Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Nafanya forex nataka niwe na kitega uchumi kingine cha ziada
Mkuu Hii milion kumi umeipata kwenye forex au unaondoa mtaji kwenye forex? Huku mitandaoni utapewa nadharia zaidi ya uhalisia. Iweke fixed deposit kwa miez mitatu huku ukichunguza business opportunities, miezi mitatu ikiisha hujapata ongeza mingine. Utakapopata biashara ya kufanya usiwekeze mtaji wote kwa pupa, Weka kiasi nyingine rudisha fixed deposit kwa miez kadhaa ndani ya huo muda utakuwa umejua ni capital injection ya kiasi gani inahitajika kwenye biashara yako. Kama haina faida utakuwa bado hujapoteza mtaji wote
 
Mkuu Huku mitandaoni utapewa nadharia zaidi ya uhalisia. Iweke fixed deposit kwa miez mitatu huku ukichunguza business opportunities, miezi mitatu ikiisha hujapata ongeza mingine. Utakapopata biashara ya kufanya usiwekeze mtaji wote kwa pupa, Weka kiasi nyingine rudisha fixed deposit kwa miez kadhaa ndani ya huo muda utakuwa umejua ni capital injection ya kiasi gani inahitajika kwenye biashara yako. Kama haina faida utakuwa bado hujapoteza mtaji wote
Nimependa wazo lako ntalifanyia kazi
 
Ndio ninachotaka kufanya mkuu
Pamoja na uzefu wangu kwenye maswala ya fedha Ila Sijawahi kufanya forex' najua ni biashara halali Ila naona kama kwa sababu risk ya kupoteza ipo juu sana inasababisha iwe kama gambling. Ww umeweza vipi kucontrol risk?
 
Pamoja na uzefu wangu kwenye maswala ya fedha Ila Sijawahi kufanya forex' najua ni biashara halali Ila naona kama kwa sababu risk ya kupoteza ipo juu sana inasababisha iwe kama gambling. Ww umeweza vipi kucontrol risk?
Mimi nilimlipa mtu akanifundisha
Na mara nyingi nakuaga chini ya uangalizi wake ninapo trade
 
Habari za muda huu.

Mimi ni kijana wa miaka 19 katika kupambana kwangu nimeweza kupata kiasi cha 10,000,000/=(million kumi). Kwa wazoefu wa uwekezaji naomba mniambie naweza kuwekeza kwenye nini ili niwe napata consistent profits.

Nawasilisha kwenu.

Ningependa kujua kitu kimoja au viwili ulivyofanya ukafanikiwa kupata million 10

Nimepata majibu ulipatia forex..je tofauti n forex ulishawai fanya kitu gani au ulishawai kusimamia biashara gani ata kama ya mtu?

Kila biashara inalipa ukiifanya kwa nidhamu na umakini
 
Hongera, kwanza kwa kupata hicho kiasi cha fedha ukiwa na umri mdogo

Pia, kwa umri ulionao sina budi kukupa hongera kwa kuwa na mawazo ya kuwekeza zaidi ili uwe na kipato endelevu kupitia hiyo hela uliyonayo

Sitakutajia biashara ya kufanya, nitakutajia mbinu ya kupata wazo

1. Angalia jambo ambalo unaliweza na unalifanya kwa urahisi lakini watu wengine wanalifanya kwa tabu.......(hapa kuna mchanganyiko wa kipaji ulichonacho na kufanya kitu unachokipenda)

2. Angalia mazingira uliyopo, watu wanalalamika au watu wanateseka kupata bidhaa gani au huduma gani, kisha uza hiyo bidhaa au huduma

3. Copy biashara unayoona inaingizia watu mpunga wa kutosha kisha fanya hiyo biashara
Habari za muda huu.

Mimi ni kijana wa miaka 19 katika kupambana kwangu nimeweza kupata kiasi cha 10,000,000/=(million kumi). Kwa wazoefu wa uwekezaji naomba mniambie naweza kuwekeza kwenye nini ili niwe napata consistent profits.

Nawasilisha kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu wana jamvi naombeni ushauri, wanasema penye wengi hapakosi jambo.

Mimi ni mwajiriwa, nimekuwa nikitamani kuacha kazi na kufanya biashara lakini nakuwa muoga, nikiwa na mawazo je ikifeli?

Nimejaribu kusave na kufungua salon nikiwa bado job nikashindwa, vijana walikuwa sio waaminifu.

Sasa hivi nataka niache kazi kabisa biashara nitakayoifanya niisimamie mwenyewe, lakini naumiza sana kichwa. Je, kwa mtaji wa 6,000,000 au 7,000,000 naweza kufanya biashara gani ambayo angalau itanipatia faida ya 30,000 kwa siku?

Nashukuru sana kwa mawazo yenu mazuri.
Mkuu nilitaka kukupm kwa bahati mbaya umefunga
 
Back
Top Bottom