Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Wadau mimi ni Mwajiriwa,

Katika mambo ya urithi leo hii nimepewa mgao wangu wa 10mil cash. Nimeweka kwenye Account yangu nafikiria kitu cha kuifanyia.

Kwa nyie wazoefu, nipeni ushauri kibiashara ila mkizingatia mie ni mwajiriwa.

Nitashukuru kwa kila wazo chanya

naomba kujua...mwajiriwa wa serikali au laa?...kama ni muajiriwa wa serikali na hasa hii ya magufuli...na kwa katiba ya warioba....hairuhusiwi muajiriwa wa serikali kufanya kazi nyingine inayoingiza kipata nje ya ajira yake....

kama sio mwajiriwa wa serikali sema nikupe ushauri.
 
Uzuri wa IR ni huu,ardhi ipo,mvua zinanyesha sana,barabara zipo,wahehe wanaogopa kuiba cha mtu,wahehe hawabagui mgeni. Wewe fanya kilichokupeleka kwa utaratibu basi,halafu unaambiwa karibu tena. Wasichotaka, usiwadharau tu basi. Kazi wanafanya kwa kiwango cha kuridhisha ila baadhi ya vijiji tutapeli tumeingia.

Milingoti hasa Saligna na grandis,ina kuwa haraka na ni multipurpose yaani waweza kuuza kama nguzo za umeme,au boriti za kawaida au ukachana mbao.Wewe ukiwa na milioni moja inatosha kununua eka kumi na kupanda miche 6000 ya milingoti/pines ya mbao,kisha unaondoka kurudi zako mjini. Unakwenda huko june kuweka fireline na kurudi tena mjini. Baada ya miaka mitatu unaprun miti yako. Kwa hiyo mwendo ni huo.

Mimi na vijana wenzangu tumeunganisha nguvu na kununua eneo kubwa,tunaotesha wenyewe miche ya pines/mlingoti na kupanda ktk plots zetu. Mwaka huu tumepanda miti laki tatu kwa pamoja tuko sita tu. Ila mpaka sasa vijana waliopanda miti eneo lile tuko 24 hivi. Msimu ujao tutakuwa kama 30 jumla.

Wenzetu walikwama msimu huu kwa sababu mbalimbali. Tuna jirani mmoja kutoka Kenya yeye peke yake amepanda milingoti milioni nne. Yeye ardhi kapewa na serikali yetu tukufu. Usijali ndo hali halisi. Mmalawi mmoja kajimegea eka 1000 na amepanda miti.

Habari Malila
Asante kwa maelezo kuhusu wahehe - I take it as a genuine compliment!
Ingawa hii post ni ya miaka mingi iliyopita niko interested kujua project yenu inaendeleaje.Bado mnaiendesha? Mimi nina ndugu na jamaa wengi huko IRA.
 
Thanks msanii,

Wazo la kuwekeza ktk ardhi hasa miti (mitiki,milingoti,pines) ambayo growth rate yake ni kubwa na ina good future ni bomba sana. Hizo hela ni nyingi sana kwa shughuli za kuwekeza ktk miti ie mitiki kwa kuanzia. Siku ukipata hela kidogo kama milioni moja hivi nitafute,nitakupa mchanganuo kwa vitendo bure ushindwe mwenyewe.

Kwa sasa,tujitahidi kukamata ardhi ndugu zangu,tuendako kubovu sana.

Malali,mimi nina hiyo milioni 1 tayari.Any suggestion ni vipi naweza ku-invest?
 
Habari Malila
Asante kwa maelezo kuhusu wahehe - I take it as a genuine compliment!
Ingawa hii post ni ya miaka mingi iliyopita niko interested kujua project yenu inaendeleaje.Bado mnaiendesha? Mimi nina ndugu na jamaa wengi huko IRA.

Project inaendelea vizuri sana, tulianza 2006, tukiwa na eka 1.5 pale Mgagao tukiwa wawili, na leo tuko zaidi ya 350 tukimiliki eka 27 elfu katika mikoa mitatu.
 
Biashara ni biashara utakayo ifikiria anza na mtaji Mdogo, alafu kadri unapata uzoefu unaongeza mtaji. Na kama unaona biashara ulioanza haeleweki basi badili mapema. Na usiogope kupata hasara wakati wa majaribio.
 
Mbu,

wasiliana nasi upate ushauri wa uhakika, pia tutakuandalia Mchanganuo wa biashara(Business Plan) baada ya kukubalina na aina ya biashara unayoweza kuifanya.

Note: Kutakuwa na gharama ingawa sio kubwa. wasiliana nasi info@gmconsultz.com, ama ceo@gmconsultz.com,

JF pekee ni bussiness consultants tosha. Hizi ideas ambazo kila mmoja amedrop kwenye hii thread ni zaid ya thinking capacity ya kampuni ya consultant.
 
Anzisha biashara ya kufuga nguruwe. Kiti moto wanalopa
 
Wadau vipi,jamani uchaguzi umeshapita naona jinamiza la ukimya katka uzi huu umeshika kasi,labda kwasababu ya uchaguzi, sawa sasa uchaguzi umekwisha,naomba wataalamu wa eneo hilo la kilimo cha mbogamboga cha kumwagilizia,tupeane experience na njia bora za kuboresha kilimo hichi

Hoho zinalipa zaidi,lakini hata pilipili mbuzi zinalipa sana

Ni PM no yako tuongelee jinsi ya kutafuta masoko nje ya nchi
 
Sasa huyu Jamaa aliyeomba ushauri ameibuka na wazo kweli? Kumbe Si mchezo kubuni biashara
 
Soma post za toka mwanzo hakika utapata mawazo mazuri tuu..kama ukikosa Muombe Mungu then katoe sadaka
 
naomba kujua...mwajiriwa wa serikali au laa?...kama ni muajiriwa wa serikali na hasa hii ya magufuli...na kwa katiba ya warioba....hairuhusiwi muajiriwa wa serikali kufanya kazi nyingine inayoingiza kipata nje ya ajira yake....

kama sio mwajiriwa wa serikali sema nikupe ushauri.
Kwa mujibu wa sheria ipi mkuu, tuache mzaha na mambo serious.! Hakuna sheria inayomkataza mtumishi wa umma kufanya biashara.!
 
Wadau mimi ni Mwajiriwa,

Katika mambo ya urithi leo hii nimepewa mgao wangu wa 10mil cash. Nimeweka kwenye Account yangu nafikiria kitu cha kuifanyia.

Kwa nyie wazoefu, nipeni ushauri kibiashara ila mkizingatia mie ni mwajiriwa.

Nitashukuru kwa kila wazo chanya
Ielekeze katika Biashara ya mtandao wa masoko (Multi Level Marketing). Ni pm kwa Maelezo zaidi.
 
Na Mimi naomba mnishauri Nina mtaji wa M10 ila sasa sijajaliwa uwezo wa ubunifu wa biashara. Nawategemea wadau
Mkuu karibu tushirikiane kwenye kilimo morogoro, mm nalima ila sina mtaji wa kutosha njoo uwekeze huku kunalipa sana mkuu
 
Back
Top Bottom