Qur'an haikushuka jinsi unavyodhani.
Qur'an ni ufunuo alioshushiwa Mtukufu mtume Muhammad (saw) na Allah kupitia Malaika Jibril (as), yaani Wakati ufunuo wa Qur'an ulipokuwa unaanza malaika Jibril alimfahamisha Mtume (saw) kupitia Wahy ili awaandae Waandishi kwa ajili ya kuandika kile ambacho wakati huo atakuwa anafunuliwa,
Ukiangalia Qur'an mwanzoni mwa Sura zake inanza na; بسم الله الرحمن الرحيم, yaani kwa jina la Allah Mwingi wa rehema na ukarimu, hapo wale waandishi huanza kuandika wakijua Kwamba hapo ndio mwanzo wa ufunuo na waliendelea kuandika hadi mwisho wa sura, baada ya ufunuo kumalizika hapo ndipo mtume (saw) aliwaambia wale waandishi waanze kumsomea ili ahakiki kwani Mtume (saw) baada ya kufunuliwa Qur'an ilinasa hapohapo kwahiyo kama katika kuandika kungekuwa na makosa basi hapo angeyasahihisha.
Qur'an yote iliandikwa kwa kipindi cha miaka 23, miaka 13 Mtume (saw)akiwa Makkah na miaka 10 akiwa Madina.
Hadi mtume (saw) anafariki Qur'an ilikuwa imeandikwa kwenye vipande vya ngozi na magome ya miti maalumu ya kuandikia (scrolls) nk na ni kipindi cha Khalifa Seydna Umar (ra) ndipo alipofanya juhudi ya kuikusanya na kiuweka katika jalada moja (compiled in one volume from the scrolls) na hizi Qur'an za leo zilizoandikwa kwenye karatasi za kisasa zimetokana na hiyo Qur'an iliyokuwa compiled na khalifa Hadhrat Umar (ra), hiyo ni historia fupi ya jinsi Qur'an ilivyoshuka/ilivyoshushwa.
Inaonekana kilichokuchanganya ni neno "kushuka/kushushwa" ukadhani kwamba inaposemwa kitu fulani kimeshuka hususan kutoka mbinguni basi huenda kitu hicho kimetoka mbinguni kidhahiri.
Neno "shuka" limetumika sana katika Qur'an kwa maana ya kuja, kutokea, kupatikana nk kwa kitu chenye manufaa makubwa kwa binadamu, neno mbinguni nalo maana yake ni ulimwengu wa kiroho, ulimwengu wa heshima nk hivyo inaposemwa Qur'an imeshushwa kutoka mbinguni maana yake ni hiyo tu Kwamba Qur'an imeshushwa au imekuja kutoka kwa Mungu na sio vinginevyo.
Mfano; katika Qur'an Mungu anasema; "--- na ametushushia wanyama wanane" (39:6 Qur'an), je hapo unaweza sema Wanyama hao 8 wemeshushwa kutoka juu (mbinguni)??
Pia Allah anasema; قد انزل الله اليكم زكرا , yaani; bila shaka Allah amewashushia ukumbusho (Qur'an ), (65:10)
Isitoshe Allah anasema; و انزلنا الحديد yaani; tukakishusha chuma (57:25), hapo Allah amesema "tukakishusha chuma" haina maana kwamba Chuma amekishusha kutoka juu/mbinguni bali maana yake ni kwamba Chuma kinayo faida kubwa kwa binadamu ndio maana Allah kasema kakishusha na hivyo ndivyo inaposemwa Qur'an imeshushwa maana yake ni hiyo hiyo kwamba Qur'an inayo faida kubwa sana kwa binadamu.