Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Angalia fursa iliyopo mtaani kwako. Usianze biashara kabla hujajua hitaji lililokosekana sehemu unayotaka kuanzisha biashara. Pili hiyo biashara uanatakiwa uwe na ujuzi nayo la sivyo hela yote itayeyuka. Milioni kumi ni ndogo sana kwa biashara itapotea fasta.
 

Tafadhali nitumie simu yako -
 
Mkuu pesa ya urith haifanyiwi biashara....ujui mzee kapataje..nenda tafuta kiwanja jenga then pangisha itakusaidia maisha yako yoote
milioni 10 kiwanja na ujenzi atajenga nyumba au mabanda?
 
Kama una ajira ya uhakika nunua kiwanja na kama unacho jenga hata vyumba viwili na sebule hiyo itakusaidia kupunguza stress za maisha na pia mshahara utakaokuwa unapata kiasi kikubwa utakuwa unakihifadhi na kupata mtaji wa biashara baadae kwani kwa sasa uchumi haujatulia hivyo si vizuri kukurupuka.
 
Nina mtaji kma m5 nifanye biashara gani,maana nimefikiri nimefika mwisho jibu sina,plz msaada.
kwanza una fani gani uliyosomea? kwanza unatakiwa ufikirie biashara au kujiajili kwa fani uliyosomea mfano wewe ni hotelia fikiria kwanza kunzisha mgahawa au catering au reservtion services etc, kama mwalimu fikiria kuanzisha tuition centre au shule ya awali au shule ya msingi kutokana na mtaji wako. ingawa unaweza kwenda nje ya taaluma yako lakini utatumia nguvu nyingi kupata mafanikio kuiko kufanya kitu kilichopo ndani ya uwezo wako, mfano mimi ni mhasibu tuna accounting firm na tuna train computer accounting package ni vitu ambavyo nimesomea ni rahisi kwangu kuviendeleza
 
Njoo tufuge, nguruwe kuku na sungura. Mimi nina utaalamu, uzoefu na muda wewe una hela. Tuungane (chini ya mwavuli wa uaminifu) tufanye hii biashara.

NB: Tutakua shea kwenye huo mradi, strictly sitaki kuwa mwajiriwa.

Just an option.
 
mkuu njoo pm kuna project ndani ya mwezi tu pesa yako inarudi,cha msingi ni uthubutu,kujiamini na kutokukata tamaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…