Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

naweza kununua wapi ng'ombe hao nikiwa dsm na je ni kipindi kipi n'ombe hupunguza maziwa
 
kaka kagombee ubunge, nakuhakikishia zinatosha sana kuukwaa. Kwa mwezi utakuwa unazalisha si chini ya milioni 7 x mwaka mmoja (miezi 12)= 74 milioni. hHiyo pia izidishe miaka 5 (miezi 60)= 7 x 60 = 420 milioni.

situation anaysis ya mradi: Kama utajitosha kupitia CCM hali itakuwa kama ifuatavyo: wekeza kiasi cha milioni tano za kuwahonga wajumbe wa NEC ofcoz wapo kama 216 hivi (wadau mtanisahihisha), jitahidi kila mjumbe alau apate elfu hamsini. Hapa kuna uwezekano mkubwa wa kupita kama ni kijana mpya japo inategemea na jimbo unalotaka kugombea. Kwa ushauri wangu achana na majimbo yenye majina maana inaweza kukufika ya Bwana Mnyika pale ubungo. Kama wewe ni mchaga basi kazi ni ndogo nenda katufute jimbo lolote pale arusha, manyara na hata moshi (achana na majimbo ya ndesamburo na dr slaa hawa wameshapita
muda mrefu tu).
Jitahidi kuwahonga wenyeviti na makatibu wa ngazi ya wilaya hasa wale wa CCM na jumuiya ya vijana kama utapanga kugombea kupitia chama hicho. Pia huna haja ya kuzungumka mikoa mingi wewe deal na wale wa ngazi yako ya mkoa. Tena ushauri wangu nenda mikoa ya kusini kama huna hakika sana maana kule wabunge wengi wanahali mbaya si unajua jinsi walivyoshindwa kuwaunganisha vijana kule matokeo yake wote wanauza viatu na maji huku dar.

Kama utahiji kujua mikakati ya uchaguzi usipate shida, napatikana kwa gharama za kiasi cha milioni moja tu namaliza kazi ya kukuwekea sawa wajumbe wa halmashauri kuu. Wale wa wa jimbo wasikuumize kicha dawa ni kuwafuata kata kwa kata afu tunawaweka kwapani wajumbe wa kamati ya siasa mchezo kwisha. Tuwasiliane kwa private chat hapa hapa JF. Jambo muhimu la kuzingatia: Mfanyabiasha mzuri bni yule anayechukua HATARI katika kuwekeza. Kila la kheri.

Kweli JF ni mambo yote!
 
This is one of the most useful thread in JF. Ushauri mwingi umetolewa, inabakia utekelezaji tu kwa wajasiriamali.
 
Kanunue hisa za crdb ambazo zinauzwa at shs 150 per share. 10 m itakupatia shares 66,666. Hii maana yake nini. Kama ungepeleka DECI labda ungevuna 20m baada ya miezi 4? Sijui formula yao. Lakini ukinunua shares hizi crdb zikipelekwa kwenye soko la hisa unaweza ukaziuza zote halafu ukavuna zaidi ya asimia 100. Na hii ni baada sana sana ya miezi miwili. Kwa hiyo ukipata 20m zako iko mbaya gani/ U can decide kuziweka kwenye Fixed deposit ya hao crdb halafu ukaitumia hiyo kuombea mkopo. But this depends very much if u have a steady monthly income. Huo ni ushauri wangu wa bure

Wewe unauhakika na ulichoandika?Embu tupe formula co that is more than imagination kwa benki yoyote duniani

 
Simple! Nenda kakamat pikipiki zako tano za kichina. Kama kila pikipiki itakuingizia atleast Tsh 8000/- kwa siku then kwa zote utaweka Tsh 40000/- kwa siku. Kwa mwezi ni 1200000. Assume kila pikipiki itakucost 100000 kwa service kila mwezi. Utakuwa na uhakika wa 700000 kila mwezi...!
 
Asanteni wote mliochangia humu ndani. Kweli kuna watu si wachoyo wa MAARIFA na wapo tayari kuwasaidia wengine. Malila BIG Thanks to every detail you have given to this thread. Stay Blessed you and your Children Children.
 
Dah, hii kitu ni useful sana,
ingawa wengine wametoa michango ya kilanguzi languzi
 
Mgombezi, Je hawa ngòmbe wenye mimba ya miezi sita atanunulia wapi?
 
Mbu, Mawazo nyako ni mazuri sana,lakini je kwa hali ya sasa hivi bongo kila mtu kashastuka kuhusu ardhi,.je kiwanja cha 10mil utapata wapi?
 
kanunue maeneo ya ardhi nje ya mji(bagamoyo),kibaha,kisarawe,au kigamboni ndani ndani uyathaminishe then after 2 yeays utayauza mara 10 ya bei ulionunulia
 
Duuuuuuuuh,Nimebarikiwa sana na hii Thread,bila shaka ndiyo Bora kuliko zote ambazo nimewahi kuzisoma hapa Jf!!

Shukrani za Dhati zimwendee Bwana Mbu kwa kuanzisha Uzi huu,Bwana Malila kwa kunifungua Macho kuhusu Ujasiriamali kwenye Kilimo na Wote waliochangia!!

Tayari nimeshaanza kujihesabu Milionea,ngoja nisake Mtaji maana mawazo tayari yapo!! Jf ni "kijiwe" cha Wajanja!!!!
 
On a serious note: Mbu naomba utupe feedback ya huo mtaji..Je ulifanya biashara yoyote? ipi? na inakwendaje?

Hebu tujuze ukipata wasaa!!
 
Kama baadhi ya waliotangulia hapa napenda kusema asante Malila na Mbu kwa thread hii. Binafsi niko kwenye fani hii hii ya mashamba na mpaka sasa ninaendeleza juhudi zaidi ili kufikia malengo.
 
Kama baadhi ya waliotangulia hapa napenda kusema asante Malila na Mbu kwa thread hii. Binafsi niko kwenye fani hii hii ya mashamba na mpaka sasa ninaendeleza juhudi zaidi ili kufikia malengo.

Safi sana mkuu,
Kama tukiweza kupeana taarifa za mashamba mazuri tunapoyaona itakuwa vizuri sana. Saa nyingine unakuta shamba limekaa vizuri,lakini fedha huna, wa kumwambia huna,kesho mgeni anamegewa kipande kile. Lakini nikijua Momo anapenda basi inakuwa rahisi kukujulisha.
 
Safi sana mkuu,
Kama tukiweza kupeana taarifa za mashamba mazuri tunapoyaona itakuwa vizuri sana. Saa nyingine unakuta shamba limekaa vizuri,lakini fedha huna, wa kumwambia huna,kesho mgeni anamegewa kipande kile. Lakini nikijua Momo anapenda basi inakuwa rahisi kukujulisha.

Hii ni kweli kabisa, na mara nyingi hali inakuwa hivyo kwani mie binafsi mashamba yangu yote nimeyapata kwa kupitia taarifa za kupewa na jamaa zangu. Mara nyingi wanapewa taarifa ila pesa ya kununua inakuwa pungufu hivyo wananiunganishia mie. Pia nikishindwa na mie mara kadhaa nimewaunganishia wengine.
 
MBU leta update ulipofikia. au mawazo yote yalilyotolewa hukuyaafiki.
 
je unataka investment ya muda mfupi au mrefu, specify,pili biashara hiyo utasimamia mwenyewe au unataka uweke mtu wa kuisimamia? Je unataka biashara hiyo ndo uitegemee kwa maisha ya kila siku? Uko tayari kwenda kinyume cha imani yako(kama una imani/dini) ?


MKuu Malila, Heshima kwa kumtaka afafanue kilicho mawazoni mwake!! Lakini hiyo ya kumtaka mtu awe tayari kwenda kinyume na dini yake!! I wouldnt call that professional Consultancy! Tuweke mipaka katika mambo! hasa tukizingatia mila na desturi za kikwetu sisi watanzania. kuna biashara zingine kwa mfano danguro! zidhani mtanzania halisi mwenye dini na maadili ya kitanzania atafungua kitu kama hiki. na akifanya hivyo sina uhakika kama jamii , ndugu na marafiki watamkubali kwa wepesi wa hivyo.
cheers dude!
 
[/COLOR]MKuu Malila, Heshima kwa kumtaka afafanue kilicho mawazoni mwake!! Lakini hiyo ya kumtaka mtu awe tayari kwenda kinyume na dini yake!! I wouldnt call that professional Consultancy! Tuweke mipaka katika mambo! hasa tukizingatia mila na desturi za kikwetu sisi watanzania. kuna biashara zingine kwa mfano danguro! zidhani mtanzania halisi mwenye dini na maadili ya kitanzania atafungua kitu kama hiki. na akifanya hivyo sina uhakika kama jamii , ndugu na marafiki watamkubali kwa wepesi wa hivyo.
cheers dude!

Heri ya mwaka mpya mkuu?
Hilo eneo la kinyume na imani/dini ni pana sana mkuu, sio danguro tu. Kwetu bangi ni mboga na imani yangu ya dini inasema vyote alivyoviumba Mungu usiite najisi ( Chilumbile Nungu cha kumemena),nguruwe kwetu wanafugwa nje tu kama kuku wa kienyeji, ulanzi unanyweka tangu asubuhi mpaka jioni na ni biashara kubwa huko.Waliosomeshwa kwa biashara ya pombe za kienyeji watakuwa na msimamo upi kwa wazazi wao?

Hapo mlimani kwetu Kilimakyaro, kila baada ya nyumba mbili kuna grocery ya maji ya mende. Vipi Tabora/Songea wanakolima tumbaku? Watu wamezaliwa ktk jamii hizi zenye biashara kama hizi ambazo upande wa pili ni haramu.

Kama MBU angesema hana tatizo na imani yake, ningemwambia asafirishe swine na kuwaleta mjini kwa bei ya jumla. Napinga danguro, napinga kufuga swine/bar ktk maeneo ambayo jirani zangu ni wa imani zingine, napinga matumizi ya bangi/tumbaku.

Kwa hiyo unapomshauri mtu,angalia mazingira yake pande zote ili mradi wake uwe na kibali cha jamii anayokwenda kuishi nayo.
 
Back
Top Bottom