Mtaani kuna Black-Mail system wanaume kuweni makini sana.

Mtaani kuna Black-Mail system wanaume kuweni makini sana.

Kuna mfumo mzazi anamtuma mtoto wake aje kwako umnunulie pipi na ukishamnunulia anakuja kukuambia kuwa unamuwinda mtoto wake.

So kilichopo ndo hicho
Namuunga mkono mtoa mada mtaani kwetu juzi kuna mzee wa makamo,ana familia kabisa kaenda bar kanywa pombe zikamkolea,akaanza kucheza na mtoto wa mwenye bar huyo mtoto ana miaka 6,kumbe mwenye mtoto alikuwa anachukua video jana kaenda polisi kawaonesha video anasema mtoto wake alitaka kubakwa mzee wa watu kakamatwa ameambiwa alipe M1 ndipo aachiwe
 
Hii kweli kabisa hii michezo ipo na hasa wakikuona mwanaume upo mwenyewe unavisent vya kubadilisha mboga, gheto lipo vizuri ukiwa na kausafiri hata pikipiki, uwe makini sana usizani labda unapendwa au wewe HB kumbe wenzako wanakuwimda na tena wengine wana washirikisha na wazazi.

Siku hizi mabinti na wazazi wao hawana aibu mbele ya fedha na ukijaribu useme upige jua ndio umenasa na huchomoki hapo na wengine hutumia hata ndumba.
Wamama na mabinti lao Moja,

Wakiona kijana ana muelekeo wa maisha ,teari ,
Wanatia Kambi,
 
Mim Police Zanzibar ujinga huu upo sana Tena wazee wanakuja kuhonga ela ili kijana ashikiliwe
Ndio maana ushoga unakwenda kuongezeka sana zanzibar ...kama tunawafanya watoto wa kike kuwa mtego kwa wakiume tutegemee watoto wa kiume kupoteza hisia kwa watoto wa kike kutokana na hizi vurumai na vitisho na gasia za kuhatarisha wanaume .
 
Suo wote bali wale wanaoendeshwa na njaa
 
Sasa kuna mfumo upo ambao sio rafiki Kwa wanaume .

Wanaweza kuja watoto wakike wanakufata fata wnakuomba pipi n.k hakikisha hauwapi na usiwajibu na wala hata umkute mtoto wa mtu anashida gani usitoe msaada wowote . hawa watoto wa hivi wanakuwa wametumwa na wazazi wao.

Ukitaka kutoa msaada Katoe vituo Vya watoto yatima.

Pia usitembee na mwanamke ambaye unakaa nae mtaa mmoja hata awe mzuri Kama malaika

Sasa Wanaume mnatafutwa kuharibiwa maisha kwa kila namna.

Na wewe usimpigie Mwanamke wala kumtafuta tofauti na issue za Kazi na kibiashara .

Jaribu kuwa smart and play smart.
kuna siku watoto wangu waliachwa na gari ya shule, pale barabarani walisimama na watoto wengine wanasoma pamoja, niliogopa kuwabeba zaidi ya kuchukua watoto wangu tu na kufika kule nikatoa taarifa mmeacha watoto wa watu kule. hata watoto wangu nimewakataza marufuku kupanda gari ya mtu hata kama ni ya baba wa wale mnasoma nao. kuna mengi mtaani.
 
Sasa kama huyu utaogopa.
IMG_0710.jpeg
 
Kuna mfumo mzazi anamtuma mtoto wake aje kwako umnunulie pipi na ukishamnunulia anakuja kukuambia kuwa unamuwinda mtoto wake.

So kilichopo ndo hicho
Pengine huu mchezo ni mzuri kwa sababu unafanya wanaume wabakaji wakose kisingizio cha kubaka watoto? Nasema hivi kwa sababu sisi waafrika tuna utamaduni ambao mimi naona siyo mzuri, wa kufanya mazoea na watoto wa jirani na kutumia huo mwanya kufanya ubakaji? Mimi sidhani kama ni vizuri mtu mzima kuanza kuzoeana sana na watoto wa mtaani au kuwanunulia zawadi bila idhini ya wazazi wao. Mambo mengine japo yanaweza kuwa ni utamaduni mzuri lakini kwenye maisha ya kisasa tuyaache.
 
Namuunga mkono mtoa mada mtaani kwetu juzi kuna mzee wa makamo,ana familia kabisa kaenda bar kanywa pombe zikamkolea,akaanza kucheza na mtoto wa mwenye bar huyo mtoto ana miaka 6,kumbe mwenye mtoto alikuwa anachukua video jana kaenda polisi kawaonesha video anasema mtoto wake alitaka kubakwa mzee wa watu kakamatwa ameambiwa alipe M1 ndipo aachiwe
Mtu mzima unalewa na kuanza kucheza na mtoto wa mika 6 ni sawa? Mambo mengine siyo ya kufanya kwenye zama zenye kila unyama. Akome hata alikuwa hana nia mbaya.
 
Pia usitembee na mwanamke ambaye unakaa nae mtaa mmoja hata awe mzuri Kama malaika
Kwahiyo unashauri nikimpenda mtu hapa nihame mtaa nikamuombe uhusiano kutokea angle nyingine
 
Back
Top Bottom