Msaada nina milioni 500 hapa ambayo nataka niiwekeze niwe nakula faida tu, wapi kunafaa kwa uwekezaji huu?

Msaada nina milioni 500 hapa ambayo nataka niiwekeze niwe nakula faida tu, wapi kunafaa kwa uwekezaji huu?

Wazee kwema

Katika hustle zangu nilibahatika kupata milioni 500 ambayo kwa sasa naona km nikisema nianze kuitumia au kufanya biashara naweza iharibu yote (si mnajua hela za zali la mentali? 😅)

Kuna mtu amenishauri nikaiwekeze sehemu mi niwe nakula faida tu maisha yangu yote. Je, ni wapi ambapo naweza kuwekeza na mchanganuo wake upoje?

Nawasilisha
Fanya biashara ya ng"ombe....from chaka to shamba....from shamba to Butcher,,,,,Halafu ngozi una export..mbolea unauza...au kutumia bustanini,,,,,
 
Kabla ya kuamua wapi kwa kuwekeza inabidi upige hesabu zinazoendana na malengo yako.

Naona wengi wametoa ushauri unaolenga kukuongezea utajiri, lakini swali lako halijalenga kuongeza utajiri. Umelenga kupata passive income for the rest of your life.

Hesabu itakayokufaa inaendana na bajeti ya matumizi yako. Ili pesa ibaki for the rest of your life, unatakiwa kutumia si zaidi ya nusu ya faida inayoingiza. Kwa mfano, kama faida kwa mwezi ni mil 5, basi wewe utumie mil 2.5 tu. Ukifanya hivyo, thamani ya pesa yako haitaathiriwa na inflation.

Mifuko yenye faida ya 12% pamoja na compound interest inakufaa zaidi katika malengo yako. Ipo mingi siku hizi. Kwa sababu una kiwango kikubwa cha pesa, ni salama zaidi kuwekeza kwenye mifuko isiyopungua mitatu ili hata mmoja ukiyumba mingine inakubeba. Kwahiyo unaweza kuweka Faida Fund, UTT liquid, UTT wekeza maisha, UTT Bong fund, M-Wekeza.
 
Nitakushauri kwa faida yako....
Nenda kwa broker ntakupa broker mzuri tu chukua hiyo hela igawe mara 6 kama milioni 80 kanunue treasures bond ila hakikisha unanunua Kila mwezi
Kwa miezi sita pambana mwambie broker ahakikishe coupon yako haipungui 15%

Utapata asilimia 15 ya hiyo hela yaani milioni 80 asilimia 15yake kwa kuwa bond wanalipa mara mbili kwa mwaka wataigawanya utapata karibia milioni 6 Kila mwezi kwa mwaka mzima na hela yako ipo pale pale...

Mm napokea 3.7m Kila mwezi na biashara zangu zinaendelea vizuri tu..
Umewekeza kiasi gani mkuu
 
Kama bado ni Kijana na unatamani kufika mbali zaidi…….M300 Tia hisa za CRDB na NMB. 200m nunua Bonds za serikali za muda mrefu zenye interest ya angalao 14%. Kwanini? Hisa zitaendelea kupanda na kukupa gawio kila mwaka so ni rahisi kwa mtaji wako kuongezeka na Bonds zitakupa hela ya kuweza kujikimu huku ukilinda mtaji wako.
Ushauri wa kiturist
 
Magorofa yameshakuwa Mengi sana.Milion 500 ni hela Ndogo sana kwa Ghrofa linalolipa.Kujenga kama uwekezaji haujengi kwa Cash unajenga kwa Mkopo wa Benki Ndio kujenga kibiashara.Hekima inasema Kujenga ni kufungia hela chini so badala ya kufungia hela yako chini tafuta hela za watu wengine uzifungie chini ili ya kwako iendelee kuwa kwenye mzunguko.
Bank unatoa nini kama dhamana ndo wakupe mkopo?
 
Wazee kwema

Katika hustle zangu nilibahatika kupata milioni 500 ambayo kwa sasa naona km nikisema nianze kuitumia au kufanya biashara naweza iharibu yote (si mnajua hela za zali la mentali? 😅)

Kuna mtu amenishauri nikaiwekeze sehemu mi niwe nakula faida tu maisha yangu yote. Je, ni wapi ambapo naweza kuwekeza na mchanganuo wake upoje?

Nawasilisha
Kunywa bia wewe acha kuumiza kichwa, unaweza kukata moto next week wakalewea watu wengine hizo hela 'za zali la mentali' kama ulivyoziita.
 
Kijana fanya kazi acha kuota ndoto za mchana. Umesema zali la mentali baadae kwenye comment ukasema umepata machimboni..!! Are you an idiot or physcho?
Inawezekana katika hustle ukakutana na zali la mentali, kwani Pro J kwenye wimbo wake yule manzi walikutana ndotoni.
 
Una 500M unakuja kuomba ushauri JF namna ya kuwekeza? Sasa ulikua unazitafuta za nini kama hata hujui cha kuzifanyia? Maana najua from the first step unatafuta hela ni kwa ajili ya kutatua changamoto flan ama kuizalisha kupitia uwekezaji. Au ni pesa ya ndoto yako unakusanya mawazo ya biashara na uwekezaji siku ukizipata ujue pa kuwekeza?
 
Boss kama hutaki mambo mengi, nunua bond ya 25 years, rate sasa 13.5%, una uhakika na almost million 6 kila mwezi kwa miaka 25 ijayo , na mwishoni wanakurudishia milioni 500 yote ( of course 500m ya wakati huo thamani yake labda million 100-200), uzuri unaweza ukatumia bond yako kama collateral kupata mkopo au kuiuza tena
 
Wazee kwema

Katika hustle zangu nilibahatika kupata milioni 500 ambayo kwa sasa naona km nikisema nianze kuitumia au kufanya biashara naweza iharibu yote (si mnajua hela za zali la mentali? 😅)

Kuna mtu amenishauri nikaiwekeze sehemu mi niwe nakula faida tu maisha yangu yote. Je, ni wapi ambapo naweza kuwekeza na mchanganuo wake upoje?

Nawasilisha

MI NINA BILLION 5 SIJUI NIWEKEZE WAPI
 
Ulifanya jambo zuri, biashara nyingi za bongo kupata faida ya 15% ni ngumu sana
Ni kweli mkuu mm kama jamaa sikua na wazo Hilo kabisa na hela ilikuja ghafla sana so niliomba mahali usharudi nikaongozwa ila hela ni shetani ukicheza kidogo tu inatoweka

Kupata hela sio kazi...kazi ni kulinda hela!
 
Nitakushauri kwa faida yako....
Nenda kwa broker ntakupa broker mzuri tu chukua hiyo hela igawe mara 6 kama milioni 80 kanunue treasures bond ila hakikisha unanunua Kila mwezi
Kwa miezi sita pambana mwambie broker ahakikishe coupon yako haipungui 15%

Utapata asilimia 15 ya hiyo hela yaani milioni 80 asilimia 15yake kwa kuwa bond wanalipa mara mbili kwa mwaka wataigawanya utapata karibia milioni 6 Kila mwezi kwa mwaka mzima na hela yako ipo pale pale...

Mm napokea 3.7m Kila mwezi na biashara zangu zinaendelea vizuri tu..
Je akitaka kuchukua pesa yake aliyowekeza huwa wanatoa na faida?
 
Back
Top Bottom