..angekuwa hajahusika angekanusha tuhuma za mara kwa mara toka kwa TL kwamba yeye JPM ndiye aliyeamuru auwawe.
Mtu ukiwa rais wa nchi, una deal na vitu solid only, hizo tuhuma za TL kuwa mhusika ni JPM aliziwasilisha wapi?, au ulitaka rais wetu pia anze kujibu kila tuhuma za mitandaoni!.
TL alipoitisha ile press conference na kutangaza anafuatiliwa, alipaswa afanye nini ili issue ile ishughulikiwe?, alipaswa kuripoti kunakohusika na pale angeulizwa unamhisi nani, angesema!.
Na baada ya tukio yeye hakuhojiwa, but as a lawyer and a good law abiding citizen, baada ya kurejea nchini, alipaswa yeye mwenyewe kujipeleka polisi na kuroa statement yake na hapo angeeleza anamhisi nani, na kuutoa ule ushahidi, hapo ndipo angejibiwa.
pia angeitisha uchunguzi ili waliohusika wakamatwe na yeye asafishwe kutokana na tuhuma hizo.
Sio kazi ya rais wa nchi kuitisha uchunguzi wa tukio la kihalifu hiyo ni mandate ya jeshi letu makini la polisi. Uchunguzi ulishindikana kutokana na kukosekana kwa mashahidi wawili pekee wa tukio hilo, maana tunahisi hata silaha walizotumia ni silencer, hakuna mtu mwingine yoyote aliyeona chochote wala kusikia lolote zaidi ya wawili hao. Mpaka sasa wanasubiriwa!.
kwangu mimi huo ni ushahidi mzito wa kimazingira kuwa JPM alihusika.
Kwenye criminal liability kunahitajika kitu kinachoitwa solid evidence na sio circumstantial evidence. The burden of proof lies with the prosecution, kwa vile hakuna any investigation going on kuhusu tukio hili, jinai haina time frame, TL na dereva wake waje waandike maelezo uchunguzi uanze.
Kiukweli uchunguzi wa tukio hili ulikuwa ni simple tuu hata sisi waandishi wa IJ tungeweza kuufanya
Serious Media inaweza kuwabaini "wasiojulikana" Deo Masakilija
P