Msanii/mbu
Kama mnamaanisha ktk biashara hii ya miti,nipe e mail address zenu halafu tuone tutafanya nini.Sitaki hela ya mtu.Mimi nilishituliwa na mshikaji bure na mimi nitakusaidia bure. Michanganuo yenu mtafanya baadae mkipenda. Mimi sikufanya hiyo michanganuo.
Mkuu Malila kwa nini hilo unalotaka kulieleza usiliweke hapa, lakini kama inahitajika email nami nitakutwangia ya kwangu nifaidike.
Kwa ufupi nimekuwa ktk sector hii ya miti kwa muda mrefu sana. Naomba mchague wenyewe eneo mnalotaka nishushe data kati zifuatazo;
1; Ardhi ya bei poa iko wapi? na taabu za huko
2; mbegu zinapatikana wapi? na namna ya kuotesha?
3; Aina ya mti(mbegu,growth rate,soko,na sehemu ya kupanda ktk Tz)
4; Msimu mzuri na maandalizi yake.
5; overhead cost baada ya kupanda.
6; Field management.
Mimi ni mfugaji, nitakushauri kufuga ngombe kwa mchakato ufuatao:
Kumbuka ng'ombe huzaa kila mwaka hivyo basi baada ya miaka mitano utakuwa na ng'ombe wasiopungua 25. Kipato chako kwa mwezi unaweza kufikia si pungufu Tsh 18,000,000 endapo utakuwa na ngombe jike 20 kati ya hao 25.
Tafadhali Mkuu malila usije ingia huko msituni, kabla ya kumaliza lecture hapa! We need this mkuu! Hasa hapo kwenye field management......!
Nilikuwa na kamsitu huko IR ka pines zote ziliungua, so was very discouraged hata sijarudia kupanda tena miti!
tatizo lenu watanzania mnapenda sana kuwabana watu, haya mambo ya uzoefu sijui wa muda gani ndo yanayotunyima kazi vijana wa sasa. Mimi nimepata digrii yangu ya political Science pale Mlimani nimeingia uraini muda si mrefu mnaanza fitna za uzoefu!!! Wewe cha msingi angalia mikakati yangu kama inafanya kazi lete ulaji sio kutoa kauli zakubaniana namna hiyo. Mimi hiyo kazi naiweza na nakuhakikishia ndugu yangu Mbu ukitaka unaingia bungeni bila wasiwasi. Nipe kazi Mkuru
...stanmokiwa, mchakato wako kwa kweli umenivutia. Naomba kuuliza swali la nyongeza. Ni lazima kununua hao ng'ombe walio na miezi sita? Upatikanaje wake ni vipi,..maana kama kila mfugaji atataka ng'ombe aliye na mimba ya miezi sita demand itazidi supply, ama ushauri huo ulilenga kwangu kwakuwa naanza?
Pili, vipi kuhusu aina ya ng'ombe na upatikanaji wake? ni ng'ombe yeyote wa kienyeji naweza kununua, au ndio wale wa 'kidhungu' kina;
View attachment 4493 Ayshire,View attachment 4494 Brown Swiss
View attachment 4495 Guernsey,View attachment 4496 Holstein-Friersien,View attachment 4497 Jersey?
maana nishasikia majina kama 'chotara' nk...
nawakilisha!
Field management,
Zamani tulichukulia shughuli hizi za misitu kiurahisi sana,majanga yanapotokea hasa moto hakuna mwenye uchungu. Unatakiwa kuwa na mtu ambaye anakuwa sehemu ya msitu wako kabisa, hilo limenisaidia mimi mara mbili. Ni lazima kijana/mtu wako ahisi na yeye anafaidika na mradi ule. Badala ya kuwapa fedha cash mimi nawalipa bati za kuezekea,kwa hiyo hata kama ni mzembe akiona bati anakumbuka msitu. Njia hii inafanya familia nzima inawajibika kutunza msitu.Wenyewe wanasema win win situation.
Njia ya pili ni kuanzisha msitu mkiwa wengi kama estate vile,ili firebreak iwe kubwa sana.Hapa mimi nimefanikiwa sana kwa sababu niko na vijana kama 24 hivi na wote tunapanda miti kwa pamoja kwa kugawana eneo moja. Tunaokoa gharama sana kwa kuchangiana,kiasi kwamba kila mmoja anaona raha. Kila mwezi kuna mtu anakwenda kuwatembelea shamba kuwajulia hali zao vijana wetu.
wajameni eeh, nimebahatika "kupata" mahala ka-Mtaji. Ni kiasi cha shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.
Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida.
(i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake)
Kama ni ng`ombe, chukua waliozaliwa pwani hii hii, wale wa kutoka mikoani siku za mwanzo wanahitaji uangalifu sana mkuu. Nenda Ruvu mzee.
Mkuu malizia zote basi!
Nunua kiwanja na ujenge au nyumba mbovu na ikarabati katika miji inayokua na iliyopa maeneo ya ya barabara kuu na wekeza gesti.
Inalipa sana. Assume umejenga gesti moja ya kiwango cha 4m,nauhakika itapata wateja wa uhakika na fedha yako itarudi baada ya muda mfupi.
Kwa miji midogo gesti ya 4m inaonekana ya 5star.
Nunua kiwanja na ujenge au nyumba mbovu na ikarabati katika miji inayokua na iliyopa maeneo ya ya barabara kuu na wekeza gesti.
Inalipa sana. Assume umejenga gesti moja ya kiwango cha 4m,nauhakika itapata wateja wa uhakika na fedha yako itarudi baada ya muda mfupi.
Kwa miji midogo gesti ya 4m inaonekana ya 5star.
Nunua kiwanja na ujenge au nyumba mbovu na ikarabati katika miji inayokua na iliyopa maeneo ya ya barabara kuu na wekeza gesti.
Inalipa sana. Assume umejenga gesti moja ya kiwango cha 4m,nauhakika itapata wateja wa uhakika na fedha yako itarudi baada ya muda mfupi.
Kwa miji midogo gesti ya 4m inaonekana ya 5star.
Ndugu yangu ni PM, biashara ziko nyingi sana,huo mtaji ni mkubwa sana. Barclays walisaidia watu sana na wana jina kwa sababu ya kutoa hioz million kumi kumi.
Katabazi.
Wewe ndo ulichagua hii ya mwisho, ya field management,haya chagua tena nyingine nikupe.