Unaelewaje neno "kubariki"...pia kanisa libariki ndoa za jinsia moja
Hata hivyo sitaki vita.
Ijumaa njema.đź‘‹
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaelewaje neno "kubariki"...pia kanisa libariki ndoa za jinsia moja
Soma tena ulichoandikaAlichosema Papa
Ni kuwa ...kanisa katoliki...duniani kote
Liwapatie baraka zote wanandoa wa jinsia moja na pia kanisa libariki ndoa za jinsia moja
Yaani kusiwepo na ndoa ya jinsia moja itakayo gomewa kufungwa
Na kanisa katoliki duniani kote!!!
Sasa!!! Kwa tamko hili...
Msitafsiri kuwa PAPA AMEHARALISHA ushoga!!!!!
Hizo tafsiri zenu..bakini nazo!
Ww umemwelewaje??
Papa ndio kanisa kama hujui "POPE IS SUPREME LEADER OF CATHOLIC CHURCH" wewe ndio utaondolewaNadhani kanisa lina mkono mrefu sana,huyo papa ataondolewa soon
nafikiri umeona opposition kubwa duniani umeona kuwa hata MAASKOFU wame mkataa papa , tazama hata baadhi ya MAASKOFU WA nchi ya Poland wamekataa kubariki wanaume walio oana (couples) ...Papa Francis amewaruhusu mapadre kuwabariki wapenzi wa jinsi moja, yakiwa ni maendeleo makubwa kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja na mahusiano mengine ya kijinsia wanaofahamika kama LGBT katika Kanisa Katoliki la Roma.
Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki la Roma amesema makasisi wanapaswa kuruhusiwa kuwabariki wapenzi wa jinsi moja na wanandoa "isiyo ya kawaida", kwa misingi ya hali fulani.
Lakini Vatikani ilisema baraka hazipaswi kuwa sehemu ya taratibu za kawaida za Kanisa au zinazohusiana na miungano ya kiraia au harusi.
Iliongeza kuwa inaendelea kuiona ndoa kuwa kati ya mwanamume na mwanamke.
Papa Francis aliidhinisha waraka uliotolewa na Vatican kutangaza mabadiliko hayo siku ya Jumatatu.
Vaticani ilisema inapaswa kuwa ishara kwamba "Mungu anawakaribisha wote", lakini hati hiyo inasema makuhani lazima waamue kwa msingi wa kesi baada ya kesi.
Akitambulisha andiko hilo, Kardinali VĂctor Manuel Fernández, ambaye ni msimamizi wa Kanisa, alisema kwamba tamko jipya limebakia kuwa "imara kwenye fundisho la kimapokeo la Kanisa kuhusu ndoa".
Lakini aliongeza kuwa kwa kuzingatia "maono ya kichungaji" ya Papa" ya "kupanua" ombi la Kanisa Katoliki, miongozo mipya inawaruhusu mapadre kubariki uhusiano ambao bado unachukuliwa kuwa wa dhambi.
Watu wanaopokea baraka "haifai kuhitajika kuwa na ukamilifu wa kimaadili wa awali", kulingana na tamko hilo.
Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na mhudumu, akimwomba Mungu ambariki mtu au watu wanaobarikiwa.
Kardinali Fernández alisisitiza kwamba msimamo huo mpya hauhalalishi hadhi ya wapenzi wa jinsia moja mbele ya Kanisa Katoliki.
NB: Hii ni taarifa ya BBC: Lakini kumbukeni BBC wanatetea dhehebu la Anglican ambalo suala la ushoga ama ndoa za jinsia moja ni kawaida kwa Waingereza. Papa alichosema ni kwamba watu wenye ndoa za jinsia moja ni wenye dhambi kama wengine, isipokuwa wakija kanisani kwa kutubu basi wabarikiwe kama binadamu wengine wenye dhambi wabarikiwe ili wajirudi.