Heri ya Pasaka?
Heri ya Mfungo kwa WAISLAMU.
Ndugu zangu wataalamu wa Masuala ya Biblia na Quran NAOMBENI MSAADA wa hili swali linalonisumbia Daima?
JE ni KWELI QURAN ilishushwa kutoka MBINGUNI?
1. Inamaana Mungu alitengeneza karatasi.
2. Akatafuta Penny Compyuta printer nk?
3. Mbona ni tofauti sana na KIPINDI Cha Musa Mungu aliandika zile Amri Kumi kwenye mabamba mawili ya mawe na kumpa Musa kwenye Mlima Sinai. (Kutoka 24:12-18) Zile Amri Kumi zimeorodheshwa kwenye Kutoka 20:1-17 na Kumbukumbu la Torati 5:6-21.
4 JE tuna ushahidi Gani kama Quran ilishushwa na Mungu?
Natamani Mjadala Huu tujikite kwenye kujibu hoja sio Dini .
Natanguliza shukrani nyingi.
Habari mkuu, Naimani ni Mzima wa Afya...
Kuhusu swali la Je, ni kweli Qur-an ilishushwa kutoka mbinguni?????
Swali lako ni swali ambalo sio swali lililokamilika. Japo watu wengi wanajaribu kukujibu kwa maarifa mazuri ya hekima na wengine kukukashifu wewe pamoja na dini nyingine ambayo hawajui kama wewe upo kwenye dini hiyo au laa!!!
Kwanza kabisa tuangalie hali uliyonayo katika kuuliza swali lako!
- Je, unauliza ili kupata jibu la ndio au hapana?
- Je, unauliza kwa sababu ya kujenga hoja?
- Je, unauliza kwa sababu ya kukebehi?
- Je, unaulizia kwa sababu ya kuongeza elimu?
Vyovyote vile dhamira yako ya kuuliza unaifahamu wewe mwenyewe na nafsi yako. Lakini yoyote anaetaka kukujibu yapaswa afahamu anamjibu mtu gani na wa hali gani?
kwa maana kila mtu anajibiwa kulingana na hekima ya muulizaje.
Ikiwa swali lako unauliza na wewe ni Mtu anaeamini uwepo wa Mungu haijarishi ni dini gani basi kuna jinsi ya kujibiwa kwako..
Lakini vile vile ikiwa unauliza na wewe ni mtu ambaye hata ukisikia neno Mungu unahisi kichefu chefu na kuona ni uongo. Basi pia kuna jinsi wewe unataka kujibiwa pia.....
Kuna maswali ukitaka kumjibu mtu lazima utumie roho na imani na kuna maswali ukiwa unataka kumjibu mtu lazima utumie akili na uelewa....
Yote kwa yote...
Kukujibu kiimani ni njia sahihi zaidi ingawa hujataka kujibiwa kiimani kwa maana Thread yenyewe umeiweka kwenye Jukwaa la Jamii ya Akili(Intelligence) na hili kupelekea wewe kuwa unataka kujibiwa kiakili zaidi.
Hivyo hadi kufikia hapa nitakua nimeelewa swali lako limeelemea wapi unless otherwise unirekebishe kwamba ulitaka kujibiwa kiimani...
Na kama ulitaka kujibiwa kiimani basi moja kwa moja kwa hao member waliokujibu hapo juu utakuwa teyari umeshapata jibu lako lakini kwa kuwa umeelemea kwenye
Intelligencer twende pamoja...
JE, QURAN ILISHUSHWA KUTOKA MBINGUNI?
Jibu ni
hapana ikiwa tu unauliza kitabu kama kitabu ambacho kimepigwa copy za kutosha basi ni kweli hakikushuka kutoka mbinguni,
Lakini ikiwa unauliza
Chanzo chake ni wapi basi hapana shaka ni Maneno ambayo yameshuka kutoka
mbinguni kupitia Roho takatifu ambaye ni Malaika wa Mwenyezi Mungu...............
Jinsi ilivyoshushwa na aliyepokea hilo ni swali lingine ikiwa utauliza lakini naamini hadi hapo utakuwa umepata jibu la kwanza.....
Swali lako la pili: Inamaana Mungu alitengeneza karatasi
Jibu ni
HAPANA...
Swali la tatu akatafuta peni na printer na kadhalika?
Jibu ni
HAPANA...
Swali la Mwisho Je tunaushahidi gani kama Qur-an ilishushwa na Mungu?
Jibu ni
KAMILISHA SWALI LAKO ILI NIJUE NAKUPA USHAHIDI GANI UNAOTAKA
Lakini kama unataka roughly Quran ni kitabu ambacho chenyewe kinajitaja kwamba
"Hiki ni kitabu kisichokuwa na Shaka ndani yake, Na Ni uwongofu Kwa Wacha Mungu..
Quran 2: 2
Sasa ndugu yangu Ikiwa wewe sio Mcha Mungu saa ngapi hiyo Quran utaamini ama kuthibitisha kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu?
Bado Quran 2: 272
Inasema:
Si juu yako wewe kuwaongoa, Lakini Mwenyezi Mungu humuongoa amtakaye.
Kama haitoshi
Quran: 2: 256
Inasema:
Hapana kulazimishana katika dini.....
Sasa hao wanaokulazimisha uamini wanavyoamini wao nao hawapo sawa wanasahau kuna watu imeshasema:
Quran; 22:46
Kwani HAKIKA si macho yanayo pofuka, lakini zinazopofuka ni nyoyo ziliomo vifuani
Sasa mtu ambaye kapofuka moyo rejea kwa Firauni na Waliokufuru wengine walikuwa wakiletea uongofu walikuwa wakisema "hadha sihirul Mubiin' huu ni uchawi ulio Dhahiri.....
Bado wewe unataka Quran ishushwe kama mazingaombwe watu kama wewe watasema Aliens walipita na ndege wakadondosha karatasi hizi Basi hawataamini...
N.B
Nimejibu ulivyo uliza ikiwa unataka kujenga hoja jenga hoja kwa mazingatio ya jukwaa husika
Rakims