Mpwa, sijampoteza Mpwa wangu ndio maana nime-take trouble kuandika nilichokiandika, tuna-share uzoefu na kuweza kumsaidia Mpwa wetu huyu, inategemea unapaki wapi.
Kwa Pale Mabibo Sokoni hii inawezekana japo sio lazima....kama una uzoefu tofauti na huo basi tumsaidie, mimi uzoefu wangu ndio huo daladala na Boda boda
Asante
Elli,
Mie namshauri kwamba pesa aweke kwanza,maana kama vile anawasiwasi sana.Na hii inaweza kumfanya akapoteza uelekeo.
Carry hesabu ya wiki ili gari yako iwe salama ni Tsh:120,000,hii hesabu ya sasa,na hesabu ya zamani ndio kama hiyo aliyotoa Elli mwanzo,maana kabla ya kuanza kuingia Carry nyingi mjini hesabu ilikuwa inakaribia ya Daladala.
Tatizo akiwekeza kwenye Carry akubali kwamba kaingiza mtaji woote kwenye Carry.
Ningemshauri kamba ahakikishe haingizi zaidi ya milioni Saba kwenye biashara yoyote atakayoifanya,la sivyo atalia.Lazima awe na backup ya kuweza kuokoa tatizo linapotoea hasa kwenye vyombo vya moto. Gawa mtaji mara mbili,na unaweza kuanza kununu bodaboda moja kwanza ili upate uzoefu wa biashara,maana inaonekana ndio ndoto zako,sasa hapo itakupa picha kwamba hali ipoje.
Sio madereva wote wa bodaboda wakorofi,tafuta driver mwenye familia anaejua maisha ni nini,tatizo wengi tunatafuta vijana kwa kuona kwamba hawana majukum kumbe ndio watumiaji wa pesa kuliko wenye familia.
Mie niliwahi kufanya biashara ya bodaboda pia,nilikuwa nazo tano,na nimebakia na mbili kwa kuwa nilihamisha biashara kwenye Carry,lakini wakati nilipokuwa nazo hizo tano,ni Driver mmoja tu ndio alikuwa mkorofi,yaani pesa kulipa tatizo,kila siku pikipiki naikuta Buguruni Polisi,ukienda kuuliza unakuta keso za kuwapa mimba watoto wa watu.
Yaani alikuwa bwana mdogo basi madem walimkoma,yaani was under 20,ila mapaka siku naenda kwa mjumbe kuchukua Pikipiki mjumbe ananiambia kwa anavyojua yeye ni kwamba bwana mdogo kapiga watoto wanne mimba ndani ya mwaka mmoja tu wa kumpa Pikipiki.Maana alikuwa Day worker. Pesa wanapata ila wengie Wahuni sana,wahongaji sana na walevi.
Elli nitakuja unipe uzoefu wa Daladala