Imebidi ni ku - quote tu japo maelezo yako ni mengi sana!
Nani kakataa kuwa Tundu Lisu sio mwanasheria!? Fine, mwanasheria ana haki ya kumtetea yeyote ndio, ni lini hao wa Canada wameomba uwakili wake!? Kwa kesi ipi!? Na wakili anatafutwa na mteja au anatafuta mteja!
Sent using
Jamii Forums mobile app
Kama unaona hayo maelezo yangu ni mengi sana unaweza kusoma kitabu cha kurasa 1200?
Habari za wakili na mteja wake na mahusiano yao ni siri yao, inatetewa na faragha ya wakili na mteja, huelewi hilo?
Ukisema mwanasheria ana haki ya kumtetea yeyote, ukielewa kwamba "yeyote" inajumuisha hata mtu ambaye hajaomba utetezi (mwanasheria anaweza kutetea upande wa mtu katika mahojiano ya TV kwa sababu anaona upande huo ni wa haki, bila hata ya kuwa mwanasheria rasmi wa upande huo) halafu ukauliza ni lini hao wa Canada wameomba uwakili wake, kwa kesi ipi, na wakili anatafuta na mteja au anatafutwa na mteja unajionyesha hujui unataka kusema nini na unauliza maswali ambayo ushayafuta umuhimu wake pale ulipoandika "fine, mwanasheria ana haki ya kumtetea yeyote".
Ukishasema "mwanasheria ana haki ya kumtetea yeyote" hutakiwi kuanza kuuliza maswali kuhusu anayemtetea tena, kwamba lini wa Canada wameomba uwakili, kwa kesi ipi, nani anamtafuta mwenzake. Kuuliza maswali hayo ni kuji contradict.
Ni kama mtu anasema "unaruhusiwa kwenda mkoa wowote Tanzania" halafu anaanza kukuuliza maswali mengine mengi kama "ni lini umeenda Tabora, kwa usafiri gani, nani kaanzisha hiyo safari?".
Hayo maswali kabla ya kujibiwa ni lazima yawe justified kwamba yapo warranted na si unreasonable, ukishasema ni ruhusa kwa mtu kwenda mkoa wowote Tanzania, hayo maswali yana relevance gani? Kwa nini yajibiwe? Yana umuhimu gani wakati ushasema ni ruhusa kusafiri kwenda mkoa wowote Tanzania?
Unajichanganya kwa kukubali kitu, halafu kuhoji kitu kile kile ulichokikubali.