Uzuri wa IR ni huu,ardhi ipo,mvua zinanyesha sana,barabara zipo,wahehe wanaogopa kuiba cha mtu,wahehe hawabagui mgeni. Wewe fanya kilichokupeleka kwa utaratibu basi,halafu unaambiwa karibu tena. Wasichotaka, usiwadharau tu basi. Kazi wanafanya kwa kiwango cha kuridhisha ila baadhi ya vijiji tutapeli tumeingia.
Milingoti hasa Saligna na grandis,ina kuwa haraka na ni multipurpose yaani waweza kuuza kama nguzo za umeme,au boriti za kawaida au ukachana mbao.Wewe ukiwa na milioni moja inatosha kununua eka kumi na kupanda miche 6000 ya milingoti/pines ya mbao,kisha unaondoka kurudi zako mjini. Unakwenda huko june kuweka fireline na kurudi tena mjini. Baada ya miaka mitatu unaprun miti yako. Kwa hiyo mwendo ni huo.
Mimi na vijana wenzangu tumeunganisha nguvu na kununua eneo kubwa,tunaotesha wenyewe miche ya pines/mlingoti na kupanda ktk plots zetu. Mwaka huu tumepanda miti laki tatu kwa pamoja tuko sita tu. Ila mpaka sasa vijana waliopanda miti eneo lile tuko 24 hivi. Msimu ujao tutakuwa kama 30 jumla.
Wenzetu walikwama msimu huu kwa sababu mbalimbali. Tuna jirani mmoja kutoka Kenya yeye peke yake amepanda milingoti milioni nne. Yeye ardhi kapewa na serikali yetu tukufu. Usijali ndo hali halisi. Mmalawi mmoja kajimegea eka 1000 na amepanda miti.