Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Chakula... ni lazima watu wale ukipata eneo zuri.

Maabara (uweke na duka la dawa).... kila siku watu wanaumwa.

Stationary, kama ukipata maeneo yenye chuo na maofisi.

Ila siri mojawapo ya biashara, usiingize hela yote kwa mara moja.
 
Hyo maabara unesomea n biashara nzur lkn usiifanye bila kufaNya research ya requirements zAke
 
Kaka 2 Na 3,itakutoa Kimaisha,maabara Mpaka Uwe Na Pharmacy hapa unaweza weka mpesa pharmacy inalipa sana tatizo vibali, Pia kwa maabara lazima Uwe Na Dr Ambae ataweza kuvuta wateja kwa umahiri wake,au mwenye jina hii takusaidi
 
As-salamu alaykum! Wazo namba 1 mpaka namba 5 yote ni mawazo mazuri, lakini kwa maono yangu wazo namba 4 ni ngumu kidogo kama siyo sana kulitekeleza kwa kiasi hicho ulichokitaja [ cha milioni 8 ] Labda chagua kuwekeza pesa yako kwenye mgahawa wa chakula, miamala ya kifedha, au duka la vyakula kwangu haya ni machaguo mazuri na ingelikuwa ni mimi kwa kiasia hicho cha shilingi milioni 8 ningelifungua mgahawa mkubwa wa chakula, kama member mwingine hapo juu alivyosema kwa maandishi mtu au watu lazima wale -- mtu anaweza asinunue nguo mwaka mzima, lakini kwenye kipande cha kula ni lazima ale tu. Mkuu, ikiwa mama n'tilie anapika ubwabwa kg 5 na kila kg 1 inatoa vibakuli zaidi ya 10; hapa unaweza kuona ni jinsi gani biashara hii inalipa, lakini changamoto zake pia ni kubwa . . . kila la heri mkuu!
 
Wekeza kwenye saluni unafungua ya kike na kiume sehemu moja zinakuwa ni classic saloon zenye wadhifa ..mgahawa wa chakula unalipa pia it just depend eneo na ulivobuni eneo lako watu siku hizi wanapenda kula maeneo hata kama sehemu padogo lakini pavutie hata kwenye kiselfie
True brother
 
As-salamu alaykum! Wazo namba 1 mpaka namba 5 yote ni mawazo mazuri, lakini kwa maono yangu wazo namba 4 ni ngumu kidogo kama siyo sana kulitekeleza kwa kiasi hicho ulichokitaja [ cha milioni 8 ] Labda chagua kuwekeza pesa yako kwenye mgahawa wa chakula, miamala ya kifedha, au duka la vyakula kwangu haya ni machaguo mazuri na ingelikuwa ni mimi kwa kiasia hicho cha shilingi milioni 8 ningelifungua mgahawa mkubwa wa chakula, kama member mwingine hapo juu alivyosema kwa maandishi mtu au watu lazima wale -- mtu anaweza asinunue nguo mwaka mzima, lakini kwenye kipande cha kula ni lazima ale tu. Mkuu, ikiwa mama n'tilie anapika ubwabwa kg 5 na kila kg 1 inatoa vibakuli zaidi ya 10; hapa unaweza kuona ni jinsi gani biashara hii inalipa, lakini changamoto zake pia ni kubwa . . . kila la heri mkuu!
Nashkuru sana kiongoz. Umenipa nguvu zaid ya uthubutu
 
Fanya pesa pesa hizi..! Mtaji unabaki palepale unless otherwise uibiwe..!
 
Kuna game ya liverpool na real madrid UCL jumamosi, bet hela yote 8M, liverpool itashinda bao 2-0 alafu uje unipe 10% ya faida
 
Habarini wana JF,

Baada ya kupambana kwa kipindi kirefu nimeweza kusave fedha kiasi mpaka kufikisha tsh million nane.Lengo la uzi huu ni kutaka kuwashirikisheni ndugu zangu hapa. Nina mawazo kadhaa ya kibiashara kulingana na eneo nililopo.

Lengo langu sasa ni angalau nipate ushauri which one is the best kati ya hayo mawazo niliyo nayo.

Mawazo hayo ni:
1. Stationery
2. Duka la vyakula/mangi
3. Mgahawa wa chakula
4. Maabara ndogo ya kupima afya
5. Kibanda cha miamala ya kifedha.

NB. Biashara zote nilizotaja hapo juu ninatamani kuongeza thamani kwa kuweka M- Pesa isipokua tu hiyo ya maabara.

KARIBUNI WAKUU.
[emoji115]
HIYO HELA IGAWE MAFUNGU MANNE MKUU.

1. CHUKUA MILIONI 3 FUNGUA STATIONERY.

2. CHUKUA MILIONI 3 INGINE FUNGUA DUKA LA DAWA MUHIMU,
HUKU UKIWA NA MALENGO YA KULIENDELEZA ILI MTAJI UKIKUA UFUNGUE MAABARA HAPOHAPO.

3. CHUKUA MILIONI 1 WEKA KWENYE BIASHARA YA MIAMALA YA PEASA,
AMBAYO UTAIFANYIA HAPO KWENYE OFISI YA STATIONERY.

4. MILIONI 1 IWEKE KAMA AKIBA YA DHARURA ZOZOTE ZA KIBIASHARA.

NB:
KUKIWA NA USIMAMIZI MZURI NA LOCATION NZURI KIBIASHARA
NI LAZIMA UTATUSUA.
 
Mawazo safi nimeyapenda
 
Back
Top Bottom