Gereza Kuu la Machava mjini Maputo zaidi ya wafungwa na mahabusu wapatao 6,000 wamefungua mageti ya selo na kuwazidi nguvu askari magereza kisha kuchukua bunduki kadhaa aina ya AK47
Hali ni mbaya sana jijini Maputo na kuwa kuna dalili ya serikali ya FRELIMO kuyumba hata kupinduliwa, taarifa za vyombo vya usalama zimedokeza ..
Majimbo ya Nampula, Gaza, Sofala, Inhambane na Maputo nchini Mozambique hali ni mbaya sana vurugu, maandamano, uporaji umetapakaa wakaazi wakisema mambo ni mabaya sana
Maeneo mengine katika majimbo ya Niassa, sehemu za Cabo Delgado na Zambezia hali siyo mbaya sana ...
Viongozi wa upinzani watoa raia wananchi wasiharibu miundo msingi na miundo mbinu kwani wanatumai kuchukua nchi hivi karibuni na kuwa miundo hiyo ni muhimu kwa nchi kiuchumi, kijamii kuwepo.