Mrejesho wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika 3 - 4 January 2024

Nashukuru sana kwa maelezo yako mazuri na marefu. Umekuwa na msisitizo kuhusu kuwa na katiba mpya. Na umeibua mada ya kuhusu wazanzibar waulizwe. Sasa ninakuuliza nani awaulize hao wazanzibar? Je, huku bara hawatakiwi kuulizwa kuhusu muungano?

Kuwauliza wazanzibar na wa bara hayo ndiyo maridhiano kiongozi wangu.

Je, tuendelee na ile ya Warioba au tuifanyie marekebisho.

Nimeongelea kuhusu EAC maana ndiyo direction yetu kuwa na federal state. Sasa unaposema miaka 25, mbona ni michache sana? Kwahiyo tuunde katiba itakayodumu miaka 25 tu? Katiba isiyoangalia mwelekea wa EA federation?

Mimi nadhani bado 4R zinahitajika. Lazima tukae kama nchi tujadiliane na kuridhiana. Tukienda kwa mihemko tutajikuta tunaunda katiba mbayo haitadumu.

Yangu ni hayo.
 
Kama mimi ni chawa wewe ni funza.
Hamna shida chawa. Huo mkutano wa kitapeli ulikuwa ni mkutano wa kumpa promo rais na kuhadaa ulimwengu kuwa anataka mabadiliko. Lakini ukweli ni kuwa hakuna jipya lolote toka kwenye mkutano huo.
 
Hamna shida chawa. Huo mkutano wa kitapeli ulikuwa ni mkutano wa kumpa promo rais na kuhadaa ulimwengu kuwa anataka mabadiliko. Lakini ukweli ni kuwa hakuna jipya lolote toka kwenye mkutano huo.
Sasa unashauri mikutano isifanyike? Kifanyike kitu gani?
 
Sasa unashauri mikutano isifanyike? Kifanyike kitu gani?

..kimekuwa na ucheleweshaji wa makusudi na hujuma dhidi ya mchakato wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

..Mikutano anayoitisha na Tume na vikosi kazi anavyounda ni sehemu ya mkakati wa Rais Samia kupoteza muda ili Katiba Mpya na Tume Huru visipatikane kabla ya uchaguzi, au hata ktk utawala wake.

..Mikutano aliyoitisha na Tume alizounda haijafuatiwa na hatua za dhati za utekelezaji wa maazimio au mapendekezo yaliyotolewa.

..Mazungumzo ya maridhiano kati ya chama chake na Chadema yamevunjika na analalamikiwa kwa kukataa sehemu kubwa ya mapendekezo ya wenzake.

..Pamoja na Raisi kudai anataka maridhiano lakini ameendelea kuteua maofisa ktk jeshi la Polisi ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kukiuka haki za wananchi mbalimbali haswa wapinzani.

..Mwisho, maridhiano hayawezi kukamilika bila kuwaomba radhi, kuwafuta machozi, na kuwapa haki, Watanzania ambao haki zao zilivunjwa na tawala mbalimbali za nchi hii. Kwa mfano, taifa linapaswa kuelezwa nini kilimtokea Abdulah Kassim Hanga na wengine ambao walikamatwa na vyombo vya dola na hawajapatikana mpaka leo.


..
 
Nashukuru kwa maelezo yako.
Umeeleza kuwa sehemu kubwa ya mapendekezo yaliyotolewa na chadema yalikataliwa. Je unaweza kutueleza ni mapendekezo yapi hayo?

Unaweza kuyaorodhesha hapa

Kuna kamati ya maridhiano iliundwa wakiwemo Chadema je chadema wanataka mapendekezo yao tu yakubaliwe?

Tumeona kwenye mkutano Salum Mwalimu ambaye ni kiongozi mkubwa ndani ya Chadema akipongeza jitihada hii ya 4R, Je msimamo wa Chadema ni nini sasa?

Mbowe amekuwa akilalamikiwa miaka mingi kuwa hataki kuondoka kwenye uenyekiti. Je, kiongozi huyo atakuwa credible kuzungumzia Demokrasia ya nchi nzima wakati ameshindwa ndani ya chama chake? Je, hatuwezi kuwa na shaka kwamba Mr. Mbowe anatafuta mslahi yake binafsi kupitia Chadema? Je, unaweza kutoa maelezo ya kuuaminisha umma kuwa Chadema wanaheshimu na Kufuata Demokrasia?

Mwisho na si kwa uchache kutokana na makando kando ya kutokuaminiana baina ya Chama na Chama nani sasa atakaye mfunga paka kengere?

Utarudi kwenye falsafa ya 4R na kuipa credit.

Karibu.
 

..Kama vyama haviaminiani inabidi
atafutwe msuluhishi wa kimataifa.

..Kwa mfano, mazungumzo yaliyopelekea muafaka wa kwanza kati ya Ccm na Cuf yalisimamiwa na Bw.Emeka Anyauko Mnigeria aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola.

..Moja ya mapendekezo ya Chadema kuhusu maridhiano ilikuwa ni Raisi kuunda Tume ya Haki, Ukweli, na maridhiano, ili kushughulikia malalamiko ya wananchi mbalimbali kuhusu ukiukwaji wa haki zao.

..Chadema wanaamini pendekezo hilo ni nguzo muhimu ya kulirudisha taifa ktk mstari wa haki na usawa kwa watu wote. Labda utueleze kwanini Rais na Ccm wamekataa pendekezo hilo kama kweli wanaamini ktk 4R.
 
Sasa unashauri mikutano isifanyike? Kifanyike kitu gani?
Tunataka katiba mpya ya rasimu ya jaji Warioba. Tulikuwa kwenye hatua ya kura ya maoni. Ni utekelezaji umebaki. Hii mikutano ambayo watu wanafanya kisha maoni yao hayafanyiwi kazi ni kupotezeana muda. Kiuhalisia hakuna dhamira ya dhati zaidi ya kiki za kisiasa zisizo na tija.
 
Sasa JokaKuu nashindwa kuelewa point ikiyopo hapa.

Sasa huyo msuluhishi wa kimataifa anatafutwa na nani? Tutakuwa tunaendelea na paradox na hakuna kitu amnacho kitafanyika. Yaani tuanze hatua ya kutafuta msuluhishi aweze kukubalika pande zote. Halafu tuanze conflict resolution tutaandika lini katiba sasa?

Sasa tunarudi tena kwa Rais huyu huyu aliyeanzisha 4R Chadema wanamtaka aunde Tume ya haki. Sasa ndugu yangu hawa Chadema watamuamini Rais kuunda tume ya haki?

Tayari kuna miswada ya vyama vya siasa, Mswada wa Tume ya Uchaguzi, nk. Ndani ya hiyo miswada kuna majibu ya hayo madai.

Sasa unataka kumlazimisha Rais afanye vyote ambavyo Chadema wanadai? Why? Kwenye maridhiano kuna kupata na kuachia. Kwanini wewe utake vyote vyako tu?

Hata ile hatua ya kumuomba Rais aunde Tume ya Haki bado ni sehemu ya Falsafa ya 4R.

Falsafa hii ipo na mizizi mirefu sana. Ukiamua kuielewa na kuifuata hata kwenye familia inataweza kufanya kazi.

Bado 4R Idea ina make sense.
 
Nadhani mtu wangu kuna jambo umeliruka. Kumbuka kulikuwa na bunge la katiba. Na kwenye bunge la katiba wengine walitoka. Sasa kura za maoni zingepigwaje?

Rasimu ya Warioba ilitakiwa kujadiliwa kwenye bunge maalum la Katiba. Hilo lilikuwa takwa la kisheria. Sasa tupigie kura ipi sasa. Na tayari ile sheria iliyofanya iundwe rasimu ya Warioba ni outdated, ni lazima iundwe sheria nyingine.

Sasa basi unataka kitu gani kifanyike? Tuendelee tu kwa matakwa yako bila kufuata utaratibu na sheria?
 
Nasema hivi acha upotoshaji usio na tija yoyote. waliotoka kwenye bunge la katiba ni wale waliogoma kuona maoni halali ya wananchi yanachezewa na ccm na vibaraka wake ndani ya bunge lile. Lakini bunge lile halikusimama, liliendelea Hadi kupatikana katiba pendekezwa ambayo ilisubiri kura ya maoni, ila dhalimu magu alipoingia madarakani akasema kipaombele chake sio katiba mpya. Mchakato ukasimamia hapo kwenye hatua ya kura ya maoni.

Wahuni hao wa ccm Sasa hivi wamekuja na zubaisha bwege eti Hadi elimu itolewe ya katiba, kama vile katiba mpya ni jambo linalohitaji stashahada kwa Kila mwananchi Ili litimie. Ndio maana nakuambia huo mkutano lengo lake lilikuwa ni kumtafutia Rais sifa asizostahili kuwa ana Nia njema. Lakini kwa tunaofahamu tabia za viongozi wa ccm, tunajua ulikuwa ni mkutano wa kupotezeana muda tu.
 
Haitakiwi rais akubali yote yanayitakiwa na cdm, inatakiwa mambo yote yanayoweza kuweka mazingira ya haki kutendeka yawepo. Sio suala la rais anataka lipi na lipi hataki. Ugumu wa hayo ya cdm kukataliwa ndio kilio Cha muda wote wa ukosekanaji wa haki. Isitoshe cheo Cha urais ndio tatizo kubwa ya upatikanaji wa haki hapa nchini. Sasa unataka tukubali tu rais kuwa kinara wa upatikanaji wa haki, wakati ukweli wa matendo hauendani? Hakuna mapendekezo yoyote ya msingi yanachukuliwa kwenye hiyo propaganda iitwayo 4R zaidi ya hadaa.

Rasimu ya Warioba ilikuwa na maoni halali ya wananchi, na katiba yake ingekuwa ya miaka 50+, ila kwakuwa haikuwa na maslahi kwa ccm, Bali maslahi kwa taifa ndio maana wakaishia kuichakachua. Hakuna wajinga wa kupoteza muda na hizo mbwembwe/hadaa za 4R, wakati kinachotakiwa kinafahamika. Bakini nyie kusifia hizo hadaa za 4R, lakini wenye akili zetu tunajua ni usanii kama usanii mwingine.
 
Kwanza swali sijakuuliza wewe. Halafu nilichouliza ni tofauti na maelezo yako.

Jamaa yako kauliza kuhusu kutafuta msuluhishi. Nikauliza ni nani amtafute huyo msuluhishi?

Jamaa yako kauliza pendekezo la Rais kuunda tume ya haki. Sasa huku unamlalamikia rais huku unamuomba aunde Tume ya haki, hiyo tume ya haki iundwe kutokea wapi?

Jibu haya maswali kwanza acha mbwembwe.
 
Walipo toka kwenye bunge la katiba ulitaka na wengine watoke? Je, unalijua lengo la Bunge la katiba?
 
Kwa taarifa yako hawamuombi rais kama mtu, Bali mamlaka ya rais kutokana na katiba hii mbovu inavyotaka. Na wanaomba kwa kuwa hakuna jinsi, lakini kiuhalisia rais hapaswi kuunda hiyo tume, maana yeye na chama chake ni sehemu ya huo uhalifu.
 
Walipo toka kwenye bunge la katiba ulitaka na wengine watoke? Je, unalijua lengo la Bunge la katiba?
Kwa kukusaidia tu, kususia vikao vya bunge ni sehemu ya kutaka mchakato uheshimiwe. Hao waliobaki ndio walikuwa wanachezea maoni ya wananchi, ulitegemea watoke halafu maoni ya wananchi yakwpitishwa huoni ingekuwa hatari kwa hao majizi wa ccm?
 
Kwa taarifa yako hawamuombi rais kama mtu, Bali mamlaka ya rais kutokana na katiba hii mbovu inavyotaka. Na wanaomba kwa kuwa hakuna jinsi, lakini kiuhalisia rais hapaswi kuunda hiyo tume, maana yeye na chama chake ni sehemu ya huo uhalifu.
Rais kaanzisha 4R kwa lengo la kuelekea kwenye mabadiliko ya katiba. Sasa unasema Rais wamemuomba kwanini unataka ombi lao liwe ni lazima?

Kwani hao Chadema weshikili hati milki ya watanzania? Kwanini wanalazisha takwa lao tu na wenzao wakikataa wanasusa? Lazima 4R zifundishwe kwa watu wote ili ustahimilivu uwepo.
 

..bunge la katiba chini ya Samuel sitta na Samia Suluhu waliandika katiba ambayo ilipaswa kupigiwa kura ya maoni.


..sijui kwanini Rais Samia na wenzake ktk Ccm wamejizimisha data kuhusu katiba waliyoipitisha wakati wa bunge maalum.

..Ndio maana nasema Rais Samia ni mlaghai. Kama ana nia ya dhati kuhusu Katiba mpya angeanza kutetea ile waliyoipitisha akiwa naibu kiongozi wa bunge la katiba.

..Badala yake kila siku anahamisha magoli. Kwanza alianza na kisingizio cha kujenga uchumi. Baadae akaja na kesi ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti Mbowe. Majuzi alileta hoja kwamba Watanzania tunahitaji kupatiwa mafunzo kuhusu Katiba.
 
Kwa kukusaidia tu, kususia vikao vya bunge ni sehemu ya kutaka mchakato uheshimiwe. Hao waliobaki ndio walikuwa wanachezea maoni ya wananchi, ulitegemea watoke halafu maoni ya wananchi yakwpitishwa huoni ingekuwa hatari kwa hao majizi wa ccm?
Nimekuuliza unalijia lengo la Bunge Maalum la katiba? Je unazijua hadidu za rejea za bunge maalum la katiba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…