Mtaani kuna Black-Mail system wanaume kuweni makini sana.

Kuna mfumo mzazi anamtuma mtoto wake aje kwako umnunulie pipi na ukishamnunulia anakuja kukuambia kuwa unamuwinda mtoto wake.

So kilichopo ndo hicho
Namuunga mkono mtoa mada mtaani kwetu juzi kuna mzee wa makamo,ana familia kabisa kaenda bar kanywa pombe zikamkolea,akaanza kucheza na mtoto wa mwenye bar huyo mtoto ana miaka 6,kumbe mwenye mtoto alikuwa anachukua video jana kaenda polisi kawaonesha video anasema mtoto wake alitaka kubakwa mzee wa watu kakamatwa ameambiwa alipe M1 ndipo aachiwe
 
Wamama na mabinti lao Moja,


Wakiona kijana ana muelekeo wa maisha ,teari ,
Wanatia Kambi,
 
Mim Police Zanzibar ujinga huu upo sana Tena wazee wanakuja kuhonga ela ili kijana ashikiliwe
Ndio maana ushoga unakwenda kuongezeka sana zanzibar ...kama tunawafanya watoto wa kike kuwa mtego kwa wakiume tutegemee watoto wa kiume kupoteza hisia kwa watoto wa kike kutokana na hizi vurumai na vitisho na gasia za kuhatarisha wanaume .
 
Suo wote bali wale wanaoendeshwa na njaa
 
kuna siku watoto wangu waliachwa na gari ya shule, pale barabarani walisimama na watoto wengine wanasoma pamoja, niliogopa kuwabeba zaidi ya kuchukua watoto wangu tu na kufika kule nikatoa taarifa mmeacha watoto wa watu kule. hata watoto wangu nimewakataza marufuku kupanda gari ya mtu hata kama ni ya baba wa wale mnasoma nao. kuna mengi mtaani.
 
Hii ndio wanaiita kukabia juu.kazi kweli kweli.zama za kina mama kua magolikipa zimeisha
 
Kuna mfumo mzazi anamtuma mtoto wake aje kwako umnunulie pipi na ukishamnunulia anakuja kukuambia kuwa unamuwinda mtoto wake.

So kilichopo ndo hicho
Pengine huu mchezo ni mzuri kwa sababu unafanya wanaume wabakaji wakose kisingizio cha kubaka watoto? Nasema hivi kwa sababu sisi waafrika tuna utamaduni ambao mimi naona siyo mzuri, wa kufanya mazoea na watoto wa jirani na kutumia huo mwanya kufanya ubakaji? Mimi sidhani kama ni vizuri mtu mzima kuanza kuzoeana sana na watoto wa mtaani au kuwanunulia zawadi bila idhini ya wazazi wao. Mambo mengine japo yanaweza kuwa ni utamaduni mzuri lakini kwenye maisha ya kisasa tuyaache.
 
Mtu mzima unalewa na kuanza kucheza na mtoto wa mika 6 ni sawa? Mambo mengine siyo ya kufanya kwenye zama zenye kila unyama. Akome hata alikuwa hana nia mbaya.
 
Pia usitembee na mwanamke ambaye unakaa nae mtaa mmoja hata awe mzuri Kama malaika
Kwahiyo unashauri nikimpenda mtu hapa nihame mtaa nikamuombe uhusiano kutokea angle nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…