Msaidizi wangu wa ndani anagawa vitu vyangu kwa wanandoa

Balaa sana
 
BINTI NI MKARIMU SANA, HANA NIA MBAYA, ILA MWELEWESHE TARATIBU, LAKINI DEAL PARPENDICULARY NA HUYO PARASITE/PANYA ANAYE MSHAWISHI H/GIRL WAKO
 
Yani unamuogopaje mtu unayemlipa, kula na kulala kwako, ni aidha utoe maelekezo aache na unamwambia akizingua basi aende, wala hujalogwa, umejiloga
 
Mimi ni muoga sana .huwa inanicost
Pole sana upo kama mimi, nimerithi kwa mzee wangu yaani alikuwa anapelekwa pelekwa na mama yangu wa kambo hadi kero, sasa na mimi ndiyo hivyo najikutaga nashindwa kumwambia mtu ukweli nakuwaga na hofu sana hata ugomvi huwa sipendagi.
 
Pole sana jifanye kama unamuuliza mbona vitu vinapungua haraka, jitahidi kumwambia kiupole mwambie maisha yalivyo magumu vitu vilivyopanda bei, mueleweshe tu aache kugawa vitu bajeti inaharibika.
 
mshirikishe kuwa miezi ya hivi karibuni, unanunua chakula mara kwa mara maana hakifiki mwisho wa mwezi, mimi wangu kupenda tv Jamani,chakula ataunguza, basi kama anajaza maji yatajaa yatamwagika hana hata habari, mwezi wa kwanza tu kuanza kazi bili ilikuja 70000, nilimshirikisha ile bill ni kubwa sana, kwa upole tu akaniuliza kwani ulikuwa unalipa ngapi nikamuonesha ya mwezi uliokuwa umepita ilikuwa 21000, akasema sikujua kama maji yana gharama sana, basi baada ya hapo akawa mwangalifu.
 
Kweli dunia ipo ukingoni boss anamuogopa mfanyakaz...sem nimegundua kuwa unawaza akiondoka utapata tbu kumpata mwingne angali upo busy na kazi
 
we usimdanganye wafanyakazi wazuri ngumu sana kuwapata, atafute namna tu hata kama ni kufungia vitu chumbani, au kupika chakula kingi usiku then kinabaki kidogo cha mchana tu. vingine vyote stoo na ufunguo wa stoo unakaa nao
Huyo hawezi kuwa mzuri kwa tabia hii ya kugawa ovyo vitu vya Boss wake!
 
we usimdanganye wafanyakazi wazuri ngumu sana kuwapata, atafute namna tu hata kama ni kufungia vitu chumbani, au kupika chakula kingi usiku then kinabaki kidogo cha mchana tu. vingine vyote stoo na ufunguo wa stoo unakaa nao
Ahaaaa daaah
 
Duuh aseeeee
 
Hapao kwenye kuacha TV on ndiyo tabia yangu nachaga TV on masaa 24 Nikiwa Nyumbani na hakuna shida TV inawaka tu bila shida. Kwahiyo TV kuwa on hakuna shida ila inategemea na aina ya TV kama hizi TV za Mchina kuungua ni rahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…