Mkuu
bab-D umakini kwenye Hali ya Hewa ya ukanda huo nao lazima uuzingatie sana sana! usianze kilimo kwenye kipindi cha changamoto na ukinzani mwingi kati ya hali ya hewa,soko na nguvu kazi.
Kwa nini nasema hivyo?
HALI YA HEWA
Ukianza project ya nyanya kipindi cha mvua nyingi,utakutana na vikwazo vingi sana. Kipindi hiki wadudu na ukungu hushamiri. Hivyo utatumia nguvu nyingi sana kuikabili hii changamoto hasa kwa nyanya. Nashauri bora upande HOHO.
SOKO
Kuna kipindi zao fulani huwa linafurika sokoni na kupelekea mpolomoko wa bei, ukikutana mkulima ambaye hajatumia nguvu nyingi kwenye gharama yeye yupo radhi auze hata plastic 1 ya nyanya kwa sh1000,lazima akuvuluge tu!
NGUVUKAZI
Mara nyingi sana kwenye msimu wa kilimo upatikanaji wa wasaidizi huwa ni tatizo kubwa sana. Make nao hujikuta wapo kwenye uzalishaji kwenye family zao. Inabidi uzidishe umakini kwenye kutarget kipindi gani huwa wapo loose.
Hakikisha unaingia nao mkataba. Chukua angalau wawili wenye uzoefu wa kazi. Ingia mkataba wa hadi mavuno. Mimi huwa tunaelewana sh200000-250000. Kawaida mkataba huanza baada ya kupanda zao.Utatoa advance baada ya kuona sustainance ya zao.
Nimeona nikazie hapo ili uangalie uwezekano wa either usipeedup project yako kujihami na hizo constraints tajwa hapo juu. Ukianza na ukinzani mwingi utateseka sana na kwanini ufail wakati kuna uwezekano wa kukwepa majanga? na why uanze na majanga?
Pambana mkuu na karibu sana kwenye kilimo!!
CC
Zanzibar Spices