Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu


Hiyo asilimia ni kwa kima cha chini tu! Kama hamuelewi su hamkuelewa basi sasa mmeelewa, lakini lile jambo letu limetimizwa!
 
Sisi wazoefu tulijua tu mtaja Lia siku ya payday, always maneno yanakuwa mengi utendaji kidogo. Mimi nilishawaho ongezewa mshahara shs alfu 5. Mnapewa percentage mnapiga hesabu kuubwaa mwisho wa siku tukapewa formula ya kukokotoa ongezeko inafika mpaka kibaha. Duh msitegemee mshahara kutoboa tafuta issue nje ya mshahara utatoboa
 
Alafu mpaka unamaliza kutoa hako ka salary iliyoongezeka ishakatwa yote kwenye tozo
Hawa jamaa wa MoF&P wanafahamu hesabu hadi wanaumwa,unakumbuka PM aliwahi kuunda TaskForce kuwachunguza?Wazuri wa hesabu za kutoa kidogo&kujumlisha zaidi.
Hadi hapo akili zitakapoturejea,tutakuwa tumenyooka!
 
wanawarusha roho tu. tulioko jikoni tunajua. haujatoka.
Watu mnapenda kujiupgrade, eti mlioko jikoni[emoji23][emoji23][emoji23].

Wewe endelea tu kuuza genge la nyanya hapo mtaani au ukomae na vile vibarua ambavyo mshahara kuingia ni mpaka tarehe za mwisho kabisa (30-31), walioko jikoni na wenye kazi za kueleweka wamelipwa tayari.
 
Shukuruni basi hata hiki kidogo mlichopewa.
Kwa miaka sita hamkupata hata sumni zaidi ya kupunguziwa kodi.

Fanyeni kazi sasa.
Hapa Kazi Tu na iendelee sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…