Msafara wa Mwigulu Nchemba. Je, Kipindi Cha Magufuli ungeyafanya Haya?

Msafara wa Mwigulu Nchemba. Je, Kipindi Cha Magufuli ungeyafanya Haya?

Hajasahau yaliyomkuta alipokuwa waziri wa mambo ya ndani enzi za JPM. Alipigwa chini akiwa Kigoma akakosa usafiri wa kurudi Dar.
 
Ndio maana wanakomalia tozo ili waje mtaani kufanya ujinga kama huu. Waziri ana convoy kushinda hadi makamu wa raisi au waziri mkuu. Lakini ni kwamba kiburi cha huyu bwana kishafikia kilele na soona anawekwa mbali na fedha za umma.
 
Anamchukulia mama Poa.....Hili kundi litampa mama tabu sana. Tena wanamuimbia, tuna imani na Mwigulu?

Namuona na chapombe kando yake

Unajuaje kama hawamuwakilishi? Isitoshe unamuita mama mtu anayekudharau hivyo ?
 
Watanzania bado sana......pamoja na tozo zote hizi bado kuna watu wanaenda kumshangilia Mwigulu😳

Mwigulu ongeza tozo.
Ikibidi weka tozo ya pumzi kabisa!
 
Hawa watu bodaboda huwa hawaendi kwenye misafara hii bila kuwalipa...

Huyu Mwigulu anatoa wapi pesa za kuwalipa hawa iwapo yupo kwenye safari za kawaida tu za kikazi za serikali huku tukijua hulipwa posho ya safari kama mtumishi wa umma..??

Ndo kusema pesa ya posho yake ya safari analipa bodaboda wa kumwimbia barabarani badala ya kuachia familia yake ili wanunue chakula na maji...?

Hawa viongozi wetu mbona hawana haya wala aibu kiasi hiki..? Anawezaje kuwatumilia vumbi wananchi masikini hawa anaowatoza tozo huku yeye akiwa kwenye V8 New Model la TZs 600,000,000 peke yake...? Ina make sense kweli hii...?

Yaani katikati ya hali ngumu kifedha kwa wananchi na kufunga mikanda (maana wanatuambia hivyo) lakini cha ajabu wao wanatumia mali ya umma hovyo hovyo kiasi hiki halafu wanataka tukubaliane na mambo yao ya kijinga...?

Mbona wanatufanya wananchi majuha na wajinga hivi...?

Nani atabisha kuwa hawa sio wezi wa mchana kweupe wa fedha zetu za tozo na kodi...???

Matendo yao yanathibitisha madai haya bila shaka yoyote...
 
Kenya Kwanza wametoa fundisho zuri kwa wana EAC kwamba yale ambayo waliaminishwa hayawezekani kumbe yanawezekana kama mtu akiamua.
 
Mwigulu ni rais ajaye!!! Huo ni uamuzi wa mbingu na hakuna mwenye kuweza kugeuza
 
Back
Top Bottom