Tuseme sijui kitu ebu nionyeshe wapi isa alifariku mbona unanizungusha nipo humu online ila wapi unanizungusha😂😂😂..
Wewe unadhani katika Qur'an utapata aya inayosema, nabii fulani na fulani kafa!!, kwani Quran imekuwa ni kitabu cha matangazo ya vifo vya manabii?? Qur'an inapotaja vifo vya manabii huwa inataja kwa ujumla mfano katika (3:144) au inataja kwa namna ambayo inabidi mtu utumie akili kujua.
Sasa tuliza fikra zako na tutazame hizi aya mbili za Qur'an (tafsiri);
"Na Allah atakaposema; Ewe Isa bin Mariam! Je uliwaambia watu; Nishikeni mimi na mama yangu kuwa waungu wawili badala ya Allah??, (Isa) atasema; Wewe ndiwe mtakatifu hainipasi mimi kusema ambayo sina haki nayo, kama ningalisema bila shaka ungalijua; Unajua yaliyomo nafsini mwangu, lakini mimi siyajui yaliyomo nafsini mwako, hakika wewe ndiye ujuaye sana mambo ya ghaibu". [ Qur'an 5:116]
Aya inayofuatia ambayo ni muendelezo wa hiyo iliyotangulia inasema:-
"Sikuwaambia lolote ila yale uliyoniamuru ya kwamba; Mwabuduni Allah, Mola wangu na Mola wenu, na nilikuwa shahidi juu yao nilipokuwa kati yao, lakini
uliponifisha Wewe ukawa mchungaji juu yao, na wewe ni shahidi juu ya kila kitu". [Qur'an 5:117]
Hilo ni swali Allah atamuuliza nabii Isa (as) siku ya Qiyama kwamba; yeye aliwaambia watu wamuabudu yeye na mama yake??, naye atajibu siku hiyo ya Qiyama kwamba hakuwaambia lolote isipokuwa yale aliyoamrishwa na Allah kwamba Wamuabudu Allah, na hajui huko nyuma kama watu walimuabudu yeye kama Mungu kwakuwa alikuwa kafariki.
Swali ni hili: kama nabii Isa
leo yupo hai mbinguni na leo hii bado anaabudiwa kama Mungu sasa atawezaje siku ya Qiyama kumwambia Allah kwamba:-
Sikuwaambia lolote ila yale uliyoniamuru kwamba Muabuduni Allah Mola wangu na mola wenu----- uliponifisha wewe ukawa mchungaji wao---!!??
Hapo ina maana Isa (as) hivi sasa hajui kama anaabudiwa yeye na mama yake kama Miungu wawili kwakuwa kafa na ndio maana siku ya Qiyama atajibu hivyo.
Hiyo ni aya inayothibitisha kuwa hivi sasa Isa (as) kafa ndio maana hajui kama yeye anaabudiwa na siku ya Qiyama atajitetea mbele ya Allah akisema kwamba kipindi anaabudiwa alikuwa hajui kwakuwa Allah alikuwa kamfisha na Allah mwenyewe ndiye hivi sasa amebaki kuwa mchungaji wa hao wanaomuabudu Isa (as), Isa leo hajui chochote kwakuwa kafa zamani mno (Qur'an 3:144).
Nimeandika kwa kirefu na kwa msisitizo ili kukufafanulia hii point muhimu ya kifo cha nabii Isa (as).
Qur'an ni kitabu cha watu wanaotumia akili.