Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Kuanzisha biashara inategemea na fursa zilizopo eneo unalotaka kuanzisha biashara yako. Usiwe na papara zunguka eneo husika fanya uchunguzi wa kutosha then ukuje na proposal na sisi tutakushauri kati ya hizo chaguzi zako. Tunaweza tukakushauri ufungue duka la mchele kumbe sio kipaumbele cha eneo lako.
 
Habari ndugu zangu. Mimi ni kijana mwenye miaka 26 sasa nimepambana kutafuta mtaji wa kuanzisha biashara nzuri itakayo nifanya niendelee zaidi kiuchumi na kijamii

Naombeni mawazo yenu ni biashara gani nzuri naweza kuifanya na huu mtaji wa milion 10

Kusema kweli kwa upande wangu ninapenda sana kufanya biashara ya kilimo au kufungua kiwanda kidogo cha kusaga na kukoboa mahindi

Ila nadhani humu ndano kuna watu wenye uelewa mkubwa zaidi yangu na wanaweza kunipa mbinu mbalimbali na maarifa ya kukuza haka kamtajo kangu

Nawakaribisha kwa mawazo yenu.
Fuga kuku wa mayai, nibiashara ambayo watanzania wengi bado hawaja ichangamkia, uhitaji wa mayai ni mkubwa sana
 
Kuanzisha biashara inategemea na fursa zilizopo eneo unalotaka kuanzisha biashara yako. Usiwe na papara zunguka eneo husika fanya uchunguzi wa kutosha then ukuje na proposal na sisi tutakushauri kati ya hizo chaguzi zako. Tunaweza tukakushauri ufungue duka la mchele kumbe sio kipaumbele cha eneo lako.
Asante sana kwa ushauri
 
Ingia kwenye kilimo ama Ufugaji, saiz Biashara ziko chache sana zinazo lipa. Nyingi saiz usumbufu tu TRA kila kona yaani hakuna kupumua unajikuta faida kiduchu sana aisee.

Njoo Pm In Advance
 
Yes ufugaji wa kuku wa mayai na kuku wa nyama Is the best project kama ukiwa serious unatoboa
Kabisa mkuu, kuna Jamaa yangu anapiga hizo mishe ila yy ame simamia kwenye upande wa kuku wa Nyama aisee Jamaa anapiga hela vizuri tu. Kikubwa hizi Ishu uwe serious na utenge mda kabisa.

Kuku wa Mayai nao ni wazuri ila upate Vifaranga kutoka kampuni nzuri, sema yenyewe mkuu unasubilia miezi 6 ndio unaanza kula hela yako.
 
Back
Top Bottom