Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

unaishi wapi?je uliwahi kuwa na ndoto ya kufanya biashara yoyote hapo awali?how busy are you at your work?una mtu unayefikiria kuwa anaweza kusimamia biashara unapokuwa kazini?nadhani wazo zuri la biashara ni lile ulilo nalo wewe ili watu wengine wakusaidie kuliboresha...
 
Kwa mfano ninunue boda boda 8 kwa bei ya jumla.. nifungue account say BOA bank. Kila nikipewa cash nadeposit huko.. Then cash inflow niwe nanunua boda boda moja kila mwezi. After six months si naweza kukopa na kununua boda boda nyiingi zaidi au!???
Dahh kaz kweli kweli!!!
Nahitaji kutulia
Futa kabisa wazo hilo.
Kwanza kwa pesa hiyo huwezi kununua bodaboda nane.
Halafu usiwekeze kwenye Biashara moja.
Ushauri wa bure:
10m,unaiona ni pesa kubwa,lakini kiukweli ni pesa ndogo sana.Ila inaweza kuzalisha pesa kubwa kama ukituliza kichwa chako.
Na hali ilivyo ni kwamba bado unapapara,nakushauri iweke Bank kama miezi mitatu kisha ndio uifanyie mradi wako unaotaka kufanya.La sivyo utajuta.

Kwanza nakushauri toa kama 700,000 umtolee sadaka Marehem ili upate Baraka zake,maana bila yeye usingezipata.
na tabia ya pesa za Urithi,yaani kama ulitoa hata elfu moja katika hizo ukaenda kunywea bia basi hata ufanye nini umaskini ni wa kwako hadi unaingingia kaburini.Maana wafu wanaona matendo yetu
 
Usije ukarogwa kabisa kabisa. Nilkpoteza 8.5 kwa huo mradi. Tafuta Suzuki Carry mpe mtu na uwe unaifuatilia kwa karibu sana akuletee 50,000 kwa siku. Kama una shamba anzisha ufugaji wa kuku au bata.
 
Hiyo 700,000 unamanisha akatoe sadaka kwa hakina mwingira!! Nafikiri Mtoa mada anataka kujua biashara gani afanye ilipe
 
Usije ukarogwa kabisa kabisa. Nilkpoteza 8.5 kwa huo mradi. Tafuta Suzuki Carry mpe mtu na uwe unaifuatilia kwa karibu sana akuletee 50,000 kwa siku. Kama una shamba anzisha ufugaji wa kuku au bata.

mkuu ungesema ulipoteza vp hiyo 8.5 ingekuwa msaada kwa wana jamii wengine!,sababu wapo wanaofanikiwa katika biashara fulani na wapo wanaoshindwa biashara hiyo hiyo!
 
the-true-wash, kwanza unaonekana kichwa hakijatulia, ninashauri utafute kampuni mbili zinazofanya vizuri au mwelekeo mzuri, nunua hisa za million tano kila kampuni, halafu tulia ujichunguze nini unapendelea, fanya utafiti wa soko na kila kitu then uza hisa uanzishe ila sasa ukikurupuka, utarudi na uzi mwingine "yamenikuta".

Hisa zinalipa unaweza hata double hiyo hela baada ya miaka kadhaa. Bank hata Investment Account hailipi.
 
Last edited by a moderator:
mkuu ungesema ulipoteza vp hiyo 8.5 ingekuwa msaada kwa wana jamii wengine!,sababu wapo wanaofanikiwa katika biashara fulani na wapo wanaoshindwa biashara hiyo hiyo!

Hawa vijana ni pasua kichwa. Hawatakaaa kamwe wakuletee pesa yote. Wana a lot of excuses. Nakumbuka kwenye boda boda tano nililetewa siku mbili tu jumla ya 250,000 kwa week baada ya hapo zote zilikua majanga. Baada ya mwezi moja ikaibwa, insurance wakagoma kunilipa. Miezi mitatu baadae boda moja tena ikapata ajali Tabata- Matumbi. Dogo akakimbia boda ikakaa polisi miezi sita. Wakati huo huo hawa wengine wanazingua balaaa mara alete pesa mara asilete mara hivi mara vile iliishia kuniletea stress tupu. Kwa ufupi hivyo ndivyo nilivyopoteza 8.5 investment. Nakushauri usifanye maana hata huo uzima wa pikipiki ni mdogo sana na mizigo na suluba wanazozifanyia hizo pikipiki hao vijana waweza kuua mtu. Usifike huko
 
Hapo nimekuelewa mkuu #Elli , japo kumbuka kuwa hakuna biashara inayokuwa na hasara ikakosa faida!,mfano mm nipo kwenye Dala dala na madereva wakianza story napiga chini napaki gari hadi wiki nzima then nawapa dereva wengine,kwahiyo hapo madereva wanakuwa wanajua kabisa tukianza stori kazi hatuna!,kwahiyo ukiwa unamuacha kila siku mtu anakuletea pesa nusu unategemea nn?!!
 
Ungekuwa na Banda la kuku! Ungejaribu kufuga kuku!! Kama huna Banda na msimamizi, nunua hisa kwa mwaka ujipange na utulie
 
Nami nataka kufuga sasa naomba unielekeze hapo kwenye kiwanja safi cha kufanyia mifugo hiyo ya ngombe mkuu nahitaji
ng`ombe kweli wanalipa ( maziwa sio nyama),lakini jamaa yuko nje ya nchi. Mziki wa kutunza ng`ombe ukiwa mbali,tena ng`ombe wa maziwa si mchezo. Angekuwa bongo ningemsaidia kumwonyesha kiwanja safi cha kufugia ng`ombe hao.
 
Hapo nimekuelewa mkuu #Elli , japo kumbuka kuwa hakuna biashara inayokuwa na hasara ikakosa faida!,mfano mm nipo kwenye Dala dala na madereva wakianza story napiga chini napaki gari hadi wiki nzima then nawapa dereva wengine,kwahiyo hapo madereva wanakuwa wanajua kabisa tukianza stori kazi hatuna!,kwahiyo ukiwa unamuacha kila siku mtu anakuletea pesa nusu unategemea nn?!!
Yes yes uko sahihi at least kwenye dala dala na ndio maana nikamwambia at least atafute Ki Suzuki Carry maana kwa 10M asingeweza kupata Daladala lakini nilipenda pia kumwambia anunue Daladala, niliamua kuhamia kwa daladala pia, kuna changamoto japo sio sana ukilinganisha na piki piki maana mradi wa piki piki kwa siku ni sh.7,000-8,000 kwa flat rate ya Tshs.50,000/= kwa week.

Kama ataweza aongeze milioni tano atapata daladala nzima kabisa ya kuanzia ambayo kwa siku at least atapata sh.100,000/= ila akumbuke hii laki moja sio faida na sio pesa ya kukalia Bar na kuuza JINA, ni kwajili ya matengenezo ya gari na wewe faida yako jiwekee isizidi 20,000/= kwa siku nzima
 
Usije ukarogwa kabisa kabisa. Nilkpoteza 8.5 kwa huo mradi. Tafuta Suzuki Carry mpe mtu na uwe unaifuatilia kwa karibu sana akuletee 50,000 kwa siku. Kama una shamba anzisha ufugaji wa kuku au bata.
Mkuu,usimpoteze mwenzio,hakuna Suzuki Carry inaleta hesabu ya 50,000 kwa siku.Ninauzoefu wa Biashara hiyo na ninaifanya.
 
Mkuu,usimpoteze mwenzio,hakuna Suzuki Carry inaleta hesabu ya 50,000 kwa siku.Ninauzoefu wa Biashara hiyo na ninaifanya.
Mpwa, sijampoteza Mpwa wangu ndio maana nime-take trouble kuandika nilichokiandika, tuna-share uzoefu na kuweza kumsaidia Mpwa wetu huyu, inategemea unapaki wapi.

Kwa Pale Mabibo Sokoni hii inawezekana japo sio lazima.. Kama una uzoefu tofauti na huo basi tumsaidie, mimi uzoefu wangu ndio huo daladala na Boda boda.
 
Mpwa, sijampoteza Mpwa wangu ndio maana nime-take trouble kuandika nilichokiandika, tuna-share uzoefu na kuweza kumsaidia Mpwa wetu huyu, inategemea unapaki wapi.

Kwa Pale Mabibo Sokoni hii inawezekana japo sio lazima....kama una uzoefu tofauti na huo basi tumsaidie, mimi uzoefu wangu ndio huo daladala na Boda boda

Asante Elli,
Mie namshauri kwamba pesa aweke kwanza,maana kama vile anawasiwasi sana.Na hii inaweza kumfanya akapoteza uelekeo.
Carry hesabu ya wiki ili gari yako iwe salama ni Tsh:120,000,hii hesabu ya sasa,na hesabu ya zamani ndio kama hiyo aliyotoa Elli mwanzo,maana kabla ya kuanza kuingia Carry nyingi mjini hesabu ilikuwa inakaribia ya Daladala.
Tatizo akiwekeza kwenye Carry akubali kwamba kaingiza mtaji woote kwenye Carry.

Ningemshauri kamba ahakikishe haingizi zaidi ya milioni Saba kwenye biashara yoyote atakayoifanya,la sivyo atalia.Lazima awe na backup ya kuweza kuokoa tatizo linapotoea hasa kwenye vyombo vya moto. Gawa mtaji mara mbili,na unaweza kuanza kununu bodaboda moja kwanza ili upate uzoefu wa biashara,maana inaonekana ndio ndoto zako,sasa hapo itakupa picha kwamba hali ipoje.

Sio madereva wote wa bodaboda wakorofi,tafuta driver mwenye familia anaejua maisha ni nini,tatizo wengi tunatafuta vijana kwa kuona kwamba hawana majukum kumbe ndio watumiaji wa pesa kuliko wenye familia.

Mie niliwahi kufanya biashara ya bodaboda pia,nilikuwa nazo tano,na nimebakia na mbili kwa kuwa nilihamisha biashara kwenye Carry,lakini wakati nilipokuwa nazo hizo tano,ni Driver mmoja tu ndio alikuwa mkorofi,yaani pesa kulipa tatizo,kila siku pikipiki naikuta Buguruni Polisi,ukienda kuuliza unakuta keso za kuwapa mimba watoto wa watu.

Yaani alikuwa bwana mdogo basi madem walimkoma,yaani was under 20,ila mapaka siku naenda kwa mjumbe kuchukua Pikipiki mjumbe ananiambia kwa anavyojua yeye ni kwamba bwana mdogo kapiga watoto wanne mimba ndani ya mwaka mmoja tu wa kumpa Pikipiki.Maana alikuwa Day worker. Pesa wanapata ila wengie Wahuni sana,wahongaji sana na walevi.
Elli nitakuja unipe uzoefu wa Daladala
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom