...shabaash! sasa Malila hebu nipatie mifano miwili mitatu ya hizo 'high risk business', ukiondoa biashara kichaa kama 'unga' nk...maana kuna watu watafikiria huku ilhali watu tuna heshima zetu.
Ni biashara gani ya muda mrefu ambayo naweza kuzitumbukiza hizi 10m/=, na huo muda mrefu unakadiria muda gani na returns zake kwa makisio?
...chief! sina pa kuzirudisha ndugu yangu, zishakuwa zangu hizi...ndio maana nataka nizizungushe zipate kuzaa.
...stanmokiwa, huu ushauri wako ni mzuri sana na nitaufanyia kazi, kwani umenionyesha naweza tumia 65% tu ya Mtaji! Je, Soko la maziwa si mbaya sana, au ndio kutegemeana na location?
...umeniacha feri mkuu, ngoja niachane nayo hiyo biashara ya 'kuchoma ndizi!'
...nilivyomuelewa mimi, amesema ni kiasi/wastani kama 1.5m/= kwa miezi mitatu kwa hao ng'ombe watano.
...Fidel80 hilo la biashara ya piki piki ni wazo zuri, hasa Kwakuwa vibajaj navyo vinazidi mijini,....ila nimevutiwa zaidi na hilo wazo la mgahawa... maana'ke watu watake wasitake watakula, hasa watu wa maofisini... siku za kazi (i.e Jumatatu-Ijumaa) mfano pale Dar City Centre ule mgahawa wa HEE-DEE! ...naliweka wazo lako kwenye daftari nije nilitafakur baadae, thanks!
...Farmer, maisha ndivyo yalivyo; kuna watu wanamipango ya biashara bila mitaji, na kuna wenye mitaji bila mipango ya biashara. Ndio maana nimetumbukiza karata hapa nipate mawazo ya wote.
...Mensarum shukran. Nadhani nanyi biashara yenu ni kutoa ushauri! Ni wazo mojawapo umenipatia, shukran... tutawasiliana.