Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Wadau mimi ni Mwajiriwa,

Katika mambo ya urithi leo hii nimepewa mgao wangu wa 10mil cash. Nimeweka kwenye Account yangu nafikiria kitu cha kuifanyia.

Kwa nyie wazoefu, nipeni ushauri kibiashara ila mkizingatia mie ni mwajiriwa.

Nitashukuru kwa kila wazo chanya
Angalia fursa iliyopo mtaani kwako. Usianze biashara kabla hujajua hitaji lililokosekana sehemu unayotaka kuanzisha biashara. Pili hiyo biashara uanatakiwa uwe na ujuzi nayo la sivyo hela yote itayeyuka. Milioni kumi ni ndogo sana kwa biashara itapotea fasta.
 
Mkuu Mbu,

Njia nyingine pia ya kuharakisha mjadala ingekuwa kutuambia product idea zako halafu ukapata maoni kuhusu soko likoje kwa kila product idea.

Otherwise kama alivyosema WoS what's your core strength? Maana sio siri biashara ni zaidi ya mke, ni zaidi ya familia. You'll find yourself spending more time on your business especially in the beginning kuliko muda utakaokuwa unaspend na mamaa/papaa na watoto.

Off head kuna hii kitu ya online dating. You can throw a twist on the game by requiring your members to test for HIV, and charge men for ladies contacts.

Kuna wagoni wengi tu mfano maofisini ambao ni madomo zege lakini kila mwezi wanapenda kubadili mboga. Hao watakuwa wateja wako wakuu.

Plus internet population ya Tz itaexplode by Aug. this year .. so you can start building now.

Tafadhali nitumie simu yako -
 
Kama una ajira ya uhakika nunua kiwanja na kama unacho jenga hata vyumba viwili na sebule hiyo itakusaidia kupunguza stress za maisha na pia mshahara utakaokuwa unapata kiasi kikubwa utakuwa unakihifadhi na kupata mtaji wa biashara baadae kwani kwa sasa uchumi haujatulia hivyo si vizuri kukurupuka.
 
Nina mtaji kma m5 nifanye biashara gani,maana nimefikiri nimefika mwisho jibu sina,plz msaada.
kwanza una fani gani uliyosomea? kwanza unatakiwa ufikirie biashara au kujiajili kwa fani uliyosomea mfano wewe ni hotelia fikiria kwanza kunzisha mgahawa au catering au reservtion services etc, kama mwalimu fikiria kuanzisha tuition centre au shule ya awali au shule ya msingi kutokana na mtaji wako. ingawa unaweza kwenda nje ya taaluma yako lakini utatumia nguvu nyingi kupata mafanikio kuiko kufanya kitu kilichopo ndani ya uwezo wako, mfano mimi ni mhasibu tuna accounting firm na tuna train computer accounting package ni vitu ambavyo nimesomea ni rahisi kwangu kuviendeleza
 
Njoo tufuge, nguruwe kuku na sungura. Mimi nina utaalamu, uzoefu na muda wewe una hela. Tuungane (chini ya mwavuli wa uaminifu) tufanye hii biashara.

NB: Tutakua shea kwenye huo mradi, strictly sitaki kuwa mwajiriwa.

Just an option.
 
mkuu njoo pm kuna project ndani ya mwezi tu pesa yako inarudi,cha msingi ni uthubutu,kujiamini na kutokukata tamaaa
 
Back
Top Bottom