JF,
Nina Tsh 10,000,000/= , naomba msaada wa mawazo biashara gani nitafanya. SIna experience yoyote, nina elimu ya Degree, sina hobby yoyote ya kusema labda nichague kuifanyia bishara. Nachohitaji ni mawazo mbalimbali/tofauti tofauti ya biashara.
NB: Kama huna comment ya maana plz pita kimya kimya (sitaki matusi, ujinga, upumbavu, utoto). Narudia, ukiwa huna comment pita KIMYA KIMYA.... No bullshit comments.....
Mdau rasomaka;
Angalia mazingira unayoish, km inawezekana anzisha biashara ya bodaboda za mkataba (miez 10 baada ya hapo inakuwa ya kwake huyo dereva, matengenezo n jukumu la dereva)
Kwa 10 millions unanunua pkpk 4 (pkpk moja inauzwa around 1.8 mil san lg inapendwa zaid, ingawa zpo nyngne za bei pungufu)
Na kila pkpk kwa siku inaingza sh. elfu 10, baada miez 6 kila pkpk imeshajrudshia hela yake ya manunuz ile miez mi4 ilyobak faida. (Mwisho wa mkataba kila pkpk inazaa nyingine)
Biashara n kupata faida, kutanuka na kuzaa biashara nyingne.
Ukikusanya hela ya pkpk 4 kwa miez 3 (1,200,000×3=3600,000/=) ni hela ambayo unaweza kununua pkpk ya matairi matatu (bajaji) ya mizigo/maji ambayo itakuletea kipande kwa siku sh. elfu 15 ( kwa mwez lak 4 ukiondoa matengenezo)
Au kuamua kununua pkpk nyngne tena na kupanua wigo mkubwa wa bzness ambapo mpk pkpk za kwanza znaisha mkataba wake, ztakuwa zmeshazalisha nyngne nyingi.
Pia kwa hela unayokusanya unaweza kubuni biashara nyngne kutokana na eneo unaloish.
Changamoto:
Kila biashara haikosi changamoto, kwa pkpk changamoto kubwa ni kuibiwa/kutoroka na pkpk.
Mkataba uwe wa maandishi kwa m/kt wa mtaa ikiwezeka hata polisi mnaandkshiana ili kuwe na usalama.
Bodaboda ya mkataba n nzur kwa wote, tajiri na dereva, dereva anafaidika kwa kuwa baada ya kumalza mkataba anaimiliki inakuwa yake hivyo atakuwa makini na ataitunza. Matengenezo n jukumu lake.
Bodaboda za kipande kwa kila siku n majanga sana, dereva akishaona imechoka anaiacha na kutafuta nyingne mpya.
Ni hayo mawazo yangu nawasilisha.