Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Wakuu habari za humu ndani? Poleni na majukumu na heri za mwaka mpya 2020.

Awali ya yote Mtanzania mwenzenu ndugu yenu ninaomba msaada wa kimawazo ya biashara kwa kuwa nahitaji kubadili 8 million iwe billion, changamoto ni kwamba biashara gani inaweza kubadilisha hiyo pesa ndani ya muda mfupi pia ni vyema kujua faida na hasara nisingependa kuipoteza kwa kiasi kikubwa ila nikuiongeza.

Naombeni mawazo yenu wenye uelewa zaidi kibiashara na si mawazo potofu kwa wachagia mada tusaidiane na sio kupotezana tuwe wazalendo na wapenda maendeleo kama vijana na wanaharakati ukijihisi mpotoshaji naomba kaa pembeni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo la kumpa mtu ushauri ni kuendelea kumpoteza katika kuomba ushauri unapaswa useme wewe kwa upande wako unapenda kufanya jambo gani ili wachangiaji wakuongezee maarifa juu ya hilo jambo.

Nasema hivyo kwa kuwa watakuja wakusema kafuge kuku ng,ombe n.k nawatakuja wakusema kafanye biashara fulani nafulani.


Unaweza kuchukua ushauri ila usiwe ushauri utakao kutatulia changamoto za mradi unao enda kuufanya.

Mwisho wa siku unajikuta katika hela yako unamebakiwa na sifuri.
 
WEWE NENDA KAFUGE NGURUWE HAYO MAMBO YA SWOT ANALYSIS NDIO YANAFANYA WASOMI WENGI WASIWE WAFANYA BIASHARA WAZURI! MUULIZE BARHESA AU MENGI KAMA WALIPOANZA BIASHARA WALIKUWA NA UOGA WA KUTHUBUTU! BIASHARA NI KUANZA TU ACHANA NA HIYO MICHAKATO
 
1. Ninunue bajaji moja (mpya) na niipigie kazi mwenyewe bila kumpa kijana yoyote.

2. Nifungue biashara ya duka la rejareja nizichange hizo shilling 50 had mtaji ukue.

3. Niende kulima mpunga kukodi, kuandaa shamba heka 1 had kupanda nitenge laki 3 nisubiri muda wa mavuno nivune guni 9 had 10 katika kila heka nikilima heka 10 kwa million 3-4 kama hali ikiwa vizur nipate angalau makadirio ya gunia 100 niweke stock, maana kuna kipind mpunga unafika had elf 90 gunia moja, hapo nikipata hata million 8 kwenye 4 nitakayoichimbia siyo mbaya

Au nifanye biashara ipi nyingne naomba ushauri zaidi.

GunFire
 
Fanyia kazi hili wazo.

Risk yake ni ndogo ukilinganisha na hizo biashara zingine tajwa.
 
Kama upo maeneo ya mijini, nunua bajaj piga kazi mwenyewe, pakibuma sehemu moja unahamia sehemu nyingine, ukiichoka biashara unaiuza hiyo Bajaj kwa bei yoyote ya soko. Risk ya hii biashara ni ndogo sana.

Sikushauri kabisa kufanya biashara ya duka la rejareja au kulima ikiwa hujawahi kabisa kuifanya hiyo biashara katika maisha yako kwa kutumia mtaji wako. Ni biashara nzuri kwa maneno ya kusikia kwa wengine au kupiga mahesabu kwenye makaratasi lakini kiuhalisia ni tofauti sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…