Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Dah.. Bora niendelee kupiga forex tu!

Nikitengeneza $10 kila siku kwa mwezi nina kama kilo 6!

Watumishi poleni..


Bora Magu hakuongeza kabisa mshahara ila vitu havikuwa bei juu namna hii!

Sasa hiyo 20 inamsaidia nini mtu ambae garama za maisha zimepanda kwa kasi namna hii?
Ila bei ya vitu ni dunia nzima
 
 
Pole mkuu piga moyo konde maisha lazima yaendelee hata kama unapitia situation ngumu kiasi gani
 
ulitakiwa usubirie kwanza mshahara wa mwezi huu ndipo ukope unaiaminije ccm na serikali yake kirahisi hivo
 
Anyway wana siasa sio wa kuwategemea

Wakuu tujiongeze sna nje na hizi kazi nina mawazo tofauti sna.

Mwakani nitareta mrejesho wa kuwa na other side income

Nitapambana hadi nipate huu mshahara ninaolipwa Kwa mwezi.

Usiku mwema

Ndo umejuw Jana?
 
Mkeka huu hapa
IMG-20220723-WA0000.jpg
 
Kamwe aliyeshiba hamjui mwenye njaa. Pamoja na sifa na tambo zote walizofanya serikali kuhusu kuongeza mishahara wameishia kuongeza elfu 20,000?

Ikiwa ni muda mchache toka bank ya NMB kunipa notification ya mshahara kuingia na kufanikiwa kuona kilichoongezeka. Nimepigwa butwaa kuona tambo zote zile increment haizidi 20K!

Nadhani Sasa ni muda wa watumishi wa umma kujitambua na kuacha kushoboka na serikali. Serikali ime-inflate gharama za maisha kwa kiwango kikubwa but then haina efforts za kuboresha maslahi.

Maamuzi ya namna hii yanapunguza morali ya kazi na kushusha uadilifu. Tutegemee uzembe makazini na kuongezeka ubadhirifu.

Serikali imeshindwa kusimamia utumishi wa umma hususani kwenye suala la maslahi.
Wafanyakazi mnaogopa hata kugoma au kuandamana hata siku moja mnategemea nini?
 
Back
Top Bottom