Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Toa 2.5m nunua boxer endesha mwenyewe kwa siku unapata 60-70k kwa mwezi unapata 1.8 or 2m ...hujaishi kifalme mpaka hapo?
 

Nenda ukaziweke kwenye FIXED DEPOSIT ACCOUNT Bank ya NMB, utapata TShs 49,875/= kila mwezi kwa rate ya 9.5% per annum.
Angalia taarifa zao ziko hapa, pamoja na CALCULATOR yao, halafu jaza kiasi cha pesa unayotaka ili uweze kujua utapata kiasi gani

StackPath
 
Hebu nifafanulie hili vizuri, website yao haifunguki
 
Mmhh umewahi kuweka na kupewa faida kwa hiyo rate? Mimi huwa naona rates zao hazizidi 7% kwa mwaka.
 
Mkuu hebu naomba unieleweshe vizuri hapa
Naam ndugu; nijuavyo Mimi ni kwamba, rates za NMB bank zinaanzia 2% hadi 7% kwa kiasi kisichozidi 199,999,999/=. Inategemeana na muda wa kuweka pesa zako. Na kiasi cha chini kabisa ni 500,000/=.

Mfano ukiweka 10m kwa miezi mitatu inakuwa kama ifuatavyo; 3/12 *2.75/100*10,000,000 =68,750.
Hivyo ukiweka 10m kwa muda wa miezi mitatu katika akaunti ya muda maalumu (fixed deposit account), utapata 68,750 kama faida. Naam, kwa kiasi kikubwa rates zinaanzia kati ya 2% hadi 7% kwa mwaka.

Ukiwa na 200m and above wanakuambia uwaone *treasury department*. Niliwahi kuuliza rate ya 9.5% inatumikaje, waliniambia ni kwa anayeweka kuanzia 700m na kuendelea. Kwa taarifa zaidi, unaweza kuwatembelea ili upate kujua kwa kina.
 
Asante sana mkuu

Duuh return yake ni ndogo mnoo, Bora niendelee kucheza upatu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…