Hawa watu bodaboda huwa hawaendi kwenye misafara hii bila kuwalipa...
Huyu Mwigulu anatoa wapi pesa za kuwalipa hawa iwapo yupo kwenye safari za kawaida tu za kikazi za serikali huku tukijua hulipwa posho ya safari kama mtumishi wa umma..??
Ndo kusema pesa ya posho yake ya safari analipa bodaboda wa kumwimbia barabarani badala ya kuachia familia yake ili wanunue chakula na maji...?
Hawa viongozi wetu mbona hawana haya wala aibu kiasi hiki..? Anawezaje kuwatumilia vumbi wananchi masikini hawa anaowatoza tozo huku yeye akiwa kwenye V8 New Model la TZs 600,000,000 peke yake...? Ina make sense kweli hii...?
Yaani katikati ya hali ngumu kifedha kwa wananchi na kufunga mikanda (maana wanatuambia hivyo) lakini cha ajabu wao wanatumia mali ya umma hovyo hovyo kiasi hiki halafu wanataka tukubaliane na mambo yao ya kijinga...?
Mbona wanatufanya wananchi majuha na wajinga hivi...?
Nani atabisha kuwa hawa sio wezi wa mchana kweupe wa fedha zetu za tozo na kodi...???
Matendo yao yanathibitisha madai haya bila shaka yoyote...