Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

Mshahara umetoka, nyongeza ipo lakini lazima ucheke tu

55000 x 7= 385000
..Marehemu kachelesha sana watumishi.

Hongereni kwa kilichopatikana.
Kweli usolijua ni kama usiku wa giza, hiyo miradi ya JPM ingekamilika akiwepo ndo mngemjua vizuri msukuma vile anapenda sifa, wafanyakazi wasingetamani aondoke madarakani, tulikuwa tumeshazoea sisi wenye akili, huwezi pingana na mabepari wakakupenda hivyo hata angesema akope pesa alipe mishahara kama mama anavyofanya wangempa masharti ambayo mtu wa mlengo wake wa kisiasa asingeafiki, R.I.P JPM.
 
Kamwe alieshiba hamjui mwenye njaa. Pamoja na sifa na tambo zote walizofanya serikali kuhusu kuongeza mishahara wameishia kuongeza elfu 20,000?

Ikiwa ni muda mchache toka bank ya NMB kunipa notification ya mshahara kuingia na kufanikiwa kuona kilichoongezeka. Nimepigwa butwaa kuona tambo zote zile increment haizidi 20K!

Nazani Sasa ni muda wa watumishi wa umma kujitambua na kuacha kushoboka na serikali. Serikali ime-inflate gharama za maisha kwa kiwango kikubwa but then haina efforts za kuboresha maslahi.

Maamuzi ya namna hii yanapunguza morali ya kazi na kushusha uadilifu. Tutegemee uzembe makazini na kuongezeka ubadhirifu.

Serikali imeshindwa kusimamia utumishi wa umma hususani kwenye suala la maslahi.
Na hyo 20000 kuitoa benk ni balaa la tozo
 
Back
Top Bottom