unapigaga nyeto eeeh ..maana naona mihemko kama yote
 
Hakuna mwana mke ambae hatongozwi hata kidogo hiyo sahau,hata mama zetu pamoja na uzee wao wanatongozwa na wazee wenzao huko,zingatia hii kauri ita kusadia hakuna mwana mke wa peke yako.NB.hata mama yetu samia anatongozwa sema mazingira yana mbana.
Hahahaha [emoji23][emoji1787][emoji23][emoji1787] mkuu unapata wap Ujasiri wa kumzungumzia SSH ..kwenye mada dhaifu kama hii ....jitafakari upya mkuu
 
Unapoamua kumchunguza mty hasa kukagua simu yake uwe na majibu kabisa kwamba je nikikuta madudu huko nitaamua nini.

Kama hujui utaamua nini ni bore ukaachana nayo. Mi huwa nakagua simu zao tu kwa kujifurahisha, ili nijue tu nae ni muongo muongo kama mimi au namchezea tu mtoto wa watu.

Nikikuta ana madudu mengi aisee nakua namtoa kwenye hesabu namuweka kwenye kundi la kimasihara coz sijui yeye kaniweka kundi gani. Ila kama ni mtoto mwema sijakuta madudu namvika uwife material.

Ila ogopa sana umeshika simu ya mtu inbox zote ziko empy, call records empty [emoji23][emoji23], aisee huyo ni zaidi ya mafia.

The last paragraph [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Haya uliyokutana nayo yanaumiza sana ila hauko peke yako, wengi wanaumizwa na mambo kama hayo, na ukweli ni kwamba mtalaka hatongozwi, namaanisha yule x wake akihitaji kupasha kiporo moto ni yeye tu hakuna kizuizi. Hawa wenzetu ni wadhaifu sana hawana msimamo. Hata wewe ukimjaribu x wako kama hamkugombana haijalishi kama ameshaolewa ila huduma utapewa,. sasa huyo hata ukisamehe na ukamuoa ni vigumu kuwatenganisha.
Ndo mzizi wa tatizo ulipo Yan ni wadhaifu mnoo mnoo
 
Ifike mahali sisi binadamu wa leo tukue. I think we need maturity katika maisha ya mahusiano. Siku hizi matatizo ni mengi yasiyo na kichwa wala miguu na ni kwa sababu hatutaki kukua.

I think unapokutana na mtu embu tusichunguzane past tuiandike future pamoja. Kila mtu ana flaws hakuna mkamilifu.

Kama kweli unampenda mtu then things will fall into place lakini ndo kuangalia simu za mwenza wako huanzisha a stupid past. #rudikalalejuan#
Lakini ni bora kuujua uozo wa mtu mapema, kuliko kuvumilia upumbavu. Haya maswala ya kujifanya hutaki kuangalia mwenendo wa mpenzi wako kisa unampenda ndo matokeo yake unaletewaimba ya ex boyfriend ulee.

Kupuuzia Lila kitu ni utoto pia.
 
Back
Top Bottom