Tokea tetesi za kuugua hadi kufariki kwa Mzee wetu Magufuli, baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wamekua wakitoa matamko mengi sana, wengine wakaanza kuandika katika mitandao hisia zao juu ya msiba huo lkn wengi sana walikua wakidhihirisha chuki zao za waziwazi juu ya Mh. Magufuli.
Maandiko yao na maneno yao kwa vyombo vya habari imesaidia sana kutupa picha halisi ya watu hawa kiasi kwamba sasa hata kesho wakija kuomba ridhaa kwetu tunawafahamu.
Kupitia maandishi yao imenipa sababu ya kufaham kwanini wale wachache miongoni mwao wenye akili wanapambana kufa na kupona Mbowe aweze kuendelea kuongoza chama chao, na hii ni kwasababu Mbowe ni mtu Smart sana, kwanza sio wakuongea tu bila kujipanga, ni mtu anaweza zuia hisia, ni mtu ambae ana ile kitu naweza kusema "Leadership Ethics).
Sasa kwa sifa za hao wengine ukimlinganisha na huyu mwamba iko sababu kubwa ya yeye kuendelea kuongoza hicho chama kwakua wenye akili walishaona hao wengine ni wanaharakati wanaojificha ktk mwamvuli wa chama.
Katika hali ya kawaida kwa mwanasiasa kijana na aliekomaa hata afe adui yako alieua familia yako yote unatakiwa kuwa smart sana kuchagua maneno yapi ya kutumia (uchaguzi wa lugha), vinginevyo unaweza kuanika tabia yako halisia na ujinga wako wote na watu walafaham madhaifu yako kitu ambacho kisiasa ni kitu mbaya.
Mbowe namkubali sana, una tabia za kiuongozi. Big up Big brother Mbowe!