PreGE2025 Mrema, Kileo, Kigaila, Salumu Mwalimu, Devotha Minja na G 55 wengine rasmi watua CHAUMMA. Walijifanya kukataa, kiko wapi!

PreGE2025 Mrema, Kileo, Kigaila, Salumu Mwalimu, Devotha Minja na G 55 wengine rasmi watua CHAUMMA. Walijifanya kukataa, kiko wapi!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Yeah na vyeo viko hivi
Mrema, Kigaila, Salum na Devotha Minja wameingia kikao cha kamati kuu ambapo watapewa vyeo
1. Kigaila makamu mwenyekiti bara
2. Salu Mwalim makamu mwenyekiti Zanzibar
3. Mrema Katibu mkuu
4. Devotha Minja atakuwa kiongozi wa wanawake
Chauma ilikuwa jeshi la mtu mmoja, Rungwe pekee bila viongozi wengine?
 
Unaona jinsi Russia anavyojitahidi kutengeneza buffer zone - no man's land - kule Ukreni, same na hapa kwetu hiki chama inaelekea ni buffer party ya kuzuia mishale mikali ya Sidiemu isifike Sisiemu Lumumba.

Sasa ni kung'atana CHAUMA kwa CHADEMA, huku mama la mama Sisiemu yuko palee anachekelea na kujizolea heshima na kura kedekede.
Nadhani Chauma ajenda yao kubwa itakuwa ni Chadema, wao Chadema inabidi waFocus na NoReformsNoElection tu.
 
Askari wanajiongezea idadi ya wapigwa virungu.

Sasa CHAUMMA itapata spotlight ambayo hawakua na kazi nayo
 
Informer wenu nipo kwenye Mkutano Mkuu wa CHAUMMA. Nimekuja na hii taarifa ya ndani kabisa kutoka jikoni. Soon watatangaza rasmi.

Tukio hili lipo Golden Tulip, Dar es Salaam. Taarifa zaidi zitakujia.
1747653889266.jpeg
 
Kinachoshangaza ni jinsi mnavyofuatilia watu ambao mlisema walikuwa mizigo, magunia ya misumari, punda n.k. Hawa wanatafuta mahali ambapo wataheshimiwa na kusikilizwa. Rungwe ni msikivu, tofauti na Lissu, Heche na Mnyika.
Mimi nilidhani wangeenda ACT-WAZALENDO lakini yote ni heri.

Amandla...
 
Ama kweli njaa mbaya sana.
Anyway wamenunuliwa kwa shilingi ngapi?
we
Wakuu,

Informer wenu nipo kwenye Mkutano Mkuu wa CHAUMMA. Nimekuja na hii taarifa ya ndani kabisa kutoka jikoni. Soon watatangaza rasmi.

Tukio hili lipo Golden Tulip, Dar es Salaam. Taarifa zaidi zitakujia.

Pia, Soma: Inasemekana G55 wanahamia CHAUMMA, kupewa nafasi za uongozi kukamiliasha 5% ya wagombea wa upinzani

we bwege fanya mambo yako acha kufuatilia watu.
 
Back
Top Bottom