Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Habari kuna sehemu nilikuwa nimeajiriwa sasa nimejikusanya na kupata milioni 5 baada ya mkataba wangu kuisha nifanye biashara gani ya kuingiza faida ya isiyopungua 30000 kwa siku ushauri wenu ni mhimu sana asanteni sana.
Bro anzisha kinaenda chakuchoma mishkak ni mitamu balaa
 
Kama una leseni na muda nunua TVS bajaj used ya 4m zipo nyingi tu ukomae nayo mwenyewe kufunga ef30 kawaida sana wanapiga mpaka 50,60 kwa siku.Utatumia kama laki 2,3 kufanya service ndogo inayobaki 800k acha kwenye acc kwa ajili ya dharula.

NOTE:Brand ni Tvs tu si nyingine
 
Hivi nyie mnatamani kweli kuiona kesho ya furaha nawashangaa watu wakija humu ushauri n bodaboda/bajaji au mama ntilie hv tutakuwa mabilionea lini?

5m m pesa nyingi kwa mtu ambaye anauchungu wa kutoka kimaisha Tanzania tupo zaidi ya watu 50m,

50millions people's n wengi mno na ndio mtaji tosha nenda nje ya mji angalia wanakosa nn na wanauhitaji wa kitu gani kwa Sana funga safari nenda mkoa ambao inaonekana haufikiki hata wilaya tathmini Biashara chapu nunua mzigo wa 2m peleka utapata MAJIBU.

Tuache kupeana mawazo ya bodaboda ambapo saiz wamekuwa kero Yan ukiwa msafi msafi ukitokea mbele yao kosa Yan karibu kijiewe kizima kinawasha pikipiki sasa ukiona hvyo n shida na risk ya pikipiki n kubwa kuliko kwenda kuiba bank
 
Habari kuna sehemu nilikuwa nimeajiriwa sasa nimejikusanya na kupata milioni 5 baada ya mkataba wangu kuisha nifanye biashara gani ya kuingiza faida ya isiyopungua 30000 kwa siku ushauri wenu ni mhimu sana asanteni sana.
Katika M5 toa M1 na mimi M1 Tutafute eneo pale makumbusho tuweke biashara mm ninamda wa kusimamia nitakua tutagawana faida
 
Cha msingi angeulizwa mtoa uzi anapenda kufanya biashara gani?
Ana skills za kitu gani?
Ana watu wa karibu ambao wako vizuri kwenye biashara gani?
Angependa kufanyia wapi biashara yake?
Hio biashara ndio itakuwa ya kuendesha familia au faida itakuza biashara?
Ashawai kufanya biashara gani?
 
Nenda bank weka hiyo hela yote fixed acc, kwa miezi 6 tu, upate angalau 40,000/= au 50,000/= kila mwezi, huku ukisubiri kipindi cha mavuno bei ikipungua, chukua fedha yako yote bank, then nunua mchele weka stock bei ikipanda uza. Lazima utatoboa. Mambo ni taratibu.
 
Bank gani nzuri mkuu kuweka mzigo?
 
Nenda bank weka hiyo hela yote fixed acc, kwa miezi 6 tu, upate angalau 40,000/= au 50,000/= kila mwezi, huku ukisubiri kipindi cha mavuno bei ikipungua, chukua fedha yako yote bank, then nunua mchele weka stock bei ikipanda uza. Lazima utatoboa. Mambo ni taratibu.
Hii biashara ni nzuri naskia.

Ila upate sehemu nzuri ya kuhifadhia mpunga

Upate watu wazoefu watakaokusaidia kupata wateja.

Na pia wakusaidie kukuzoesha katika biashara.

Kinyume na hapo utaisoma namba
 
Mkuu hiyo buku 7 ni kwa mkoa gani na sehemu ipi ya mji?

Ila pia kwa huo mtaji wa 5M kwamba atapata baishara ya kupata faida ya 30K kwa siku si rahisi sana. Inabidi akubali kuanzia chini kabisa. Na kama hana uzoefu kabisa asiweke pesa yote. Atalia machozi. Mie kwa uzoefu wangu nadhani katika watu 50 wanaoaza biashara basi wanaofanikiwa wanaweza wasizidi hata watano. Siyo kutatishana tamaa ila lazima tuambizane ukweli. Hasa hizo biashara za kununua bidhaa na kuuza. Si masihara.
Kwa mtaji wa 5m naingiza hiyo faida bila shida mkuu inategemeana na location
1)location za wavuvi na migodini
Hapa pana biashara nyingi mfano ukitengeneza ngarawa a.k.a kikwarukwaru kwa hiyo pesa unaweza pata ngarawa 20 na ngalawa moja hukodishwa kuanzia elfu 3 hadi 5

2)duka la nguo ukiwekeza 4m huwezi kosa hiyo 30

Mkuu kifupi hiyo pesa unawekeza vizuri ukichagua location usiwe mvivu kutembea hata mkoa mwingine

Ila kwenye Boda mkuu sikushauri labda uendeshe mwenyewe halafu ujenge uaminifu mkubwa sana
 
Back
Top Bottom