Afrika tu ambapo haitoi nafasi Kwa viongozi wake kusema hadharani kuachia ngazi, (kujihudhuru nafasi zao)
Sii kweli, viongozi wanao jiuzulu wenyewe, huandika barua na kutoa sababu au hutangaza kama EL. Viongozi wanaotumbuliwa ndio hukaa kimya, na ikitokea mtumbua majipu asiposema ni kwa nini amelitumbua jipu fulani, mtumbuliwa hutulia kimya anyolewe kimya kimya.
Ilikuwa vigumu sana endapo ungeling'ang'ania hiyo nafasi ya Uwazari wa Nishati,
Hii sii kweli!, kitu unachopata kwa kuazimwa tuu kwa hisani, huwezi kuking'ang'ania as if ni chako!. Mwenye chake anaweza kukichukua wakati wowote, yeye chake ni ubunge tuu na sio uwaziri!.
Nadhani ilikupa wakati mgumu saana, ila mwishowe uliamua Kwa hekima nyingi mno
Pia hii sii kweli hakuamua chochote bali aliamuliwa!.
Watanzania tunafahamu, wewe ni miongoni mwa mawaziri mliotumbuliwa pasina kufahamu sababu za kutolewa kwenye nafasi zenu
Kwani unaijua sababu ya yeye kuteuliwa?, aliambiwa sababu?. Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga!, anaeteuliwa bila kuambiwa sababu, atatumbuliwa bila kuambiwa sababu!, juzi kati katumbuliwa MFA, Balozi Mulamula, ulizisikia sababu?. Hapa unataka kujenga hoja kuwa Kalemani kaonewa!, kwani uwaziri ni haki yake au mali yake?.
Ulifanya Kwa juhudi kubwa, kama kiatu, basi wizara hiyo ilikuenea vema! Ulienda Kwa kasi ya ajabu kiutendaji,
Hapa nakuunga mkono hata mimi ni shahidi kupitia one on one na Kalemani
Ilikuwa vigumu sana kuelewaka kwetu ikiwa ungelikubali kuendelea kuongoza wizara hiyo Kwa mabadiriko yaliyoletwa na uongozi huu
Hii sii kweli!, issue ya kuendelea kuongoza wizara sii yake, huyu hakujiuzu ni
Uliwaza mbali sana, na hatimaye ukamweleza mkuu wako kuwa, hautaeleweka, ni bora awekwe mwingine,
Hii sii kweli!, yaani Kalemani ampangie cha kufanya mkuu wake?!, ingekuwa ni hivi si angejiuzulu?. Mbona hakujiuzulu na badala yake ametumbuliwa?
na ndipo watanzania tukapata waziri wa hovyo kuwahi kutokea
Hii sii kweli kabisa!. Huyu aliyepo sasa ni jembe kazi!.
Hebu mshuhudie
Mungu akubariki sana Mh Kalemani
Naunga mkono hoja.
Hekima na busara zako, tunakuombea uendelee kuitumikia nchi yako Kwa juhudi hizo hizo bila kuchoka
Naunga mkono hoja.
Kawaida ya chama chako, huwa hakipendi watu wenye kujitambua
Unamaanisha chama chake kinapenda mazuzu?, kimejaa majitu yasiyojitambua?, kama hii ni kweli ilikuwaje akawa huko na hadi sasa bado yupo?. Kama lengo ni kumfagilia Kalemani we mfagilie tuu lakini usimfagilie huku unakipondea chama chake ambacho kwake CCM ni baba ni mama!.
Ukiwa chama fulani na hiko chama kinapenda mazuzu, then na wewe ni zuzu!.
Sii kweli kuwa CCM haipendi watu wanaojitambua, CCM haipendi watu wasiojitambua ambao wanaboronga hadi kutumbuliwa!. Wanaojitambua wakiona tuu upepo umebadili mwelekeo hawasubiri na wao wanabadilika ama kuendana na kasi ya upepo au kupisha kwa kuachia ngazi na sio kusumbiri hadi kusombwa na kimbunga!.
P